Chadema yalaani kuzuiwa mikutano........................

Kwa hiyo CHADEMA itaiondoa rushwa mahakamani kwa kususia mfumo wa sheria au kwa ku expose mfumo wa sheria?

Unaelewa distinction niliyoitoa kati ya mahakama za chini na mahakama za juu? Unaijua Mahakama ya Rufaa Tanzania na historia yake kuhusu kesi za kisiasa? Umeona precedents za watu kama majaji Francis Nyalali, Kahwa Lugakingira na Robert Kisanga, nikiwataja wachache tu, katika kutoa rulings na findings zilizo sema kweli kwa watawala ?

Tatizo hapa ni kwamba mna defeatist attitudes, na huwezi kushinda hata siku moja kama ukiwa na defeatist attitude. You gotta play to win. Peleka kesi mahakamani, tuonyeshe ushahidi, hata kama ni wa kimazingira tu, kwamba CCM inatumia mahakama kuwaminya CHADEMA. Tupe vifungu vya katiba vinavyovunjwa na Polisi, tuonyeshe kwamba polisi hawana nguvu wala haki ya kuzuia political association, wananchi si wajinga, tutaona. Wajuzi wa sheria watachambua mambo, mta expose hilo.

Sio hata kabla hamjapeleka kesi mahakamani mshaanza kuji defeat wenyewe kwa hypothetical situations, wananchi tutawaona walalmishi mnao argue theoretically bila factual backing.
Nimesoma gazeti la Majira,Tanzania Daima,The Citizen na Mwananchi Tundu Lisi ameelezea kwa uwazi kabisa vifungu vya kisheria vilivyoanishwa vinavyovunjwa na jeshi la polisi alizungumzia pia hatua watakayoifanya kama Jeshi la Polisi hatawapa kibali huko mbeleni ikiwa ni pamoja na kutoa hoja ya dharura bungeni kwa kutokubali bunge kuendelea na shughuli yeyote mpaka watakapoelezwa ni kwa nini jeshi la polisi linazuia wabunge wa CDM kufnya kazi zao ikiwemo mikutano ya hadhara
Hatua nyingine ni kushitaki kwenye bunge la jumuiya ya madola kwa hiyo hawalalamiki tuu wana plan B kama Plan A haitafanya kazi
 
It is real boring!! Yaani kweli watu wazima and their so called great thinking wameamua kujadili hii thread either kwa ku-support move ya CHADEMA au kuipinga just kwa kusoma headlines tu...aaagh...kweli kabisa...mimi nimezisoma stories zote mbili...nafikiri suala la kwanza ilikuwa ni wachangiaji kuomba mwanzishaji wa thread aweke texts hapa, ikibidi zote mbili kutoka magazeti hayo mawili tofauti ambayo yameona umuhimu wa hiyo stori na kuipatia umuhimu unaostahili.

Tusiwe sawa na wanasiasa ambayo huwa wanalipuka kwa kusoma headlines tu, hata kama ni summary ya kile kilichoandikwa katika text lakini kusoma na kuelewa, inakusaidia kugrasp the whole concept, then unajiuliza maswali mawili matatu kichwani...maana siku hizi kuna vyombo vya habari vinawasilisha mambo ndivyo sivyo...kisha unachangia, mjadala unanoga lakini hii ilivyo sasa aaah...maana kuna mwingine nimemsoma ameandika eti CHADEMA hawajaonesha vifungu vyovyote vya kisheria vilivyovunjwa katika move ya polisi that is more or less than bullshit...inatokana na kutosoma kabla...someni magazeti...maana electronic media jana zilichelewa katika hiyo press. Tuendelee
 
Polisi hawapaswi kuwazuia CHADEMA kufanya mikutano. Lakini labda CHADEMA wanataka kuendelea na harakati za Uchaguzi wakati Uchaguzi umekwisha. Conservatives waliposhinda Uingereza,jambo la kwanza lililotokea,David Cameron aliunda Cabinet,pamoja na Lib Dems.
Labour waliposhindwa,jambo la kwanza kabisa,Ed Millerband,kiongozi wa Labour,aliunda Shadow Cabinet. Hawaendelei na Kampeni za Uchaguzi. Ile Shadow Cabinet inaipinga Serikali,siyo tu katika Bunge,lakini,kila wakati.
Yaani wao wana politics ambayo Shadow Cabinet itapingana na Real Cabinet,mpaka siku ya election. Hiyo diyo politics yao. Kwa hiyo mikutano ambayo CHADEMA wanayotaka kufanya sasa hivi siyo politics,ni kukengeua from real politics kama inavyofanywa katika Nchi nyingine zote. Katika Uchaguzi Mku wanabishana hilo tu,kwamba kama watafanikiwa kuunda Real Cabinet,au kama itawabidi kuridhika kuunda Shadow Cabinet.
Waunde Shadow Cabinet wabishane na Serikali ndani na nje ya Bunge. Hawahitaji kufanya mkutano wa hadhara.
Unajifunza siasa naona au una lako jambo si bure. Sasa uoga wote wa nini? Chadema wanawezaje kukutana na wanachama na wapenzi wake for any reason?
 
Hivi mikutano inazuiwa kwa nini kama sisi ni democratic country? Labda watujuze ni nini maana ya kuwa huru pengine bado tuko kwenye utumwa wa Chama Cha Majambazi.
 
Back
Top Bottom