Mongoiwe
JF-Expert Member
- Feb 26, 2008
- 524
- 263
Hivi karibuni kumetokea mauaji ya watu watatu huko Arusha na wengine wengi kujeruhiwa, sababu imeelezwa kuwa ni Mbunge wa Viti maalumu kupitia Jumuiya ya Wanawake (UWT) wa Mkoa wa Tanga, Mery Chatanda.
Ni huyu Marya Chatanda ambaye amewataka Maaskofu kuvua majoho yao na kuingia katika siasa na ni huyu ambaye ametinga katika uchaguzi wa Umeya huku akijua yeye ni mbunge wa mkoa wa Tanga na siyo Arusha na kupiga kura za Umeya, kama haitoshi pia ametinga katika mkutano wa ALAT Arusha na kusababisha mtafaruku huko kama ule wa Umeya na Madiwani na wabunge wa Chadema kususia mkutano huo.
Je, huyu Mary Chatanda ni nani?
Pengine ni mtoto wa Katiba, ni mtoto wa kigogo ama mke wa Kigogo gani, ni muasisi wa chama ama taifa? Naomba msaada kwa wadau.