CHADEMA yawatahadharisha Uzini

abdulahsaf

JF-Expert Member
Aug 31, 2010
858
130


na Nasra Abdallah, Zanzibar

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimewataka wakazi wa jimbo la Uzini, kutokubali kuwa kama kuku wanaorushiwa mahindi pindi wanapotakiwa kuchinjwa.

Wito huo ulitolewa na Mkurugenzi wa Uchaguzi na Kampeni wa chama hicho, Msafiri Mtemelwa, katika mwendelezo wa kampeni zao ambapo juzi walifanya mkutano wa hadhara katika Shehia ya Umbuji na Miwani.

Mtemelwa alisema mahindi anayozungumzia ni kanga, mchele na fulana ambazo zimekuwa zikitolewa na CCM ili kuwashawishi kukipigia kura chama hicho halafu uchaguzi unapokwisha wanawasahau kabisa.

Alisema enzi za kudanganyika na vitu vya aina hiyo vimepitwa na wakati na kuongeza kwamba wananchi kwa sasa wanatakiwa kuangalia mustakabali wa maisha yao na vizazi vijavyo kwa kuwa vitu wanavyopewa hutumika ndani ya muda mfupi.

Naye mbunge wa viti maalum Pemba, Raya Ibrahim, alisema kitendo cha CCM kuwaletea wananchi wa Uzini mgombea ambaye si mzaliwa wa jimbo hilo ni matusi makubwa kwao.

Raya alisema kitendo hicho kimejenga picha mbaya kwa wananchi kwamba jimbo hilo halina watu wanaofaa kuongoza au waliosoma; kwamba itamuwia vigumu kiongozi wa namna hiyo kuwakumbuka wananchi waliomchagua.

Naye Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Hamad Musa Yusuph, alisema kwa mwaka huu wamejipanga vilivyo na hawatakubali kuchakachuliwa kura zao kama ilivyokuwa kwa uchaguzi uliopita.

 
Tatizo kubwa la watu wa visiwani ni kupenda ubwabwa wa bure!
 
Tatizo la cdm bla bla nyingi haf mwisho wa cku mnalia kuibiwa kura, kazeni buti mcje mkaleta nyimbo za igunga bana ebo!
 
Kwel mfano wa kuku iddir fitr then ukimla basi.tuweni punda basi wazanzibar ili hata wakitupata mateke tumewapa.
 
Haina maana kuishi umepiga magoti, heri ufe umelala. Wana Uzini umefika wakati wa kusema HAPANA CCM na HAPANA CCM B,putueni muwakombee wazanzibari
 
Wako kwenye kampeni au kwenye shughuli za kutambulisha Chama? Maana CHADEMA kwa Zanzibar ni Chama kipya!
Kweli we kenge kwenye maji ambaye haelewi mambo yanavyoendelea, CDM si chama kipya ZNZ kinajulikana sana na kina wanachama, hivyo subiri matokeo uone......!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom