Chadema yatoa masharti kurudi bungeni

Sina uhakika kama jitihada hizi zipo kwenye mstari...................njia mwafaka ni kuyadai hayo yote Chadema wakiwa bungeni na wakishindwa huko ndiyo warudi kwa wapigakura kuwaelezea madhara ya CCM kulihodhi bunge .................lakini nje ya bunge Chadema is playing into CCM's deceitful hands...................CCM will be happy..... if Chadema kicks itself out of the House....................Chadema watajinyima nafasi ya kuikosoa serikali na hivyo hoja ya kutwaa dola mwaka 2015...............What a waste!!!!!!!!!!...........
 
ILI waingie bungeni, wabunge wa Chadema wameweka masharti ambayo yakitekelezwa na Serikali watakuwa hawana tatizo tena.

Masharti hayo kwa mujibu wa Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe ni Serikali kutoa tamko kuhusu hoja yao ya kutungwa Katiba mpya, kuundwa kwa Tume Huru ya Uchaguzi na kutoa msimamo juu ya madai ya kukiukwa kwa taratibu za uchaguzi mkuu wa hivi karibuni.

Katika mahojiano maalumu na HABARILEO jana, Mbowe alisema: “Matendo ya leo yanaleta matukio ya kesho.

Suala la msimamo wetu kushiriki vikao vya Bunge lijalo utategemea na mapokeo ya hoja zetu.

“Kwa sisi kugomea hotuba ya Rais, tunajua ujumbe wetu umefika kwa wahusika wakiwamo bwana mkubwa mwenyewe (Rais Kikwete), viongozi wa mashirika na taasisi mbalimbali na mabalozi, kuonesha kuwa kuna tatizo la msingi ambalo Chadema inataka lishughulikiwe.

“Tunajua kuna watu wameudhika, na tunajua kuwa hatukumfurahisha Rais, lakini ujumbe wetu umefika.

Kuna baadhi ya watu wamepotosha kuwa tunampinga Rais. Haikuwa nia yetu kutaka avuliwe urais au aondolewe ofisini, tulitaka aone kuwa kuna tatizo ambalo linatakiwa kushughulikiwa na yeye ndiye mhusika.”

Mbowe alisema hoja ya kwanza ya Chadema ni kuona umuhimu wa kuwa na Katiba mpya
itakayoliwezesha Taifa kujenga misingi imara ya demokrasia na kuifanya nchi kuwa na amani, itakayokalika na kila mtu bila kujali kabila, dini au chama chake cha siasa.

“Tunataka Katiba ambayo itamfanya kila Mtanzania aishi kwa amani na upendo, mfano mzuri ni Zanzibar, walikuwa na tatizo kama hilo lakini sasa wamelishughulikia, kwa kuwa na Katiba nzuri na wamekubaliana kuendesha mambo yao … si unaona kila mtu anafurahia hili na wote wanaishi kwa amani kabisa?” alihoji.

Mbowe alisema kilio chao cha pili ni kuundwa kwa Tume ya Uchaguzi iliyo huru ili kufanya uchaguzi ujao usiwe na dosari.

“Ndiyo uchaguzi umekwisha, lakini tunataka Tume ya Uchaguzi iliyo huru, hatutaki kasoro zilizojitokeza uchaguzi huu zijitokeze katika uchaguzi mwingine, hatutaki Tume ambayo mpaka watu waandamane au wakeshe ndipo watangaze matokeo

Alisema hoja ya tatu ni kuundwa kwa Tume huru itayochunguza malalamiko yao kuhusu kasoro zilizojitokeza kwenye uchaguzi mkuu na kutoa mapendekezo ya kufanyiwa kazi dosari zitakazokuwa zimebainishwa.

“Tuna madai ya msingi kabisa, na tumetumia njia hiyo ili kufikisha ujumbe wetu kwa kufuata taratibu na tumewasilisha kilio chetu kwa amani kabisa, hatujatukana mtu, lakini baadhi ya watu wanatubeza na wengine wanasema tuundiwe azimio la kufukuzwa bungeni, sijui kama wanaelewa taratibu na kanuni.”

Aliongeza: “Katika vipaumbele 13 vilivyotolewa na Rais, hatujasikia suala la marekebisho ya Katiba ambalo limekuwa likilalamikiwa kwa takribani miaka 15 sasa, na hakuna hatua inayochukuliwa, sasa tunataka haya tunayoyadai yawemo kwenye hivyo vipaumbele.

