Chatanda azua tena mvutano CCM, Chadema Arusha

WABUNGE na madiwani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), jana walisusa kushiriki uchaguzi wa Jumuiya za Serikali za Mitaa Tanzania (ALAT) katika Mkoa wa Arusha.

Walifikia hatua hiyo wakipinga uwepo wa Mbunge wa Viti maalumu kupitia Jumuiya ya Wanawake (UWT) wa Mkoa wa Tanga, Mery Chatanda katika mkutano huo.

Mbunge wa Jimbo la Karatu, Mchungaji Israel Natse ambaye alitaka ufafanuzi wa Chatanda kuwepo katika kikao hicho, kwa kuwa kanuni za Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) wabunge wanaopaswa kuhudhuria kikao hicho, ni wa Mkoa wa Arusha tu na sio vinginevyo.

Hata hivyo, Mwenyekiti wa muda wa mkutano huo, Ismail Katamboi ambaye ni Diwani wa kata ya Kisongo, katika Halmashauri ya Arusha, alisema Chatanda ni mjumbe halali wa kikao hicho na kutaka shughuli za kikao hicho kuendelea.

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Karatu, Lazaro Massay alisimama na kumtaka Katamboi kueleza kama Chatanda ni Mbunge wa Arusha ama Tanga.

Lakini Katamboi hakutaka kujibu swali hilo kama alivyotaka Massay bali alisisitiza kuwa Chatanga ni mjumbe halali wa mkutano huo wa Alat na hakutoa ufafanuzi zaidi.

Baada ya jibu hilo, Diwani Julius ole Sekayane (CCM) ambaye alimwakilisha Meya wa Jiji la Arusha, alisimama na kuwataka wajumbe kuendelea mkutano kwa kuwa Chatanda ni mjumbe halali katika mkutano huo na anayedai kuwa sio halali amekosea.

Baada ya malumbano hayo, wabunge wa Chadema, Natse wa Karatu na Mbunge wa Arusha mjini, Godbless Lema na madiwani wote wa Chadema waliondoka ndani ya ukumbi wakisema hawako tayari kushiriki uchaguzi huo.

Natse akizungumza nje ya ukumbi, alisema Chatanda sio mjumbe halali na pili wao wanaungana na wenzao kusema kuwa hawamtambui Meya wa Jiji la Arusha Gaudence Lyimo kwani hakuchaguliwa kufuata kanuni za Tamisemi.

Mkutano huo wa Alat Mkoa wa Arusha hushirikisha wabunge wote wa mkoa, wenyeviti wa halmashauri za wilaya, wakurugenzi wa halmashauri zote na madiwani wawili waliochaguliwa na baraza la madiwani la wilaya husika.

Mkutano huo ulikuwa wa kumchagua Mwenyekiti wa Alat mkoa wa Arusha, mweka hazina, kamati ya utendaji na mbunge mwakilishi wa mkoa katika mkutano mkuu wa Alat Taifa.

Mwenye Picha ya Sura Yake Tafadhali iwekwe hapa tumjue huyu beijing.
 
Mwenye picha ya Bi. Mary Chatanda naomba anipatie niione. Bila shaka kwa kui-study Picha nitajifunza mengi. Sijawahi kumwona physically au kwenye TV, hata nikikutana nae mahali nitashindwa kumfanyizia.
Wajameni naombeni picha ili niwe natembea nayo, na nikimkuta mahali popote ninamkata kelebu ya kiuno. Akiinuka ninamsindilia Konzi za Utosini.....afu najua ataanza kutukana....akipanua tu mdomo wako ....kosa, naondoa dental formula yote.
Wakati amechanganyikiwa asijue la kufanya, mi navamia MEWATA(matiti) nanyonya yote mpaka yaishe. Afu namalizia kwa kumkata teke la kurudi nyuma.
 
Keil,

Kama huyo mama anafaa kuwakilisha mkoa wa Tanga, je wabunge wa CHADEMA ambao hawakutumia utaratibu wa mkoa wanafaa kuwakilisha makundi gani?

