CHADEMA yafanyiwa vurugu kubwa na CCM wilayani Meatu

Hivi gari la CCM likisogelea mkutano wa CDM likiwa limepambwa na bendera za kijani kutakuwa na usalama? They got what they deserved. Who is Mpina to them? Wana bahati hawakuchomwa moto.
 
Hivi gari la CCM likisogelea mkutano wa CDM likiwa limepambwa na bendera za kijani kutakuwa na usalama? They got what they deserved. Who is Mpina to them? Wana bahati hawakuchomwa moto.

A stupid mind!
 
Wafuasi wa CCM wilayani Meatu juzi walilishambulia kwa mawe gari lililobeba viongozi wa CHADEMA na kuliharibu vibaya huku wakinyofoa bendera za CHADEMA na kutupa kusikojulikana.

Gari hilo lilishambuliwa wakati wafuasi hao wakienda kwenye maandamano ya kumlaki mbunge wa Kisesa Luhaga Mpina(CCM) na kisha kufuatiwa mkutano wa hadhara.

Viongozi wa CHADEMA nao walikuwa wamealikwa kwenye mkutano huo wa mbunge kama sehemu ya viongozi wa kisiasa katika jimbo hilo.

Inadaiwa kati ya watu walioshiriki uhuni huo walikuwemo baadhi ya viongozi wa CCM wilayani Meatu.

Viongozi wa Chadema waliokuwa katika gari hilo lilokuwa likiendeshwa na dereva James Daud ni Kiongozi wa msafara wa viongozi wa Chadema Joshua Mgema ,Zacharia Magembe ambaye Mlezi wa Chadema wilaya ya Meatu, Jackson Kimwaga Katibu Mwenezi wa Wilaya ya Meatu, Hadija Kidati Mwenyekiti wa Wanawake wa Chadema Wilaya ya Meatu na Joseph Lutoja Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Meatu.

Mbunge wa Jimbo hilo alilaani tukio hilo na kusema hizo ni siasa za kihuni na za kizamani ambazo zinapaswa kulaaniwa na wapenda maendeleo wote na kudai aliwaalika viongozi hao wa CHADEMA kama viongozi halali wa kisiasa katika jimbo lake.Tukio hili tayari limeripotiwa polisi


Source: Nipashe Alhamisi


My Take:
Zimepita siku 3 sasa toka tukio hili la kihuni litokee lakini Msajili wa vyama vya siasa John Tendwa bado hajatolea tamko lolote kuhusu vurugu hizi zinazoonekana ziliratibiwa na viongozi na wanachama wa CCM wilayani Meatu.Ikumbukwe John Tendwa aliapa kufuta vyama vyote vinavyosababisha vurugu.



Meatu wameiga siasa za vurugu,mbona wasukuma wastaarabu sana
 
Back
Top Bottom