Chama cha ADC chapata usajili wa muda

Dec 5, 2011
78
93
Nimemsikia msajili wa vyama vya siasa John Tendwa akisema rangi ya bendera ya chama kipya cha ADC ni sawa kabisa na za CHADEMA, bendera hizo zinatofautiana tu kwenye alama zilizopo
Great thinker hii imekaaje?
 
Yeye msajili angesema tu rangi ya ADC ni nyekundu, bluu bahari, nyeupe na nyeusi, bila ya kuitaja CHADEMA. Watu wenyewe wangegundua kuwa ni sawasawa na ya CHADEMA. Tendwa kutamka hilo ataonekana anataka kuibua hoja fulani. Jamaa huwa simuelewagi!
 
Nashangaa Tendwa kashindwa kufanya uamuzi wa kuikataa hiyo bendera!
Hawa jamaa wa ADC vitu vyao vingi ni vya kukopi!
 
Ni mbinu za CCM kutaka baadae kufoji ili kwenye mikutano ya ADC watakapokuwa wanapata watu kiduchu wao wapate nafasi ya kuwadanganya watu kwamba CDM kimekosa mvuto na kutoa picha za mikutano ya ADC wakionyesha na bendera zinazofanana na CDM kwenye magazeti yao Uchwara ya Jamba leo, Habari leo, Uharo, Mzalenda, Dailypuuzi n.k.
 
Yeye msajili angesema tu rangi ya ADC ni nyekundu, bluu bahari, nyeupe na nyeusi, bila ya kuitaja CHADEMA. Watu wenyewe wangegundua kuwa ni sawasawa na ya CHADEMA. Tendwa kutamka hilo ataonekana anataka kuibua hoja fulani. Jamaa huwa simuelewagi!
tendwa ni msahili sana, kila anolfanya linakuwa kuilenga CDM , huyu jamaa anatumika na magamba
 
Chama kipya cha Adc kimepata usajili wa muda baada ya kupeleka Manifesto yakea.source..chanel ten
 
Yeye msajili angesema tu rangi ya ADC ni nyekundu, bluu bahari, nyeupe na nyeusi, bila ya kuitaja CHADEMA. Watu wenyewe wangegundua kuwa ni sawasawa na ya CHADEMA. Tendwa kutamka hilo ataonekana anataka kuibua hoja fulani. Jamaa huwa simuelewagi!

watu wenye upara na wakawa na akili ni wachache sana. ni wa kuhesabu.
 
kuna mawili
1. CDM ni kiboko, mambo yake makubwa kila chama kitapenda kuyaiga au
2. Kuna jamaa wamejiengua ndani ya CDM na kuunda ADC hivyo mawazo yao bado yapo ki-CDM ki-CDM.
 
Hilo ni tawi la CCM na ndiyo maana wameamua kujifananisha na CDM kuanzia bendera mpaka sera eti walikuwa wanaimba katiba mpya.
 
Kuna vitu vingine vinakera sana. Hata mie sijawaelewa!

Ila Tendwa amesema kuwa endapo Chadema watalalamika basi hawa waliopata usajili leo ndio watatakiwa kubadili rangi za bendera yao.
 
Back
Top Bottom