Elections 2010 Chadema yatetea jimbo la Karatu

Habari zilizotufikia hivi punde chadema yapeta Karatu... more details to come mitaa ya karatu ya zizima kwa vifijo. Kura za urais Dr slaa yupo juuu sana.

Ha ha zile picha za kwa Michuzi kuwa CCM yafunika karatu na watu kadhaa kurudisha fomu zilikuwa kanyanga eh? Au zingine zilikuwa photoshop nini?
 
Nipo najifunza kutamka jina la dr.SLAA, DR.willy,dr.broad dr.peter ,du kila neno lina maana yake kwa jina lake. Ukikatakata jina la mpinzan wake utaona vichekesho. Reverend I see you near ferry aka white house.
 
haya ni matokeo ya baadhi za kata za udiwani katika jimbo la Karatu.

1. Dar - Chadema
2. Rhotia - Chadema
3. Karatu - Chadema
4. Qurus - Chadema
5. Endamarariek - Chadema
6. Oldean - Chadema
7. Kansay - Chadema
8. Ganako - Chadema
9. Endamagha - Chadema
10. Baray - CCM
11. Barazani - Chadema
Bado kata tatu matokeo yake hayajapatikana. Suala la Ubunge naambiwa mgombea ubunge na urais wa Chadema wanaongoza japo sijajua idadi yake. Naona wafuasi wa Chadema wapo katika ofisi za Chadema wilaya wakiendelea kushangilia ushindi kwa raha zao. Huku ofisi ya CCM ikiwa imepooza kama vile hakukuwa na uchaguzi. Picha zitafuata muda si mrefu.
Update:
12. Bugher - CCM
13. Mbulumbulu - CCM
14. Endabash - CCM
 
Asante sana Meale kwa kutujuza.

Hongereni wana Karatu, mnajua mahitaji ya mabadiliko ya kweli. Tanzania yote ingekuwa kama Karatu tungekwisha piga hatua miaka kumi mbele. Bravo Karatu
 
Mmh Kasheshe si JK alikuwa huko juzi tu mkasema mara kafunika, kafuta nyayo za slaa, chadema kwa her!

Ah Wapi walisomba watu kwa mabasi ya Mtei na shuttle za Riverside kwa kwenda mbele wale wooote mliowaona huko walitoka Arusha. Si unawajua Chechem kwa uchakachuaji?
 
Matokeo Kata ya Karatu.

Urais:
Chadema - 5756
CCM - 1689

Ubunge:
Chadema - 5582
CCM - 1868

Diwani:
Chadema - 5135
CCM - 2300
 
Ha ha zile picha za kwa Michuzi kuwa CCM yafunika karatu na watu kadhaa kurudisha fomu zilikuwa kanyanga eh? Au zingine zilikuwa photoshop nini?

wamebebwa na malori kutoka mbulu, singida, ngorongoro nk. sio wapiga kura wa pale
 
Nafikiri plausible assumption ni kwamba kote ambako Chadema wameshinda hasa ubunge, Dr. Slaa atakuwa anaoongoza kwa mbali sana dhidi ya JK aka "Mr. Beep".
 
Mmh Kasheshe si JK alikuwa huko juzi tu mkasema mara kafunika, kafuta nyayo za slaa, chadema kwa her!

Hakufunika na wanakaratu ila walibebwa watu kutoka mjini kuja kumsikiliza...kwa hiyo wanakaratu walikua hawana time nae, kwani hawadanganyiki......ni watu wenye muamko hawawezi kudanganywa kama hao wengine wanaodanganywa na khanga na tshirt...
 
Nina kiu na numbers; Hongereni wana Karatu, na tafadhali tunaomba umjumlishe hizo kura na kisha mzianike ili iturahisishie ku-audit numbers zitakazotolewa na NEC.
 
Back
Top Bottom