Chanzo cha mauaji ya mfanyabiashara ni hela

mtemiwao

JF-Expert Member
Sep 5, 2010
384
46
Wingu la sintofahamu kuhusu kifo cha mfanyabiashara wa madini aliyedaiwa na polisi kujiua mkoani Geita (runzewe) baada ya ndugu wa marehemu kukataa kuuzika mwili wa marehemu mpaka uchunguzi (postmortem) ufanyike na hela zinazokadiriwa 300m alizokuwa nazo nyumbani kwake zilichukuliwa na polisi zipatikane.

Mwili umekutwa na tundu mbili za risasi kichwani na tumboni kitu kinacholeta wasiwasi kama kweli alijiua.

Juhudi za RPC wa Geita kuwatisha wazike zimeshindikana na marehemu amekwamia Geita Hospital
 
Another case of 'rogue' elements in the police force? Who will investigate the police?
 
Kwa nini mtu unakaa na cash nyingi hivi nyumbani?? Milioni 300???

Hivi Geita hauna Benki?
Kutokana na aina ya biashara aliyokuwa anafanya hakuna cha ajabu hapo. Wafanyabiashara wengi wa madini huwa wanakuwa na pesa Kama hizo au zaidi nje ya mabenki. Ukiletewa mzigo usiku wa milioni 20 utafanyaje na huku mabenki yanakuwa yamefungwa. Mara nyingi hao wauzaji wadogo wadogo wanataka hela hapo hapo hamna habari ya njoo kesho uchukue hela.

Hamna cha ajabu kwa mfanyabiashara wa aina hiyo kuwa na kiasi Kama hicho nyumbani kwake au ofisini. Benki ni wasumbufu sana haswa mikoani...kuna watu wananielewa namaanisha nini hapa
.
 
Ni ulimbukeni tu, fikiria na yule wa Arusha aliyefanyiziwa hotelini ..........................!:nono:
Ni Ulimbukeni Kama hauna kitu unategemea mshahara. Ila kwa watu wenye hela zao ni kawaida sana kuwa na hela Kama hizo nyumbani mkuu. Usiogope mkuu,milioni 300 nyumbani kuna watu sio Issue...ni Kama sisi walala hoi kuwa na elfu 50 ya emergency nyumbani.
 
Kwa hiyo waliompiga risasi waweza wakawa ndio hao waliochukuwa 300 mil?
 
Ni Ulimbukeni Kama hauna kitu unategemea mshahara. Ila kwa watu wenye hela zao ni kawaida sana kuwa na hela Kama hizo nyumbani mkuu. Usiogope mkuu,milioni 300 nyumbani kuna watu sio Issue...ni Kama sisi walala hoi kuwa na elfu 50 ya emergency nyumbani.

Kwa karne hii hufai kufanya hivyo hata kama una hela zimejaa dunia nzima, sehemu ya kutunzia zipo zimejaa tele kwa nini ku - risk?
Ya nini na kwa mahitaji gani uweke 300 ml home?
 
Kutokana na aina ya biashara aliyokuwa anafanya hakuna cha ajabu hapo. Wafanyabiashara wengi wa madini huwa wanakuwa na pesa Kama hizo au zaidi nje ya mabenki. Ukiletewa mzigo usiku wa milioni 20 utafanyaje na huku mabenki yanakuwa yamefungwa. Mara nyingi hao wauzaji wadogo wadogo wanataka hela hapo hapo hamna habari ya njoo kesho uchukue hela.

Hamna cha ajabu kwa mfanyabiashara wa aina hiyo kuwa na kiasi Kama hicho nyumbani kwake au ofisini. Benki ni wasumbufu sana haswa mikoani...kuna watu wananielewa namaanisha nini hapa
.
nakuunga mkono mkuu,hata mimi siweki pesa bank
 
Jamani issue ya kuuwa kwa mwananchi kwa kisa cha kupora pesa yake tena kikifanywa na jeshi la polisi kwa usimamizi wa RPC si la kuleta mizaha eti kwa nini alikuwa na hela yote hiyo nyumbani.

Swala la Polisi kuua halafu RPC anawasaidia kutoa statment ya kuwasaidia wauaji eti mfanyabiashara aliamua kujiua eti baada ya kudhani ameua Polisi, inakuwaje mtu anayeamua kujiua ajipige RISASI MBILI sehemu tofauti za mwili yaani tumboni na kichwani na kisha pesa MIL.300 zipotee kwa sintofahamu wakati hapakuwa na majambazi?

Na kwa ushahidi wa wazi kuwa RPC amehusika ni pale alipotakiwa kutoa kauli baada ya Ndugu wa Marehemu kukataa kuzika na kujibu eti anapanga kutoa statment baada ya kujipanga na kupanga uongo leo saa 8 mchana. Hapa inaonekana katika hiyo Tsh. 300Mil na hivyo lazima adanganye Umma.

Ndugu zangu mimi binafsi linapokuja swala la kutegemea Wakuu wa Mapolisi Ma RPC kutoa kauli haraka haraka baada ya matukioa mie huwa siwezi kuamini haraka haraka, kumbukeni wakati wa tukio la Ditopile Mzuzuri kuuwa Konda wa Daladala, Tibaigana alisema kwamba Tiba alisema Dito alikuwa anajaribu kupiga piga kioo, pia kumbukeni hadi leo RPC Iringa bwana Kamhanda hadi leo anakula bata wakati alisimamia mauaji ya Mwangosi.

Kwa karne hii hufai kufanya hivyo hata kama una hela zimejaa dunia nzima, sehemu ya kutunzia zipo zimejaa tele kwa nini ku - risk?
Ya nini na kwa mahitaji gani uweke 300 ml home?
Sio kwa Bank system ya kiTanzania na Network issues. Hata iwe karne gani Tanzania bado tuko nyuma katika masuala ya Banking. Suala sio sehemu za kutunzia pesa Kibweka. Suala ni upatikanaji wa hela yako kwa haraka pindi utakapohitaji kwa emergency au suala la kibiashara.

Kama nilivyoelezea mwanzo Kutokana na aina ya biashara Marehemu aliyokuwa anafanya hakuna cha ajabu kuwa na pesa hiyo karibu. Tatizo letu Watanzania wengi tumezoea kukremu na kucopy mpaka kwenye maisha yetu ya kila siku...wakati system yetu hapa nchini haijafikia huko. Biashara ya madini sio Kama biashara ya kuuza nguo Kariakoo.
Mimi najaribu kuwasaidia ili muelewe kabla ya kuanza kujudge ulimbukeni wa Marehemu.
 
Ni Ulimbukeni Kama hauna kitu unategemea mshahara. Ila kwa watu wenye hela zao ni kawaida sana kuwa na hela Kama hizo nyumbani mkuu. Usiogope mkuu,milioni 300 nyumbani kuna watu sio Issue...ni Kama sisi walala hoi kuwa na elfu 50 ya emergency nyumbani.

Huo ndio ukweli halafu benki kuna ukiritimba mara hakuna network na mauzauza kibao,biashara zenyewe za papo kwa hapo je akipata dili siku ya jumapili au sikukuu? si atakuta mwana si wake.
 
Alikuwa anaitwa nani mkuu!
Wingu la sintofahamu kuhusu kifo cha mfanyabiashara wa madini aliyedaiwa na polisi kujiua mkoani Geita (runzewe) baada ya ndugu wa marehemu kukataa kuuzika mwili wa marehemu mpaka uchunguzi(postmortem)ufanyike na hela zinazokadiriwa 300m alizokuwa nazo nyumbani kwake zilichukuliwa na polisi zipatikane,mwili umekutwa na tundu mbili za risasi kichwani na tumboni kitu kinacholeta wacwac kama kweli alijiua..juhudi za rpc wa geita kuwatisha wazike zimeshindikana na marehemu amekwamia geita hospital
 
Huo ndio ukweli halafu benki kuna ukiritimba mara hakuna network na mauzauza kibao,biashara zenyewe za papo kwa hapo je akipata dili siku ya jumapili au sikukuu? si atakuta mwana si wake.

na hapo Bado haujaambiwa zaidi ya milioni kumi sijui mpaka ulipe kwa cheki au utoe taarifa masaa 24 kabla, au sijui mpaka iidhinishwe na meneja wa tawi au sijui kiasi hiki lazima ukachukue ulipofungulia akaunti, ili mradi kuchukua pesa benki ni mateso zaidi ya kuzitafuta!!!
 
Hivi kuna Mtanzania amabaye bado haamini kuwa jeshi letu la Polisi linaweza kushindwa kufanya hili?.Basi kama yupo huyo bado haijui Polisi ya Tanzania.
 
Nani alikuwa na marehemu kabla hajauwawa ambaye wali hesabu wote zile hela?acheni ushabiki wa ajabu ajabu,marehemu alimjeruhi polisi kituoni kwa hasira za gari lake kukamatwa,kisha akaimbilia kwake,alikuwa amelewa na confused,akaenda kwa jirani akakwapua combat,alipoona nyumba imezingirwa akajipiga risasi tumboni,mkewe aliruka na kumkumbatia akimbembeleza asijue,yeye aakmuamrisha mkewe aondoke mara moja ama sivyo atamuuwa,kitendo cha mkewe kumpa nafasi akajiongeza ya pili usoni.Suala la risasi mbili au tatu mwilini sio issue,inategemea amejipiga wapi.Kama angekuwa na matundu mawili ya risasi kichwani then hio ni habari nyingine,lakini tumboni alafu kichwani ni kitu cha kawaida.Mimi sitetei polisi ila tu nawashangaa mnajadili sana bila kuulizia maendeleo ya askari aliyepigwa risasi kadhaa na marehemu,bila shaka angeuwawa polisi mgesema ni sawa
 
Kova wa Dar es Salaa mpaka sasa yeye na askari wake wamejichimbia na mamilioni waliokomba pale Kariakoo itakuwa huyo wa Geita!! Polisi wa Kikwete ni majangili.
 
Back
Top Bottom