Je ni sawa kwa CHADEMA ambayo ina wabunge viti maalum 30 nchi nzima kuwapangia 2 halmashauri ya Arusha au 2 halmashauri ya Hai? Wametumia vigezo gani kuwapangia hizo halmashauri?

Katiba iko wazi sana, hakuna wabunge viti maalum wanaowakilisha mikoa. Hata ukienda kwenye katiba ya CCM hakuna kitu kama hicho. Wabunge wanaotajwa ni wale wa majimbo na wale wanaoishi kwenye mkoa husika.

Je huyo mama angegombea kupitia kundi la Waremavu ndani ya CCM mungesema akawakilishe walemavu tu? Je angegombea kwenye kundi la vyuo vikuu, mungesema akawakilishi vyuo vikuu tu?

Nakubaliana na wewe kama huyu mama aligombea Tanga ndani ya CCM ina maana yuko karibu na huo mkoa au anaishi huko. Kikawaida hata mimi ningetegemea huyo mama atimize haki yake kama diwani huko Tanga. Lakini hapa kuna complications zingine, huyu mama alikuwa katibu CCM mkoa kabla ya Uchaguzi na anaendelea na kazi hiyo huko huko Arusha. Sheria inamruhusu kuchagua halmashauri ya kutumikia, mnataka achague mkoa ambao itabidi asafiri km karibu 500 kwenda kuhudhuria vikao, why?

CHADEMA ambao hawana utaratibu wa mikoa wana haki ya kuchagua wanakotaka, ila hawa CCM kwasababu wana utaratibu wa mikoa basi wabanwe kwenye mikoa yao. Sheria haiendi hivyo mkuu, ni wote wanaruhusiwa au hakuna anayeruhusiwa.

Pia Mamuya nafikiri sio mbunge. Alichaguliwa kugombea lakini hakupata kwasababu alikuwa chini kwenye list.
 
4945701.jpg
 
Mikanganyiko yote hiyo inatokana na ulimbukeni tu!!! Mbona mambo ya maana hatuigi wenzetu walioiva kidemokrasia na utawala bora? Hivi viti maalum ni ulimbukeni tu unaokotokana na watawala kukubali kila kitu kutoka nchi za magharibi hata ambayo yanayopendekezwa na viasasi tu vinavyodhani vinatufundisha demokrasia. "Tulikuwa tunazungumza hadi tulipofikia si kuamua tu bali kukubaliana hata kama ni chini ya mti" Mwalimu.
Katiba tunayoitaka si ya kutubebesha mizigo mikubwa wananchi wetu ili tu tuwapendeze wafadhili. Watufadhili kwa fedha siyo hata mambo ya kutumia busara tu. Oneni sasa hata wawakilisha hawa wa viti maalum hawajui kikweli kweli wanawakilisha na kuwajibika kwa nani, wamekuwa chanzo cha vurugu ,maana hawaeleweki vema.Wapigiwe kura kwenye majimbo kwa utaratibu mpya unaoeleweka .Utaratibu wa viti maalum ulieleweka ni utaratibu wa chama kimoja wakati huo.Tuachane nao.
 
Hawa wabunge wa viti maalumu waruhusiwe kuhudhuria vikao kwenye halmashauri yeyote watakayoichagua au kupangiwa na chama chao lakini wasiruhusiwe kuwa na nafasi ya kupiga kura kwenye vikao vya maamuzi, kura yoyote ya maamuzi ifanywe na madiwani na wabunge wa majimbo.

Tunaweza tukafika mahala chama chenye madiwani wachache kinapata nafasi ya kuongoza halmashauri kwa sababu tu yauwingi wa wabunge wa viti maalumu,m huo hautakuwa utawala wa wananchi. Kama kigezo cha wale waliochaguliwa mikoani ni sahihi, CCM wangeweza pia kuwasambaza wabunge wao wa viti maalumu waliochaguliwa kama viongozi wa UWT, wa vyuo vikuu, UVCCM, walemavu na NGO kwenye halmashauri ambazo wana madiwani wachache kama mwanza, Arusha, Hai na kushinda kama vile Chadema walivyofanya Hai, huko tunapokwenda nadhani utaratibu huu wa sasa utasababisha vurugu tupu kwenye chaguzi za Halmashauri.
 
wakina anna abdallah waliingia kupitia mlango wa NGO fulani hivi wakati hata watendaji wakuu wa hiyo NGO hawana habari..
 
Keil,

Je ni sawa kwa CHADEMA ambayo ina wabunge viti maalum 30 nchi nzima kuwapangia 2 halmashauri ya Arusha au 2 halmashauri ya Hai? Wametumia vigezo gani kuwapangia hizo halmashauri?
.

Kigezo kilichotumika ni kuongeza idadi ya madiwani ili kupata nafasi za kuziongoza halmashauri hizo.
 
Wabunge wa Viti maalum wasingeruhusiwa kupiga kura kwenye chaguzi zozote za halmashauri.
 
Mi nahisi nina tatizo na comment za wanaume hasa hapa JF,hivi hilo la kumnyonya matiti hadi yaishe,halafu anyonyeshe vipi au alichokosea yeye ni adhabu pia kwa mwanae.............whats the point?kuna sehemu nyingine za mwanamke ukiziongelea hivi ni udhalilishaji????wala sitaki matusi,nilishasema inawezekana nina tatizo,mwenye uwezo anisaidie si kunitukana.........
 
Hili jukwaa ni la Jokes mama! waweza andika chochote just for funny.
 
Nadhani tume ya uchaguzi ndo wenye jibu sahihi kwa maswali ambayo mimi najiuliza. Viti maalum anapangiwa na chama chake kwenda kufanya kazi katika jimbo fulani au inategemea na ukaribu wa jimbo ambo mbunge anaishi. Pia sijawasikia vigogo wa CDM, mf. Mbowe, slaa, zito wakipinga hili la chatanda kufanya kazi jimbo la arusha.
Kama walishasema, mniwie radhi sijasikia
 
MBUNGE wa Viti maalumu kupitia Mkoa wa Tanga, Mary Chatanda, amezusha balaa jingine baada ya wawakilishi wa madiwani na wabunge wa Chadema, kuamua kususia kikao cha Jumuiya ya Serikali za Mitaa (Alat) kwa kutoa nje.

Chatanda ambaye pia ni Katibu wa CCM mkoani Arusha, anadaiwa kuwa chanzo cha vurugu zilizosababisha mauaji ya waandamanaji waliokuwa wanapinga uchaguzi uliomweka madarakani Meya wa Jiji la Arusha.

Madiwani, wabunge wa Chadema akiwemo mwenyekiti wa Halmashauri ya Karatu, walipinga vikali kwamba Chatanda sio mjumbe wa kikao cha Alat kwa sababu, ubunge wake hautokani na Mkoa wa Arusha.

Tukio hilo lilitokea jana saa 5:00 asubuhi kwenye kikao kilichofanyika jengo la Mkuu wa Wilaya ya Arusha, wawakilishi sita Chadema waliamua kususia kikao hicho kilicholenga kuwachagua wawakilishi wa Alat Mkoa wa Arusha.

Viongozi wa Chadema kwenye kikao hicho waliosusa ni Mbunge wa Jimbo la Arusha mjini, Godbless Lema, Mbunge wa Karatu, Mchungaji Israel Natse, Diwani wa Viti maalumu wilayani Karatu, Cecilia Pareso na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu, Lazaro Massay.

Tukio hilo lilianza pale Mbunge wa Jimbo la Karatu, Natse aliposimama na kueleza ya kuwa Chatanda sio mjumbe halali wa kikao hicho kwa sababu, anatoka nje ya Mkoa wa Arusha, hoja hiyo ilipingwa vikali na Diwani wa Terat, Julius Sekeyan.

