Chama cha waalimu chamshukia mbunge huyu.

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
Chama cha walimu
nchini CWT kimesema
kimebaini kuwepo
njama za siri za
kukisambaratisha
ambazo zinaratibiwa na
kikundi cha watu ambao
hawakuridhishwa na
mgomo wa walimu
ulioitishwa na chama
hicho hivi karibuni huku
kikiitaka serikali
kuwarudishia madaraka
wakuu wote wa shule
mbalimbali waliovuliwa
nyadhifa zao kutokana
na mgomo huo.
Rais wa CWT Gratian
Mukoba amemtaja
mbunge wa Sumve
Richard Ndasa kuwa
miongoni mwa watu
wanaopanga njama hizo
kutokana na madai yake
kuwa CWT inabakiza
zaidi ya shilingi bilioni 7
makao makuu kwa
matumizi yao binafsi
madai ambayo hayana
ukweli wowote.
Mukoba amesema
kutokana na tuhuma
zilizotolewa na mbunge
huyo, chama
kimewasilisha rasmi
malalamiko yake kwa
spika wa bunge
kikimtaka mbunge huyo
kuthibitisha hayo madai.
Kwenye line nyingine
Mukoba amesema “yani
mbunge Richard Ndasa
amesimama bungeni na
karatasi sijui
anaziokota wapi
anasema kwamba
chama cha walimu
kinabakiza bilioni 7
makao makuu akina
Mukoba wanagawana,
yeye kwanza hajui
mapato yetu kwa mwezi
ni kiasi gani, hajui hela
zetu zinagawanywaje
kwenda kwenye wilaya
mpaka kwenye shule,
hajui vitu ambavyo
vinafanywa na hela za
chama, anatamka tu
tena na karatasi
anajifanya anasoma”
Ishu nyingine ambayo
Mukoba ameizungumzia
ni kuhusu CWT
kutoridhishwa na
kitendo cha baadhi ya
wakuu wa mikoa na
wilaya kuwaondoa
walimu kwenye zoezi la
sensa ya watu na
makazi linalotarajiwa
kuanza usiku wa
kuamkia augost 26
2012.
Amesema “inaonekana
hayo ni maagizo kutoka
kwenye ofisi ya waziri
mkuu ambapo kabla ya
kuwaondoa serikali
iliorodhesha majina ya
walimu waliogoma na
viongozi wa CWT kwa
maelekezo yaliyotolewa
na Mwalimu Jumanne
Sagimi kaimu katibu
mkuu Tamisemi, mikoa
iliyoathirika sana na
zoezi hilo la Sagimi ni
Dar es salaam, Pwani,
Morogoro, Iringa n.k
ambapo walimu watatu
wa shule ya sekondari
Mererani waliondolewa
kwenye chumba cha
mafunzo ya sensa ya
watu na makazi kwa
maelekezo kuwa
walishiriki kwenye
mgomo”
Kuhusu hii ishu ya
walimu kuondolewa
kwenye sensa
nakumbuka Waziri
mkuu alizungumza
bungeni zaidi ya siku
tatu zilizopita kwamba,
toka mwanzo haikua
imepangwa walimu
pekee ndio
watasimamia zoezi la
sensa, sasa hivi kuna
vijana waliomaliza
elimu ya sekondari na
vyuo lakini hawana kazi
mtaani.
Unaaweza kumsikiliza
Mukoba hapo chini…
kwenye sauti ya kwanza
anamzungumzia huyu
Mbunge na sauti ya pili
anazungumzia walimu
kupigwa chini kwenye
tenda ya kusimamia
sensa
 
Back
Top Bottom