Alhamisi iliyopita, wabunge wa Chadema waliondoka kwenye ukumbi wa Bunge mara baada ya Rais Kikwete kuanza kuhutubia kwa mara ya kwanza tangu kufanyika uchaguzi mkuu, Oktoba 31.

Akizungumzia madai ya kuwapo mgawanyiko ndani ya Chadema, katika kufikia uamuzi huo wa kususia hotuba ya Rais, Mbowe alisema uamuzi huo ulipitishwa ndani ya kikao cha chama hicho.

“Uamuzi ule umetokana na kikao halali cha chama, katika masuala kama hayo, si lazima watu wote wakubali na diyo maana unaweza kufikia hatua ya kupiga kura, lakini mwisho wa yote uamuzi wa wengi ndio unaofuatwa
Mheshimiwa Mbowe pole sana, hivi unafikiri haki huja ndani ya sinia? kama haluwa, haki Hupiganiwa, CCM ni Mavuvuzela hawasikii maneno wanataka Vitendo.Mwenyekiti Nguvu ya Umma ndio dawa pekee yahawa CCM Kuhesahimu haki za Watu. vyenginevyo msitarajie kwa ulioyataka kama hata utajibiwa zaidi utabezwa na kukejeliwa na hasa kwakuwa tayari asubuhi mshaonyesha kutokubaliana ndani ya Chama chenu huo ni Udhaifu Mkubwa sana Kusiasa kwani hamjapea hata kidogo, maamuzi ya kikao leo yamo Magazetini tena Mtowaji ni Naibu Katibu Mkuu? inasikitisha Tafadhalini sana sana Msitufanyie Usaniii na Kutuchezea SINEMA sisi Tuna matazizo Mengi ambayo tunahisi nyie tuliowapa KURA Mutatusimamia Vyenginevyo Tutakupigeni kwa MAWE na Kukuondoweni katika Chama.
 
kudai katiba mpya, tume huru ukiwa nje ya bunge ni jambo linalotia mashaka utashi wao wa kisiasa. Wametoa kama masharti ili warudi bungeni.
 
Katika vipaumbele 13 vilivyotolewa na Rais, hatujasikia suala la marekebisho ya Katiba ambalo limekuwa likilalamikiwa kwa takribani miaka 15 sasa
Kweli ni jambo la kushangaza sana kuwa kiini cha matatizo mengi yanayolikabili taifa hivi sasa ni Katiba. lakini kiongozi wa nchi haonyeshi kuwa kama hilo ni tatizo, hata kwa kusema kuwa wameliona. Tuna safari ndefu kufikia maendeleo kwa mwendo huu
 
kudai katiba nje ya bunge. Tume huru ni kupoteza lengo mahsusi la chama. Bunge ndio sehemu ya kutunga sheria. Kesho watakuja na lingine.
 
kudai katiba nje ya bunge na kuunda tume huru ya uchunguzi kuhusu uchaguzi. Yametolewa kama masheriti ndio warudi bungeni.
 
Ogopa binadamu akipewa ujumbe unasema "kesho"aupeleke kwajirani na jirani ausambaza kwanjia hiyo basi ujue kama walikuwa kumi basi huo ujumbe utfika tofauti nausishangae ukifika unasomeka"kesha"badala ya kesho!! Hivyo watu walivyo inukuu chadema na m/kiti alivyo sema nitofauti!
 
Chini ya utawala wa CCM hakuna kitakacho badilika!! hakuna tume huru ya uchaguzi wa katiba. Mambo hayo yatawezekana tu kama CCM itakuwa chama cha upinzani au kuwepo kwa shinikizo kubwa sana kutoka kwa wananchi. Lakini uelewa wetu watanzania ni mdogo sana.Kitendo cha wabunge wa CHADEMA kinaonekana hakikupata support kubwa ya wananchi, kama nilivyowahi kusema CCM inapima 'upepo' kuhusu swala la CHADEMA, je wananchi wanamtazamo gani. na sasa CCM imeshaona kuwa wananchi wengi hawajawasupport hivyo madai yao japo ni ya msingi lakini hayatasikilizwa.
 
