CHADEMA yafanyiwa vurugu kubwa na CCM wilayani Meatu

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Wafuasi wa CCM wilayani Meatu juzi walilishambulia kwa mawe gari lililobeba viongozi wa CHADEMA na kuliharibu vibaya huku wakinyofoa bendera za CHADEMA na kutupa kusikojulikana.

Gari hilo lilishambuliwa wakati wafuasi hao wakienda kwenye maandamano ya kumlaki mbunge wa Kisesa Luhaga Mpina(CCM) na kisha kufuatiwa mkutano wa hadhara.

Viongozi wa CHADEMA nao walikuwa wamealikwa kwenye mkutano huo wa mbunge kama sehemu ya viongozi wa kisiasa katika jimbo hilo.

Inadaiwa kati ya watu walioshiriki uhuni huo walikuwemo baadhi ya viongozi wa CCM wilayani Meatu.

Viongozi wa Chadema waliokuwa katika gari hilo lilokuwa likiendeshwa na dereva James Daud ni Kiongozi wa msafara wa viongozi wa Chadema Joshua Mgema ,Zacharia Magembe ambaye Mlezi wa Chadema wilaya ya Meatu, Jackson Kimwaga Katibu Mwenezi wa Wilaya ya Meatu, Hadija Kidati Mwenyekiti wa Wanawake wa Chadema Wilaya ya Meatu na Joseph Lutoja Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Meatu.

Mbunge wa Jimbo hilo alilaani tukio hilo na kusema hizo ni siasa za kihuni na za kizamani ambazo zinapaswa kulaaniwa na wapenda maendeleo wote na kudai aliwaalika viongozi hao wa CHADEMA kama viongozi halali wa kisiasa katika jimbo lake.Tukio hili tayari limeripotiwa polisi


Source: Nipashe Alhamisi


My Take:
Zimepita siku 3 sasa toka tukio hili la kihuni litokee lakini Msajili wa vyama vya siasa John Tendwa bado hajatolea tamko lolote kuhusu vurugu hizi zinazoonekana ziliratibiwa na viongozi na wanachama wa CCM wilayani Meatu.Ikumbukwe John Tendwa aliapa kufuta vyama vyote vinavyosababisha vurugu.


 
Tendwa hawezi kusema jambo cha muhimu n kutafuta njia ya kuwadhibiti hao wahuni.
 

My Take:
Zimepita siku 3 sasa toka tukio hili la kihuni litokee lakini Msajili wa vyama vya siasa John Tendwa bado hajatolea tamko lolote kuhusu vurugu hizi zinazoonekana ziliratibiwa na viongozi na wanachama wa CCM wilayani Meatu



Ivi mwenye CV yake ataondoka lini ofisini?? nikimuona napata kichefuchefu.
 
nchi ina laana hii,haiwezekani zaidi ya miaka hamsini kinatawala chama kimoja kilichoshindwa kuwakwamua wananchi wake kwenye dimbwi la umasikini halafu jeshi na usalama wa taifa wanawasaidia wahuni hawa waendelee kuiba
 
quote_icon.png
By mohamedi tantawi
Weka ushahidi hapa

quote_icon.png
By mohamedi tantawi
Weka picha ya ilo gari lililoharibiwa

quote_icon.png
By mohamedi tantawi
Weka ushahidi hapa

quote_icon.png
By mohamedi tantawi
Nao wanaiga ya watani wao

sio reliable sosi

Mkuu salama lakini..? Familia haijambo..? Wape salamu home hapo..
 
Hivi kile kibabu cha (mav)uvccm shingela hakijaongea tu....au ndo mkuki kwa........
 
Tendwa amezeeka hawezi kwenda na kasi ya Mageuzi nchini. Anatakiwa abaki na kazi ya ushauri. Kazi nyingine aendelee kuwasimulia wajukuu zake jinsi alivyosaidia kuvuruga mfumo wa vyama vingi.
Tendwa hajitofautishi yeye na Katiba.
 
Back
Top Bottom