CHADEMA kuanza Mikutano ya Hadhara Desemba 2022

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,379
8,121
Msimamo huo umetangazwa Wilayani Sengerema na Mjumbe wa Kamati Kuu, John Heche kwa maelezo kuwa suala hilo ni Haki yao Kikatiba.

Heche amesema “Ndani ya mwezi mmoja ujao tutatangaza ratiba na kuanza mikutano ya hadhara, mwaka 2022 hautaisha bila CHADEMA kufanya mikutano ya hadhara ambayo ni Haki ya Kikatiba na Kisheria kwa Vyama vyote vya Siasa”.

Tangazo la CHADEMA limekuja kukiwa na vikao kadhaa vya Wadau wa Siasa kutafuta namna bora ya kuendesha shughuli zao ikiwemo Mikutano ya Hadhara iliyozuiwa na aliyekuwa Rais wa awamu ya 5, hayati John Magufuli Mei, 2016.

==========================

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimetangaza msimamo wa kuanza mikutano ya hadhara kabla ya mwisho wa mwaka huu.

Msimamo huo umetangazwa mjini Sengerema jana na mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, John Heche wakati wa mkutano mkuu wa chama hicho jimbo la Sengerema.

“Ndani ya kipindi cha mwezi mmoja ujao tutatangaza ratiba na kuanza mikutano ya hadhara; mwaka huu hautaisha bila Chadema kuanza kufanya mikutano ya hadhara ambayo ni haki ya kikatiba na kisheria kwa vyama vyote vya siasa,” alisema Heche.

Tangazo hilo la Chadema limekuja huku kukiwa na vikao kadhaa vya wadau wa siasa kutafuta namna bora ya kuendesha shughuli za kisiasa ikiwemo mikutano ya hadhara iliyozuiwa kwa agizo la aliyekuwa Rais wa awamu ya tano, hayati John Magufuli tangu Mei, 2016 huku madiwani na wabunge pekee wakiruhusiwa kufanya mikutano katika maeneo yao ya uchaguzi.

Mbunge huyo wa zamani wa Tarime vijijini aliwataka viongozi na wanachama wa chama hicho kikuu cha upinzani kujitolea kwa hali na mali kukijenga chama chao na kujianda kushiriki na kushinda chaguzi ili kushika dola, huku akidai chama tawala (CCM) kimefikia upeo wake kiuongozi.

“CCM haiwezi kuleta mapinduzi ya maendeleo hata ikipewa miaka 100 ya kukaa madarakani kwa sababu tuna miaka 61 ya Uhuru, lakini bado tunajadli matundu ya vyoo, tena vyoo vya shimo,” alisema Heche

Awali, Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Mwanza, Grayson Wanzagi na Katibu wa Kanda ya Victoria, Zacharia Obadi waliwataka viongozi na wana Chadema kukijenga chama kuwa taasisi imara tayari kushinda chaguzi zijazo na kushika dola.

Katika hatua nyingine, chama hicho kimesema ukuaji wa haraka wa deni la Taifa, ni mzigo kwa wananchi huku wakipendekeza mambo kadhaa kudhibiti suala hilo kwa haraka.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Mbunge wa Bunge la Wananchi la Chadema, Ahobokile Mwaitenda alisema deni hilo linawaumiza na kuwatesa Watanzania.

Taarifa ya Benki Kuu (BoT) inaonyesha hadi Septemba 2022, deni la Taifa lilifikia dola za kimarekani 38.44 billion (Sh88.4 trillion). Wakati katika hilo deni la serikali likiwa Sh71.55 trilioni.

Katika mapendekezo yao Mwaitenda aliitaka Serikali kuchambua deni lote la Taifa lililopo kwa vigezo vilivyo sababisha ukopaji na kupima matokeo yake.

Hata hivyo, akizungumza na Mwananchi jana Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Emmanuel Tutuba alisema taarifa zote za deni zinasomwa kwenye bajeti na Bunge linaloidhinisha hiyo bajeti.

MWANANCHI
 
Hii inathibitisha ubora wa mama, vinginevyo saa hii tungekuwa tunaongea mengine baada tu ya kauli hiyo
 
Viongozi wa Chadema wanajiandaa kuweka hadharani muda wowote kuanzia sasa RATIBA KABAMBE YA MIKUTANO YA HADHARA NCHI NZIMA .

Hayo yamebainishwa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama hicho , John Heche akiwa kwenye shughuli za chama chake huko Sengerema , ikumbukwe pia kwamba Heche ni Mjumbe wa Chadema kwenye vikao vya Maridhiano .

Naomba nichukue nafasi hii kuwaomba radhi wananchi wote wa Tanzania , kwa kuchelewa kutolewa kwa ratiba hii ya Mikutano ya hadhara kulikosababishwa na sababu za Kiungwana tu

Namalizia na Nukuu ya Rais mstaafu Jakaya Kikwete , aliyoitoa kwenye vikao vya ccm mwaka 2012

FB_IMG_1574277425198.jpg
 
Alikuwa anawafurahisha tu hapo ili msiulize fedha za chama zinakokwenda Hadi kukosa kibanda Cha ofisi, alitaka msiulize hata hela za join the chain za hivi majuzi , Anachopanga hapo Ni mbinu za kukusanya michango mingine ili akazitafune na kuziswaga zote, hakika alishawaokota na kujinufaisha na Saccos yake
 
Back
Top Bottom