Chakula cha mtoto 8 months

64Bits

JF-Expert Member
Aug 4, 2012
961
563
Naomba msaada wa mawazo maana i am running out of ideas. Nina mtoto wa miezi 8 anayesumbua kula. Namjaribisha vitu tofauti tofauti ila ni vichache sana anavikubali. Nikisema nimemjaribisha ni kwamba nimempa chakula hicho kama 5 times siku tofauti tofauti kagoma.

NB: mtoto nikimpa maziwa ya ng'ombe, formula milk na cerelac anatapika after approximately 1hr after kunywa. Soya milk inamtoa vipele mwili mzima.
Anakubali matunda yaliyosagwa, uji wa mahindi na mchele.

Ndizi, viazi anagoma unless unachanganya na parachichi asijue anakula nini. Im concerned that in a day anakula parachichi sana sijui kama ni healthy. Pia anaanza ku loose weight, sijui nijaribu vyakula gani vingine vinavyoweza kumjenga mwili.

Mara nyingine chakula chake huwa nachanganya na nyama au samaki for peotein na a bit of blue band for fats. Naomba mawazo yenu kwenye vyakula mbadala vinavyoweza kumjenga mwili. Asante
 
Kawaone madaktari pia wakusaidie labda wanaweza kumpa vitamins ambayo itaweza kumsaidia kuongeza appetite yake na hivyo kuongeza ulaji wake.
 
Swali,je mkimpa chakula mnachokula nyinyi wakubwa anakula au pia hapendi? Wangu alikataa vyakula vya kusagiwa lakin ukimpa hivi vyetu especialy ugali anakula vizuri tu,
Muhimu musimpe vyakula mnavyopenda nyinyi mpeni chochote ambacho anapenda na kula vizuri,matunda mjaribu ya aina yote uone yepi anapenda yepi hapendi
 
Nenda hospitali akapimwe allergy .Inaelekea ana lactose intolerance. Akifanyiwa test uhakika utapatikana.
 
Swali,je mkimpa chakula mnachokula nyinyi wakubwa anakula au pia hapendi? Wangu alikataa vyakula vya kusagiwa lakin ukimpa hivi vyetu especialy ugali anakula vizuri tu,
Muhimu musimpe vyakula mnavyopenda nyinyi mpeni chochote ambacho anapenda na kula vizuri,matunda mjaribu ya aina yote uone yepi anapenda yepi hapendi
Asante kwa mawazo yako. Ugali nimejaribu hapendi. Kuna siku nilipika ndizi za nazi akajaribu kidogo kesho yake nikampikia zake kidogo hakula. Wali wetu hawezi kutafuna bado so nampikia mchele wake laini kuna saa naufanya uji anakunywa na kuna saa naufanya mzito anakula na mchuzi. Wali anapenda. Ila ndo katika hivyo vichache anavyokula. Matunda anapenda mengi tu kama parachichi, embe, ndizi mbivu, papai kidogo, water melon na nanasi. Parachichi amekuwa anakula sana kwa kuwa naweza kulichanganya na chakula kama viazi ili ale some starch maana zaidi ya huo mchele na uji wa dona wenye karanga hakuna starch nyingine anayokubali kwa sasa. I tried oats, boga hadi mkate hapendi pia
 
Umri huo watoto hushika vitu vingi vichafu na kuweka mdomoni so angalia uwezekano wa kumpima minyoo. Avocado hupendwa na watoto wa age hiyo kwa kuwa ni laini na wanaona kama mchezo kuweka mdomoni tatizo akizidisha kula hayo anapata choo sana kama cha kuharisha so check asile sana hayo
 
64Bits Umesema anapenda uji wa mahindi na mchele, mpe huo huo tumia brown rice na mahindi usikoboe ukiweza tumia mahindi ya njano.

Kuna unga wa mchicha nafaka una virutubisho vyote vinavyohitajika na mwili wa binadamu hasa watoto kwa ukuaji bora. Unaweza ukatengeneza uji wake au ukachanganya na hivyo vyakula anavyovipenda. Unaweza ukaweka kama tui la nazi kwenye mchuzi wake ale na wali. Matumizi ni mengi ukigoogle GRAIN AMARANTH utajifunza zaidi.

Nimeshuhudia mabadiliko makubwa kwa watoto kama wanne baada ya wazazi wao kuanza kuwapa huo mchicha nafaka. Appettite iliongezeka na hata wakabadili tabia za kula. Hata watoto wangu ninawapa wataalamu wanasema ni mlo kamili.

Kama uko Arusha unapatikana makumbusho ya azimio la Arusha, unaweza wapigia simu 0786 970 700 au 0759 492 668. Do your research lakini
 
Last edited by a moderator:

Asante sana. Nipo arusha kidogo nitapita hapo aisee asante sana
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: Ilu

Similar Discussions

Back
Top Bottom