Mkutano wa Majumuisho Katika Ziara ya UWT Taifa Mkoa wa Geita

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,898
943

UWT TAIFA WAFANYA MKUTANO WA MAJUMUISHO YA ZIARA MKOA WA GEITA

CHATANDA : VIONGOZI WA UWT MIKOANI TOKENI MKAFANYE ZIARA KWENYE MAENEO YENU, MKASIKILIZE NA KUTATUA KERO ZA WANANCHI​

Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake Tanzania UWT Mary Chatanda amewataka Viongozi wa UWT wa Mikoa na wa Mashina kuhakikisha wanafanya ziara kuonana na wananchi Kuwaambia kinachofanywa na Serikali ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ili wananchi watambue Serikali yao inavyoleta fedha kwa ajili yao.

Akizungumza leo katika Majumuisho ya Mkoa wa Geita Mwenyekiti Chatanda amesema

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania UWT Mary Chatanda, amewataka Wabunge wa viti Maalum kupitia umoja huo kufanya Mikutano na wananchi na Kufika katika Vijiji, vitongoji, kata ,wilaya na Mkoa

Akizungumza leo katika Kikao cha majumuisho mkoani Geita mwenyekiti Chatanda amesema Wabunge wengi wa Viti maalumu waache mfumo wa kuwafikia mabaraza wa wilaya na kugawa Masufuria bila kufika chini jambo ambalo sio sawa.

Chatanda amehitimisha ziara yake ya siku nane Mkoani Geita ambapo anatarajia kuanza ziara yake nyingine Mkoa wa Kagera kwa Siku tisa.

"Sisi UWT Taifa tumetoka kuonana na wananchi na nyie niwatake mwende mkaonane na wanawake wenzenu na wananchi kwa ujumla Kuwaambia nini kimefanywa na Serikali yao"

UWT IMARA JESHI LA MAMA KAZI IENDELEE
 

Attachments

  • WhatsApp Video 2023-10-01 at 18.29.22.mp4
    21.1 MB
  • WhatsApp Image 2023-10-01 at 18.47.15.jpeg
    WhatsApp Image 2023-10-01 at 18.47.15.jpeg
    73.1 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2023-10-01 at 18.47.40.jpeg
    WhatsApp Image 2023-10-01 at 18.47.40.jpeg
    56.1 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2023-10-01 at 18.47.41.jpeg
    WhatsApp Image 2023-10-01 at 18.47.41.jpeg
    53.3 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2023-10-01 at 18.35.38(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-10-01 at 18.35.38(1).jpeg
    63.3 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2023-10-01 at 18.35.36.jpeg
    WhatsApp Image 2023-10-01 at 18.35.36.jpeg
    77.6 KB · Views: 1

Similar Discussions

Back
Top Bottom