Chato wabadili muda wa kazi kwa watumishi wote; kufanya usafi asubuhi

kichomiz

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
19,002
11,929
Wakuu heshima mbele.

Mwenzenu katika mihangaiko yangu ya kusaka mkate wa kila siku,
Leo nimeshangazwa na sheria za wilaya ya Chato au sijui ni Tanzania nzima?na sijui hii sheria Bunge la JMT lilikaa lini na kuipitisha,nimeamka leo asubuhi mida ya saa 2:00 na kuelekea dukani kununua mswaki, nikashangaa kuona maduka yote yamefungwa.

Nilipouliza wenyeji wakaniambia hapa Chato kila alhamisi watu hawatakiwi kufanya shughuli zao mpaka ifike saa nne unusu,
Hali kadharika na usafiri ni hivyo hivyo, nilipouliza kwa nini nikaambiwa eti imeteuliwa kuwa ni siku maalum ya usafi.
Kwa sasa niko hapa halmashauri napo shughuli hazifanyiki, maofisi yamefungwa mpaka ufike muda husika,nilipohoji nikaambiwa hii ni sheria ya mkuu wa wilaya.

Na ukibainika unafanya kazi faini ni tsh 100,000: Na wanasema inamwezi mmoja sasa.

My take.

Je hiii sheria ni kweli ipo kwenye sheria za JMT au ni maamuzi binafsi?
Na je serikali haioni kama inapoteza mapato kwa kwa kupoteza masaa 4 ya kazi?
Je na hawa wafanya wanaosababishiwa hasara ya mapato yao,wanaweza kuwashitaki na kudai fidia?
Elimu ya uraia bado inahitajika sana maeneo kama haya.

Chanzo:
Mimi mwenyewe.
 
Mimi naona sawa tu kama ni sheria inayohusu Chato, jaribu kudadisi zaidi kama madiwani wa Chato walikaa wakakubaliana sheria hiyo iwepo. Miji mingi nchini ni mchafu, ili kujenga utamaduni wa kufanya usafi na kutotupa taka hovyo, inabidi kujiwekea taratibu kama hizo. Matunda yake utakuja kuyaona muda si mrefu!!
 
Huoni kwamba watu wanapoteza masaa mengi ya mapato?ni kwa nini wasingepanga siku ambazo si za kazi?
 
Kama wenyeji wa hapo wameona ni sawa....waache wakae siku moja watapata akili....

Na wao wanalalamika,saa hizi ndio wanaanza kufungua maofisi na wafanya biashara wanafungua biashara zao.
 
nadhani huwa kuna sheria ndogo ndogo ambazo either halmashauri au manispaa inaweza kujiwekea kufanikisha malengo yao, Lakini hili la mpaka sa nne is too much jamani! Inahitaji maboresho if at all is true
 
Mimi naona sawa tu kama ni sheria inayohusu Chato, jaribu kudadisi zaidi kama madiwani wa Chato walikaa wakakubaliana sheria hiyo iwepo. Miji mingi nchini ni mchafu, ili kujenga utamaduni wa kufanya usafi na kutotupa taka hovyo, inabidi kujiwekea taratibu kama hizo. Matunda yake utakuja kuyaona muda si mrefu!!
Hata siku moja huwezi ukalazimisha suala la usafi kwa nguvu. nitapita mwakani kushuhudia usafi wa chato uefikia wapi
 
Hata siku moja huwezi ukalazimisha suala la usafi kwa nguvu. nitapita mwakani kushuhudia usafi wa chato uefikia wapi

Cha kushangaza zaidi ni kufunga kazi kwa masaa manne na nusu,alafu ni kila alhamisi hii haijakaa sawa kabisa.
 
Haina maana kufanya kazi na kurundika uchafu bila kuuondoa na kuuchoma.
Ni sheria nzuri japo kwenye utekelezaji ndio kunaleta kizungumkuti
OTIS
 
Haina maana kufanya kazi na kurundika uchafu bila kuuondoa na kuuchoma.
Ni sheria nzuri japo kwenye utekelezaji ndio kunaleta kizungumkuti
OTIS

Lakini vipi kuhusu hayo masaa ya kazi?me naona ingekuwa nzuri kama wangeipanga siku ambayo si ya kazi.
 
Napenda kufahamu jambo moja muhimu, je ni amri kutoka kwa Mkuu wa wilaya au ni mapendekezo ambayo wananchi wameyapokea na kuyafanyia kazi kwa utaratibu waliojiamulia kwa vikao husika?

Kwa maoni yangu kutokana na tabia mbaya tuliyojijengea wa -TZ wengi(si wote) hatufanyi kitu kwa ridhaa zetu hasa usafi na utunzaji mazingira ndio maana miji/mikoa mingi ni michafu na maendeleo ni duni, ukiuliza kila mtu atatupa lawama sehemu/mamlaka fulani bila kujali yeye mwenyewe amewajibika vipi katika hilo.

Kuhusu muda wa kazi, kidogo hapo inatakiwa busara itumike kutokana na mazingira mahalia na shughuli zao za uzalishaji mali zikoje,ingawa nina wasiwasi kidogo kuwa sehemu nyingine utakuta mtu aneyelalamika ni mchezaji wa pool table kutwa nzima nje ya grocery fulani kama tulivyozoea kuwaona baadhi ya vijana ambao ndio nguvu kazi ya Taifa wanavyofanya sehemu nyingi ya nchi hii hivi sasa.
Otherwise Big up Mkuu wa Wilaya na jopo lako kwa maamuzi/amri sahihi kwa jamii husika.
 
Hizo ni taratibu walizojiwekea.. kwani wana chato wamelalamika? hata Tanga nakumbuka enzi za Kalembo kuna kipindi walikua na utaratibu kama huo sijui kama bado unaendelea
 
Jambo la kawaida, ukifika Rwanda wana siku maalum ya usafi hadi Rais anaukua mtaani kufanya usafi.
 
Napenda kufahamu jambo moja muhimu, je ni amri kutoka kwa Mkuu wa wilaya au ni mapendekezo ambayo wananchi wameyapokea na kuyafanyia kazi kwa utaratibu waliojiamulia kwa vikao husika?

Kwa maoni yangu kutokana na tabia mbaya tuliyojijengea wa -TZ wengi(si wote) hatufanyi kitu kwa ridhaa zetu hasa usafi na utunzaji mazingira ndio maana miji/mikoa mingi ni michafu na maendeleo ni duni, ukiuliza kila mtu atatupa lawama sehemu/mamlaka fulani bila kujali yeye mwenyewe amewajibika vipi katika hilo.

Kuhusu muda wa kazi, kidogo hapo inatakiwa busara itumike kutokana na mazingira mahalia na shughuli zao za uzalishaji mali zikoje,ingawa nina wasiwasi kidogo kuwa sehemu nyingine utakuta mtu aneyelalamika ni mchezaji wa pool table kutwa nzima nje ya grocery fulani kama tulivyozoea kuwaona baadhi ya vijana ambao ndio nguvu kazi ya Taifa wanavyofanya sehemu nyingi ya nchi hii hivi sasa.
Otherwise Big up Mkuu wa Wilaya na jopo lako kwa maamuzi/amri sahihi kwa jamii husika.

Mkuu we unaona ni sahihi kupoteza masaa manne na nusu ya kazi?uje utembelee haya maeneo uone usafi wenyewe.
 
Hizo ni taratibu walizojiwekea.. kwani wana chato wamelalamika? hata Tanga nakumbuka enzi za Kalembo kuna kipindi walikua na utaratibu kama huo sijui kama bado unaendelea

Hawajajiwekea ila wamelazimishwa,wangejiwekea wasingelalamika.
 
Wakuu hii ni sheria ambayo naona mkuu wa Mkoa Bw.Massawe ameamua kuiweka kwa mkoa mzima maana alianza nayo alipokuwa mkuu wa wilaya ya Karagwe na ilikuwa ni kwa wilaya hiyo tu. Kusema kweli usafi wa wilaya uliboreka sana maana unafanywa maeneo yote na kusimamiwa na viongozi wote wa mitaa/vitongoji/kata. Kwa suala hilo la muda hapo tunaweza kupendekeza upunguzwe.
 
kama inatekelezeka sio mbaya!
hawa potezi masaa manne kikawaida ofisi sinafunguliwa saa mbili na wateja kwa huduma nyingi zinaanza saa tatu hivy kiukweli kuna saa moja tu.
waache wajaribu na tuwapime kwa mafanikio yao kama yatakuwa wazuri tutaiga na kuboresha kwani miji ni michafu mno bila sababu
 
Taratibu zingine bana ni shida tu!Ndo maana tunazidi kuwa masikini cku hadi siku,hv masaa 4 na nusu bla kufanya kazi k.V biashara na kufungua ofisi ni hasara ya mapato ya mamilion,usafi ni jukum la kila mtu bila kulazimishwa,kwangu mm sheria kama hii haifai kwa mustakabal wa nchi yetu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom