Chadema yatoa masharti kurudi bungeni

Acha u sisiemu! wameingia bungeni ili kutetea wananchi, na wananchi wengi ambao ni vijana kama sisi tunaitaji katiba mpya coz sheria nyingi za nchi zilizopo sasa IVI ni za kizamani, i mean hazitushilikishi sisi vijana wa kisasa zinaitaji marekebisho.kama hakitaeleweka sasa ivi ujue hata 2015 itakuwa ivyo ivyo, ''DIFFERENT DAYZ SAME MO' SHIT''

Wananchi walio wengi wangekuwa wanakubaliana na matakwa ya Chadema, wangedhihirisha hilo kwakuwapa viti vingi vya Ubunge.

Sheria zipi ambazo hazikupi nafasi wewe kijana wa kisasa?

Marekebisho ya katiba ni kweli yanahitajika, ila hayawezi kuja kwa hoja za nguvu; yanahitaji busara na nguvu za hoja. Halafu natoa tena angalizo kuwa, hata katiba iliyopo sasa hakuna mahali imeandikwa kuwa mgombea mwenye kura chache anaweza kutangazwa mshindi wa uchaguzi.Hivyo basi, kama kuna mgombea amepata upendeleo huo, hiyo ni kinyume cha katiba; yaani katiba na sheria hazijaheshimiwa. Hii ni kusema kwamba hata ukiiandika katiba nzuri vipi, iwapo viongozi watakuwa na hulka za kutokuheshimu sheria basi matatizo kwenye chaguzi yataendelea kuwepo.
 
Ninavyoelewa wanataka kumweleza kikwete tatizo la katiba ila hawajagoma kuingia bungen hii itasaidia sana
 
nimesoma hiyo thread vizuri bt cjaona kama mbowe ametoa masharti ya kurudi bungeni bali ameeleza nini kifanyke kurekebisha mapungufu na kuelekea uchaguzi huru na wa haki. navyo vinawezekana tu kwa kuwana katiba mpya iliyotungwa nawatanzania na sio waingereza. habari leo wmwpotosha kwa kuwaka heading isiyoendana na maelezo ya ndani. nashindwa kutifautisha habari leo na magazeti kama ya uwazi, ijumaa,
Kama linapotosha habari tulisusie wabaki wanasoma wenyewe tuone nani zaidi msomaji au mhariri.
 
Mtoa mada amefix kichwa cha mada husika kwa malengo yake binafsi au hakuelewa vizuri kilicho elezwa na mbowe.
 
Ili waingie bungeni wanatoa masharti?
Ili waingie bungeni walichohitaji ni kura za wananchi.
Maana ya demokrasia ndio hiyo, huwezi kulazimisha Bunge au serikali kufanya mambo kwenye majukwaa ya kisiasa wakati wewe ni mbunge, kaliongeeni bungeni. Kama kura zenu Bungeni hazitoshi, changamoto ni kutafuta kura hizo kwenye chaguzi zijazo.
Hii ya kusema hamuingii Bungeni mpaka mtekelezewe masharti, ni hysteria.
Na mtawaangusha waliowapigia kura kwa kiasi kikubwa kwa sababu hamjawaambia kuwa kususa ndicho mnachoenda kufanya.
Kuzitafuta vipi hizo kura?
Kwa Uchaguzi kusimamiwa Tume hii hii inayochakachua?
Wewe ndio somo hulielewi kabisa! Pole
 
Kuzitafuta vipi hizo kura?
Kwa Uchaguzi kusimamiwa Tume hii hii inayochakachua?
Wewe ndio somo hulielewi kabisa! Pole

Kwani zile kura zilizowapa wabunge 23 wamezitafuta vipi?Kulikuwa na tume tofauti kwenye majimbo hayo?
 
Tume huru ni kwa manufaa ya nani ! lets be realistic and rational, CDM concern are first line national interest. Let rally behind this and see to our new generation equal/fair participation in leading TZ to a prosperity future.
 
Back
Top Bottom