Habari leo ni Watz wa jana na hawataki kuwepo leo na kesho. Hatukubali propaganda za kishenzi maana tulishaona mengi ya kishenzi
 
ILI waingie bungeni, wabunge wa Chadema wameweka masharti ambayo yakitekelezwa na Serikali watakuwa hawana tatizo tena.

Masharti hayo kwa mujibu wa Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe ni Serikali kutoa tamko kuhusu hoja yao ya kutungwa Katiba mpya, kuundwa kwa Tume Huru ya Uchaguzi na kutoa msimamo juu ya madai ya kukiukwa kwa taratibu za uchaguzi mkuu wa hivi karibuni.

Katika mahojiano maalumu na HABARILEO jana, Mbowe alisema: “Matendo ya leo yanaleta matukio ya kesho.

Suala la msimamo wetu kushiriki vikao vya Bunge lijalo utategemea na mapokeo ya hoja zetu.

“Kwa sisi kugomea hotuba ya Rais, tunajua ujumbe wetu umefika kwa wahusika wakiwamo bwana mkubwa mwenyewe (Rais Kikwete), viongozi wa mashirika na taasisi mbalimbali na mabalozi, kuonesha kuwa kuna tatizo la msingi ambalo Chadema inataka lishughulikiwe.

“Tunajua kuna watu wameudhika, na tunajua kuwa hatukumfurahisha Rais, lakini ujumbe wetu umefika.

Kuna baadhi ya watu wamepotosha kuwa tunampinga Rais. Haikuwa nia yetu kutaka avuliwe urais au aondolewe ofisini, tulitaka aone kuwa kuna tatizo ambalo linatakiwa kushughulikiwa na yeye ndiye mhusika.”

Mbowe alisema hoja ya kwanza ya Chadema ni kuona umuhimu wa kuwa na Katiba mpya
itakayoliwezesha Taifa kujenga misingi imara ya demokrasia na kuifanya nchi kuwa na amani, itakayokalika na kila mtu bila kujali kabila, dini au chama chake cha siasa.

“Tunataka Katiba ambayo itamfanya kila Mtanzania aishi kwa amani na upendo, mfano mzuri ni Zanzibar, walikuwa na tatizo kama hilo lakini sasa wamelishughulikia, kwa kuwa na Katiba nzuri na wamekubaliana kuendesha mambo yao … si unaona kila mtu anafurahia hili na wote wanaishi kwa amani kabisa?” alihoji.

Mbowe alisema kilio chao cha pili ni kuundwa kwa Tume ya Uchaguzi iliyo huru ili kufanya uchaguzi ujao usiwe na dosari.

“Ndiyo uchaguzi umekwisha, lakini tunataka Tume ya Uchaguzi iliyo huru, hatutaki kasoro zilizojitokeza uchaguzi huu zijitokeze katika uchaguzi mwingine, hatutaki Tume ambayo mpaka watu waandamane au wakeshe ndipo watangaze matokeo

Alisema hoja ya tatu ni kuundwa kwa Tume huru itayochunguza malalamiko yao kuhusu kasoro zilizojitokeza kwenye uchaguzi mkuu na kutoa mapendekezo ya kufanyiwa kazi dosari zitakazokuwa zimebainishwa.

“Tuna madai ya msingi kabisa, na tumetumia njia hiyo ili kufikisha ujumbe wetu kwa kufuata taratibu na tumewasilisha kilio chetu kwa amani kabisa, hatujatukana mtu, lakini baadhi ya watu wanatubeza na wengine wanasema tuundiwe azimio la kufukuzwa bungeni, sijui kama wanaelewa taratibu na kanuni.”

Aliongeza: “Katika vipaumbele 13 vilivyotolewa na Rais, hatujasikia suala la marekebisho ya Katiba ambalo limekuwa likilalamikiwa kwa takribani miaka 15 sasa, na hakuna hatua inayochukuliwa, sasa tunataka haya tunayoyadai yawemo kwenye hivyo vipaumbele.

Alhamisi iliyopita, wabunge wa Chadema waliondoka kwenye ukumbi wa Bunge mara baada ya Rais Kikwete kuanza kuhutubia kwa mara ya kwanza tangu kufanyika uchaguzi mkuu, Oktoba 31.