Wakati hali ya malumbano ikiendelea, Natse alisimamia msimamo wake huku akidai ya kuwa, wanaotakiwa kuwepo ndani ya kikao hicho ni wenyeviti wa halmashauri wa wilaya ndani ya Mkoa wa Arusha, wakurugenzi wa wilaya, wajumbe wawili wa kuchaguliwa na mabaraza husika na wabunge wa Mkoa wa Arusha.

“Mary Chatanda sio mjumbe halali katika kikao hiki, huyu anatoka Tanga sasa iweje leo tufanye uchaguzi wa viongozi wa Alat Mkoa wa Arusha, awe mpiga kura kwanini asiende kusubiri uchaguzi wa Tanga?” alihoji Natse

Wakati hayo yakiendelea, Chatanda alikuwa amekaa kwenye kiti chake, huku akionekana usoni mwake kama mwenye jazba na muda wote alikuwa akichezea simu yake ya mkononi.

Hata hivyo, viongozi wa muda ndani ya kikao hicho, akiwemo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha Vijijini, Halifa Hidda, waliamua kutoa ufafanuzi na kwamba, hata Chadema wakisusia wao wataendelea na uchaguzi kama kawaida.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti baada ya kutoka ndani ya ukumbi huo, baadhi ya wawakilishi wa Chadema wakiongozwa na Mchungaji Natse, walidai uamuzi wa kususia kikao hicho ulitokana na madai ya kupinga kitendo cha Chatanda kuwepo ndani.

Source: Mwananchi
 
Keil,

Kama huyo mama anafaa kuwakilisha mkoa wa Tanga, je wabunge wa CHADEMA ambao hawakutumia utaratibu wa mkoa wanafaa kuwakilisha makundi gani?

Je ni sawa kwa CHADEMA ambayo ina wabunge viti maalum 30 nchi nzima kuwapangia 2 halmashauri ya Arusha au 2 halmashauri ya Hai? Wametumia vigezo gani kuwapangia hizo halmashauri?

Katiba iko wazi sana, hakuna wabunge viti maalum wanaowakilisha mikoa. Hata ukienda kwenye katiba ya CCM hakuna kitu kama hicho. Wabunge wanaotajwa ni wale wa majimbo na wale wanaoishi kwenye mkoa husika.

Je huyo mama angegombea kupitia kundi la Waremavu ndani ya CCM mungesema akawakilishe walemavu tu? Je angegombea kwenye kundi la vyuo vikuu, mungesema akawakilishi vyuo vikuu tu?

Nakubaliana na wewe kama huyu mama aligombea Tanga ndani ya CCM ina maana yuko karibu na huo mkoa au anaishi huko. Kikawaida hata mimi ningetegemea huyo mama atimize haki yake kama diwani huko Tanga. Lakini hapa kuna complications zingine, huyu mama alikuwa katibu CCM mkoa kabla ya Uchaguzi na anaendelea na kazi hiyo huko huko Arusha. Sheria inamruhusu kuchagua halmashauri ya kutumikia, mnataka achague mkoa ambao itabidi asafiri km karibu 500 kwenda kuhudhuria vikao, why?

CHADEMA ambao hawana utaratibu wa mikoa wana haki ya kuchagua wanakotaka, ila hawa CCM kwasababu wana utaratibu wa mikoa basi wabanwe kwenye mikoa yao. Sheria haiendi hivyo mkuu, ni wote wanaruhusiwa au hakuna anayeruhusiwa.

Pia Mamuya nafikiri sio mbunge. Alichaguliwa kugombea lakini hakupata kwasababu alikuwa chini kwenye list.

maelezo mazuri sana. Hivi ndo inabidi tujibizane kwa ufahamu wa kanuni, mazoea n.k. Katika maelezo umesema sheria inaruhusu mbunge wa VM kuchagua halmashauri ya kutumikia, ni sheria gani hiyo mkuu?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom