kada maarufu wa chama cha mapinduzi Njombe ambaye alikuwa katibu mwenezi wa kata ya Njombe mjini,Mjumbe wa kamati ya utekelezaji ya jumuiya ya wazazi wilaya ya Njombe pia mjumbe wa mkutano mkuu wa jumuiya ya wazazi Taifa Bwana Lupenza leo amejiondoa rasmi kwenye chama hicho.
Tukio hili ni kubwa kwa hapa Njombe kwani huyu ni moja kati ya makada maarufu wa chama cha mapinduzi waliokuwa mstari wa mbele kupambana na vyama vingine vilivyopo Njombe.
Kujiondoa kwa kada huyo ni ishara tosha kuwa mapigo ambayo yalifanywa na chadema kwenye uchaguzi wa udiwani hapa Njombe mjini yalikuwa ni makubwa kupita kiasi.
Mara baada ya uchaguzi kumalizika na ccm KUPOTEZA kwa kura nyingi kuliko sehemu yoyote Tanzania kumekuwa na vita kubwa ndani ya chama cha mapinduzi hoja kubwa ikiwa ni matumizi mabaya ya fedha za kampeni zilizotolewa na makada wa chama hicho kizee.
Inadaiwa kuwa wapo makada wa chama waliochukua fedha nyingi kwa ajili ya kampeni lakini hawakufikisha kwa wananchi jambo ambalo baadhi ya makada wa ccm hawakubaliani nalo na hivyo kutangaza nia ya kuhama chama.
Baada ya Lupenza kutangaza kujitoa katika chama hicho kuna taarifa za uhakika kuwa wapo pia viongozi wawili waandamizi wa chama hicho ambao wanatarajia kujitoa kuanzia tarehe 12.3.2014.
Kwa namna yoyote ili upepo wa chama cha mapinduzi hapa Njombe ni mbaya sana hasa kutokana na kuongozwa na viongozi wachovu kama chama chenyewe kilivyochoka na kukosa mvuto kwa wananchi.
Bwana Lupenza ametangaza uamuzi wake wa kujitoa ccm katika kituo cha Radio Uplands ya Njombe mjini.Pia ameahidi kujiunga na chama makini kabisa kilichopo hapa Tanzania bila kutaja ni chama gani.