Faida 20 za Kula Parachichi

Aug 15, 2022
19
46
FAIDA ZA PARACHICHI
(Faida 20 za Kula Parachichi)

Parachichi ni aina ya kipekee ya tunda. Matunda mengi kwa asili ni wanga lakini parachichi limejaa mafuta yenye manufaa makubwa kiafya.

Tafiti mbalimbali zilizofanyika zimebaini kuwa tunda la parachichi limesheheni manufaa makubwa katika afya ya mwanadamu.

Ikiwa unapenda kuwa na afya bora kwa kula tunda la parachichi, basi karibu nikushirikishe faida 20 za kula tunda la parachichi.

1. Parachichi limejaa virutubisho mbalimbali
Parachichi ni tunda la pekee ambalo limebeba virutubisho mbalimbali ambavyo ni muhimu kwa ajili ya miili yetu. Baadhi ya virutubisho vinavyopatikana kwenye parachichi ni:

Kalori 240 (184 inatokana na mafuta)
Miligramu 11 za sodiamu
Gramu 13 za wanga
Gramu 10 za nyuzinyuzi za lishe
Gramu 1 tu ya sukari
Vitamini K: asilimia 26
Vitamini C: asilimia 17
Potasiamu asilimia 14
Vitamini B5: asilimia 14
Vitamini B6: asilimia 13
Asidi ya Folate: asilimia 20
Vitamini E: asilimia 10
Virutubisho vyote hivi ni muhimu kwa ajili ya mwili kujijenga na kujilinda dhidi ya magonjwa.

2. Lina virutubisho vitokanavyo na mimea
Pamoja na parachichi kuwa na virutubisho vingine mbalimbali, bado parachichi lina virutubisho muhimu tunavyovihitaji kutoka kwenye mimea. Virutubisho hivyo ni:

Carotenoids – Inayopatikana kutoka kwenye parachichi ina manufaa makubwa kwa ajili ya miili yetu katika kulinda macho dhidi ya matatizo mbalimbali yakiwemo yale yatokanayo na umri.

Persenones A na B – Hii huzuia uvimbe na saratani mwilini.

D-Mannoheptulose – Hii ni aina ya sukari inayopatikana kwenye parachichi, na inaaminika kusaidia kutawala kiwango cha sukari mwilini.

3. Husaidia kupunguza uzito
Swala la kupunguza uzito linaathiriwa sana na mfumo mzima wa lishe. Hivyo kula vyakula ambavyo vinawezesha mchakato wa metaboli kwenda vyema kutakuwezesha kupunguza uzito kwa muda mfupi.

Parachichi ni tunda zuri ambalo huwezesha mchakato wa metaboli kwenda vizuri mwilini.

4. Parachichi lina Fatty Acid

Fatty Acid ni asidi itokanayo na mafuta ya parachichi ambayo ni muhimu sana kwa ajili ya shughuli mbalimbali katika miili yetu.

Fatty Acid inahitajika katika uzalishaji wa homoni, ukuaji wa seli pamoja na ufyonzwaji wa virutubisho.

5. Hupunguza lehemu mbaya (cholesterol)
Mafuta ya lehemu ni hatari ikiwa kiwango chake kitakuwa kingi mwilini; mafuta haya husababisha matatizo mbalimbali hasa maradhi ya moyo.

Matunda ya parachichi hayana lehemu mbaya inayoweza kuathiri afya yako. Utafiti unaonyesha kuwa watu wanaokula parachichi kiwango chao cha lehemu mwilini ni tofauti na wale wasiokula kabisa.

6. Kukabili maradhi ya kisukari
Parachichi ni tunda ambalo kiwango chake cha sukari hakina athari kwenye mwili. Hivyo utumiaji wa parachichi utakuwezesha kuweka kiwango cha sukari mwilini kuwa katika hali nzuri ya wastani.

7. Hulinda afya ya moyo
Madini ya potasiamu yanayopatikana kwenye tunda la parachichi kwa zaidi ya asilimia 14 ni muhimu sana katika utendaji kazi wa misuli ya moyo.

8. Huzuia uvimbe
Asidi ya Oleic inayopatikana kwenye parachichi, imebainishwa na wataalamu kuwa husaidia kwa kiasi kikubwa kuzuia uvimbe mwilini.

9. Hulinda afya ya macho
Kemikali ya lutein na zeaxanthin ni muhimu sana kwa ajili ya kulinda na kuimarisha afya ya macho.

Ikumbukwe kuwa parachichi ni tunda lenye kiasi kikubwa cha lutein ambayo pia hulinda macho dhidi ya matatizo mbalimbali yatokanayo na umri.

10. Parachichi lina Potasiamu nyingi kuliko ndizi
Watu wengi wanapenda ndizi kwa kuwa ni chanzo kimoja wapo cha madini ya potasiamu, lakini hawafahamu kuwa ndizi ina potasiamu asilimia 10 na parachichi lina asilimia 14. Hivyo parachichi ni bora zaidi.

Potasiamu ni muhimu katika miili yetu kwani hutuwezesha kutawala kiwango cha sodiamu katika miili yetu na kutuepusha na madhara yatokanayo na madini haya ya sodiamu.

11. Huboresha afya ya nywele na ngozi
Naamini umewahi kusikia kuwa parachichi hutumika kutengenezea mafuta ya nywele na ya ngozi; hii ni kutokana na kusheheni vitamini E ambayo ni muhimu kwa ajili ya afya ya nywele na ngozi zetu.

Hivyo badala kununua mafuta ya gharama kubwa ili kupata vitamini E kwa ajili ya ngozi na nywele zako, basi kula tunda la parachichi sasa.

12. Huzuia saratani
Tafiti zilizofanyika zimebainisha kuwa kula matunda ya parachichi kunasaidia kupunguza kasi ya ukuaji wa seli za saratani ya tezi dume.

Hata hivyo, tafiti juu ya swala hili siyo nyingi sana lakini bado unaweza kula parachichi na kupata faida nyingine kemkem.

13. Huimarisha mifupa
Kutokana na parachichi kuwa na vitamini K pamoja na madini ya kopa na folate ambavyo ni muhimu kwa ajili ya mifupa, tunda hili linakuwa na nafasi kubwa katika kuimarisha mifupa.

14. Huboresha mmeng’enyo wa chakula
Vyakula vyenye nyuzinyuzi ni muhimu sana kwa ajili ya kuufanya mmeng’enyo wa chakula uende vizuri. Parachichi ni tunda lenye nyuzinyuzi kwa karibu asilimia 13 ambazo ni sawa na kiwango cha asilimia 54 unachotakiwa kula. Je bado huoni umuhimu wa tunda hili? Anza kula ili uboreshe mmeng’enyo wako wa chakula sasa.

15. Ni muhimu kwa wajawazito
Kuwepo kwa kiasi kikubwa cha folate, potasiamu, Vitamini C na B6 ambazo ni muhimu kwa ajili ya afya na ukuaji wa mtoto; kunalifanya tunda la parachichi kuwa na umuhimu mkubwa kwa wajawazito.

Hivyo inashauriwa wanawake wajawazito wazingatie ulaji wa matunda hasa tunda la parachichi.

16. Huimarisha kinga ya mwili

Kinga ya mwili hutegemea vitamini B, C na E ili kujiimarisha na kujijenga. Hivyo ulaji wa parachichi utaimarisha kinga ya mwili yako kwani parachichi limesheheni vitamini B, C na E.

17. Huboresha afya ya ubongo
Madini ya kopa yanayopatikana kwenye parachichi kwa zaidi ya asilimia 19 yana nafasi kubwa sana katika kuufanya ubongo ufanye kazi vyema.

Hivyo basi, ukitaka kuweka afya ya ubongo wako katika hali nzuri na kuweza kufikiri vyema, basi kula tunda la parachichi mara kwa mara.

18. Huboresha ufyonzwaji wa virutubisho
Baadhi ya virutubisho hufyonzwa kunapokuwa na mafuta (fat soluble); virutubisho hivyo ni kama vile vitamini A, E, D na K.

Kula parachichi kutawezesha virutubisho hivi kufyonzwa vyema mwilini.

19. Hukuweka katika hali nzuri (mood)
Baadhi ya tafiti zimeeleza kuwa watu wenye msongo wa mawazo wana upungufu mkubwa wa madini ya potasiamu.

Kwa kuwa parachichi ni chanzo kikubwa cha madini ya potasiamu, basi tunda hili linaweza kusaidia sana kukuweka katika hali nzuri.

20. Huongeza nguvu za mwili
Miili yetu inategemea sana wanga, protini na mafuta ili kupata nguvu. Ni wazi kuwa sasa unafahamu kuwa tunda la parachichi ni chanzo kikubwa cha virutubisho hivi vitatu.

Hivyo kuongeza parachichi katika mlo wako kutakuwezesha kuuongezea mwili wako nguzu zaidi.

Neno la mwisho:

Naamini sasa hutopuza tena tunda la parachichi kwani umefahamu faida tele za tunda hili. Parachichi ni tunda linalopatikana kwa urahisi bila gharama kubwa ikilinganishwa na matunda mengine kama vile tofaa (apple).

Fanya matunda kuwa sehemu ya mlo wako sasa hasa tunda la parachichi ili uwe na afya njema. Je wewe huwa unakula parachichi kwa kiasi gani?

74b7b430-7d2d-11ed-90a7-556e529f9f89.jpg

9c2b5c30-7d26-11ed-90a7-556e529f9f89.jpg

9b877e40-7d2a-11ed-90a7-556e529f9f89.jpg
 

Attachments

  • 1683766090973.gif
    1683766090973.gif
    42 bytes · Views: 45
Tunda langu pendwa.... Mpaka sokoni wamenikariri mm nanua parachichi tu
hili ndo tunda sikulipenda toka udogoni yani kiasi kwamba kama nimeshiba sana halafu atokee mtu mbele yangu anakula parachichi basi nitapatwa na hali ya kutapika,marehemu mama yangu alikua analipenda sana na alinambia nijilazimishe kula sababu lina faida nyingi lkn kila nilipojaribu niliishia kuhisi hali ya kutapika.mimi usiku huwa nakula matunda tu kisha ndo nalala,nakumbuka mwaka jana kuna mtu alinunua na kula mbele yangu nikajikuta nakumbuka kauli ya mama nikajiapiza kimoyomoyo huu mwaka hautaisha lazima nilipende hili tunda.kwasababu sipendi ladha yake mwanzoni nikawa nakula nikiwa na njaa sana pamoja na ndizi mbivu yaani ratiba ya chakula mchana nikaifuta ili usiku niwe na njaa sana niweze kula, njaa ikiwa kali hata usichopenda utakula tu,nimejikuta naizoea ladha yake taratibu mpaka nakula pekee bila ndizi na mpaka kufikia hatua ya kukaa namba moja kwenye matunda yangu pendwa sasahivi hunambii kitu kuhusu parachichi
 
hili ndo tunda sikulipenda toka udogoni yani kiasi kwamba kama nimeshiba sana halafu atokee mtu mbele yangu anakula parachichi basi nitapatwa na hali ya kutapika,marehemu mama yangu alikua analipenda sana na alinambia nijilazimishe kula sababu lina faida nyingi lkn kila nilipojaribu niliishia kuhisi hali ya kutapika.mimi usiku huwa nakula matunda tu kisha ndo nalala,nakumbuka mwaka jana kuna mtu alinunua na kula mbele yangu nikajikuta nakumbuka kauli ya mama nikajiapiza kimoyomoyo huu mwaka hautaisha lazima nilipende hili tunda.kwasababu sipendi ladha yake mwanzoni nikawa nakula nikiwa na njaa sana pamoja na ndizi mbivu yaani ratiba ya chakula mchana nikaifuta ili usiku niwe na njaa sana niweze kula, njaa ikiwa kali hata usichopenda utakula tu,nimejikuta naizoea ladha yake taratibu mpaka nakula pekee bila ndizi na mpaka kufikia hatua ya kukaa namba moja kwenye matunda yangu pendwa sasahivi hunambii kitu kuhusu parachichi
Haloooo.... Ulipate la Moshi yan Parachichi kama yai vile ndani nyieeeeeeee..
 
Back
Top Bottom