Akizungumzia madai ya kuwapo mgawanyiko ndani ya Chadema, katika kufikia uamuzi huo wa kususia hotuba ya Rais, Mbowe alisema uamuzi huo ulipitishwa ndani ya kikao cha chama hicho.

“Uamuzi ule umetokana na kikao halali cha chama, katika masuala kama hayo, si lazima watu wote wakubali na diyo maana unaweza kufikia hatua ya kupiga kura, lakini mwisho wa yote uamuzi wa wengi ndio unaofuatwa

Walishakubali kuapishwa na tayari wako bungeni,,, wanataka kurudi tena kivipi.... Kwa hayo malalamiko wangegoma kabisa kuapishwa kushinikiza malalamiko
 
Wala si CHADEMA au kiongozi yeyote wa CHADEMA aliyewahi kutamka kususia au kutohudhuria vikao vya bunge. Usiamini habari yoyote inayoandikwa na gazeti la 'Habari Leo' bila ya kufanya uhakiki kwa kutumia vyombo vingine vya habari vinayoaminika, vinayoandika habari kwa kufuata taalum na siyo kuwa vyombo vya propaganda za CCM na serikali yake. Kutokana na mwenendo wa gazeti kama 'Habari Leo' siyo vizuri kulitumia gazeti hilo kama chanzo chenye uhakika wa habari, maana tunalazimika kujadili kitu amabacho hakipo!
 
Kama mwanaJF ninayewasiliana kwa karibu sana na viongozi wa hiki chama, nataka kufafanua kwamba CHADEMA hawakujiuzulu ubunge. Mwenyekiti wao amesisitiza kwamba kususia kwao hotuba ya J.K. ilikuwa ni kuwasilisha ujumbe kwamba kulikuwa na ukiukaji wa sheria na kanuni (uchakachuaji) ktk kufikia matokeo ya kumtaja J.K. kama mshindi.

Ktk kikao cha Bunge kijacho Wabunge wa Chadema watatilia mkazo suala hilo, ambalo linaambatana na Ibara ya Katiba inayotamka kwamba NEC ikishamtaja mshindi baina ya wagombea wa kiti cha u-Rais, basi hakuna chombo au taasisi yoyote itakayoweza kuhoji. Hiki ni kipengele kinachoweza kuwa abused na kuleta maafa kwa taifa.

Niwakumbushe wanaJF kuwa, Dk. Slaa, mgombea wa kiti cha u-Rais wa Chadema, alisisitiza kwamba NEC walikuwa wanakiuka sheria na kanuni kabla ya kutangazwa kuwa J.K. ni mshindi. Dk. Slaa angekamilisha ushahidi wa kukiukwa kwa sheria, angeweza kwenda Mahakama Kuu kuweka injuction kwamba NEC wasitangaze hadi hapo takwimu za kura muhimu kuchambuliwa na kuhakikiwa na wahusika wote. Kwa bahati mbaya, NEC nao ktk juhudi zao za kuibeba CCM, waliharakisha uchakachuaji wa kura na kutangaza.

Jukumu la Wabunge wa Chadema sasa, sio tu kusisitiza umuhimu wa kubadilisha Katiba, bali pia kutoa ushahidi wa uchakachuaji uliofanywa na NEC. Hapo basi ndipo umuhimu wa kuwa na muundo mpya wa Tume ya Uchaguzi utadhihirika.

Jukumu kubwa zaidi la Chadema kama chama ni kuendeleza na ku-intensify kampeni nchi nzima ya Tanzania hadi vitongojini na kaya ili waTanzania waimarike na wawe jasiri kuamua viongozi wao wawe ni wa aina gani. Lazima elimu ya uraia itiliwe mkazo sana kati ya sasa na Oktoba 2015.

Kutokana na ukweli kwamba Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa, hatakuwa na majukumu Bungeni ktk kipindi hiki, ndiye atakayeongoza mikakati ya kutoa elimu hiyo ya uraia akitumia kipaji chache cha kuchambua matatizo ya taifa letu kama alivyodhihirisha katika kampeni za Uchaguzi Mkuu wa 2010.
 
ILI waingie bungeni, wabunge wa Chadema wameweka masharti ambayo yakitekelezwa na Serikali watakuwa hawana tatizo tena.

Masharti hayo kwa mujibu wa Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe ni Serikali kutoa tamko kuhusu hoja yao ya kutungwa Katiba mpya, kuundwa kwa Tume Huru ya Uchaguzi na kutoa msimamo juu ya madai ya kukiukwa kwa taratibu za uchaguzi mkuu wa hivi karibuni.

Katika mahojiano maalumu na HABARILEO jana, Mbowe alisema: “Matendo ya leo yanaleta matukio ya kesho.

Suala la msimamo wetu kushiriki vikao vya Bunge lijalo utategemea na mapokeo ya hoja zetu.

“Kwa sisi kugomea hotuba ya Rais, tunajua ujumbe wetu umefika kwa wahusika wakiwamo bwana mkubwa mwenyewe (Rais Kikwete), viongozi wa mashirika na taasisi mbalimbali na mabalozi, kuonesha kuwa kuna tatizo la msingi ambalo Chadema inataka lishughulikiwe.

“Tunajua kuna watu wameudhika, na tunajua kuwa hatukumfurahisha Rais, lakini ujumbe wetu umefika.

Kuna baadhi ya watu wamepotosha kuwa tunampinga Rais. Haikuwa nia yetu kutaka avuliwe urais au aondolewe ofisini, tulitaka aone kuwa kuna tatizo ambalo linatakiwa kushughulikiwa na yeye ndiye mhusika.”

Mbowe alisema hoja ya kwanza ya Chadema ni kuona umuhimu wa kuwa na Katiba mpya
itakayoliwezesha Taifa kujenga misingi imara ya demokrasia na kuifanya nchi kuwa na amani, itakayokalika na kila mtu bila kujali kabila, dini au chama chake cha siasa.

“Tunataka Katiba ambayo itamfanya kila Mtanzania aishi kwa amani na upendo, mfano mzuri ni Zanzibar, walikuwa na tatizo kama hilo lakini sasa wamelishughulikia, kwa kuwa na Katiba nzuri na wamekubaliana kuendesha mambo yao … si unaona kila mtu anafurahia hili na wote wanaishi kwa amani kabisa?” alihoji.

Mbowe alisema kilio chao cha pili ni kuundwa kwa Tume ya Uchaguzi iliyo huru ili kufanya uchaguzi ujao usiwe na dosari.

“Ndiyo uchaguzi umekwisha, lakini tunataka Tume ya Uchaguzi iliyo huru, hatutaki kasoro zilizojitokeza uchaguzi huu zijitokeze katika uchaguzi mwingine, hatutaki Tume ambayo mpaka watu waandamane au wakeshe ndipo watangaze matokeo

Alisema hoja ya tatu ni kuundwa kwa Tume huru itayochunguza malalamiko yao kuhusu kasoro zilizojitokeza kwenye uchaguzi mkuu na kutoa mapendekezo ya kufanyiwa kazi dosari zitakazokuwa zimebainishwa.

“Tuna madai ya msingi kabisa, na tumetumia njia hiyo ili kufikisha ujumbe wetu kwa kufuata taratibu na tumewasilisha kilio chetu kwa amani kabisa, hatujatukana mtu, lakini baadhi ya watu wanatubeza na wengine wanasema tuundiwe azimio la kufukuzwa bungeni, sijui kama wanaelewa taratibu na kanuni.”

Aliongeza: “Katika vipaumbele 13 vilivyotolewa na Rais, hatujasikia suala la marekebisho ya Katiba ambalo limekuwa likilalamikiwa kwa takribani miaka 15 sasa, na hakuna hatua inayochukuliwa, sasa tunataka haya tunayoyadai yawemo kwenye hivyo vipaumbele.

Alhamisi iliyopita, wabunge wa Chadema waliondoka kwenye ukumbi wa Bunge mara baada ya Rais Kikwete kuanza kuhutubia kwa mara ya kwanza tangu kufanyika uchaguzi mkuu, Oktoba 31.

Akizungumzia madai ya kuwapo mgawanyiko ndani ya Chadema, katika kufikia uamuzi huo wa kususia hotuba ya Rais, Mbowe alisema uamuzi huo ulipitishwa ndani ya kikao cha chama hicho.

“Uamuzi ule umetokana na kikao halali cha chama, katika masuala kama hayo, si lazima watu wote wakubali na diyo maana unaweza kufikia hatua ya kupiga kura, lakini mwisho wa yote uamuzi wa wengi ndio unaofuatwa

kasheshe hiyo. Kelele za mlango hazimnyimi mwenye nyumba kulala.
 
Ili waingie bungeni wanatoa masharti?
Ili waingie bungeni walichohitaji ni kura za wananchi.
Maana ya demokrasia ndio hiyo, huwezi kulazimisha Bunge au serikali kufanya mambo kwenye majukwaa ya kisiasa wakati wewe ni mbunge, kaliongeeni bungeni. Kama kura zenu Bungeni hazitoshi, changamoto ni kutafuta kura hizo kwenye chaguzi zijazo.
Hii ya kusema hamuingii Bungeni mpaka mtekelezewe masharti, ni hysteria.
Na mtawaangusha waliowapigia kura kwa kiasi kikubwa kwa sababu hamjawaambia kuwa kususa ndicho mnachoenda kufanya.

We Zemarocoplo nasikitika sana kwa uelewa wako na uchamgiaji wako WA HOVYOHOVYO!!!!

ELEWA HILI: Chadema wanafanya hayo yoote kwa kuwa wao ni KAMBI YA UPINZANIA INAYOTAMBULIKA KIKATIBA, na sheria ya VYAMA VINGI KWA NCHI YOYOTE DUNIANI INAYOFUATA MFUMO HUO.

CUF,TLP,NCCR,UDP haviwezi kufanya hivyo, kwa kuwa wao ni wawakilishi katika bunge AMBAO hawatoki kwenye CHAMA KIKUU CHA UPINZANIA BUNGENI!!!!!!!

Kambi ya upinzani inaundwa na wabunge WALIO WENGI bungeni,kutoka CHAMA CHA SIASA, baada ya CHAMA TAWALA.

Kugoma kwao, na vitu vingine VINATOA TASWILA TOFAUTI, ukuilinganisha na vyama vingine vilivyo na wawakilishi bungeni.

Kama CHADEMA wangefanya hivyo (kutoa masharti) wakiwa wao wana wabunge wachache kulinganisha na chama, kingine cha upinzani bungeni NDIO UNGETOA HOJA YAKO IYO YA HOVYOHOVYO!!

Kua wewe!!! Uwepo wa chadema BUNGENI ni lazima,kwa kuwa wao ni serikali KIVULI, mpuuzi wewe,CHAMA TAWALA KINAHITAJI UWEPO WAO BUNGENI, kinyume cha hapo HILO NI BUNGE BANDIA na la mabavu, NA DUNIA ITAIONYESHEA KIDOLE TZ!!

Unafikili Kikwete, akiambiwa hakuna kwenda ULAYA (kama Mugabe) si ndio atakufa!! anavyopenda kwenda ulaya na Amercano apate ujiko ujiko kwa vishori vyake, alafu akataliwe kwa hija kama hiyo Lazima afanye mabadiliko.

CCM Mkubwa we!!
 
Ningepata video ya mahojiano ningechangia, ikumbukwe source ni Habari Leo. Kuna utata mwingi sana ktk habari hii
 
Sidhani kama CCM inahitaji uwepo wa Chadema bungeni. Wanaohitaji uwepo wa Chadema ni wananchi waliowapigia kura. Kutokuingia Bungeni ni kuwasaliti wananchi na si kuihujumu CCM.

Idadi yao(46) ni ndogo kiasi kwamba hata wasipokuwepo vikao vyote vya Bunge vitaendelea bila kuvunja kanuni yoyote.Kumbuka pia kuna wabunge 11 wa Chadema ambao hawaungi mkono unamuzi huu wa kinazi.

TLP, CUF na NCCR hawawezi kufanya hivyo kwa sababu hakuna sababu ya msingi ya kufanya hivyo.

Hilo la Kikwete kufa, kama ndicho unachoombea/unachotegemea kutokana na Chadema kugoma kuingia Bungeni basi huna haiba za kitanzania kabisa.
 
Hiki kichwa cha habari kimekaa sawa kweli? Masharti ya kurudi bungeni au kukaa bungeni akiwemo JK aliyeshindishwa kwa kura za wizi wa NEC?

Hii habari kama ya kimtego mtego naona mwandishi ana lengo lake . Halafu gazeti lenyewe HABARI LEO ? Naomba tutafute vyanzo vingine maana maadui wa Chadema ni wengi ingawa hawajui peoples power ilivyo noma
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom