CHADEMA yafanyiwa vurugu kubwa na CCM wilayani Meatu

Nao wamezidi kiherehere,halafu hiyo gari gani yenye uwezo wa kubeba abiria wote hao au walipakatana.Kwiii!Kwwii! kwi! teh tehee.......
 
Tendwa hawezi kusema jambo cha muhimu n kutafuta njia ya kuwadhibiti hao wahuni.
Achana na Tendwa kwanza ni nonexistent kwenye siasa za chadema, kama wafuasi wa CDM ndo wangekuwa wamefanya hivyo, tayari angeshakuja na vitisho!!!!!
 
Wafuasi wa CCM wilayani Meatu juzi walilishambulia kwa mawe gari lililobeba viongozi wa CHADEMA na kuliharibu vibaya huku wakinyofoa bendera za CHADEMA na kutupa kusikojulikana.

Gari hilo lilishambuliwa wakati wafuasi hao wakienda kwenye maandamano ya kumlaki mbunge wa Kisesa Luhaga Mpina(CCM) na kisha kufuatiwa mkutano wa hadhara.

Viongozi wa CHADEMA nao walikuwa wamealikwa kwenye mkutano huo wa mbunge kama sehemu ya viongozi wa kisiasa katika jimbo hilo.

Inadaiwa kati ya watu walioshiriki uhuni huo walikuwemo baadhi ya viongozi wa CCM wilayani Meatu.

Viongozi wa Chadema waliokuwa katika gari hilo lilokuwa likiendeshwa na dereva James Daud ni Kiongozi wa msafara wa viongozi wa Chadema Joshua Mgema ,Zacharia Magembe ambaye Mlezi wa Chadema wilaya ya Meatu, Jackson Kimwaga Katibu Mwenezi wa Wilaya ya Meatu, Hadija Kidati Mwenyekiti wa Wanawake wa Chadema Wilaya ya Meatu na Joseph Lutoja Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Meatu.

Mbunge wa Jimbo hilo alilaani tukio hilo na kusema hizo ni siasa za kihuni na za kizamani ambazo zinapaswa kulaaniwa na wapenda maendeleo wote na kudai aliwaalika viongozi hao wa CHADEMA kama viongozi halali wa kisiasa katika jimbo lake.Tukio hili tayari limeripotiwa polisi


Source: Nipashe Alhamisi


My Take:
Zimepita siku 3 sasa toka tukio hili la kihuni litokee lakini Msajili wa vyama vya siasa John Tendwa bado hajatolea tamko lolote kuhusu vurugu hizi zinazoonekana ziliratibiwa na viongozi na wanachama wa CCM wilayani Meatu.Ikumbukwe John Tendwa aliapa kufuta vyama vyote vinavyosababisha vurugu.


Mkuu achana na huyo mtu, anasema pale anapoona upinzani hasa CDM wanasonga mbele, namshangaa kazi yake ni kusajili vyaama na siyo mlezi wa vyama kama anavyojisadikisha. Na sijui ofisi hii mtu anatakiwa kukaa muda gani, inafaa sasa vyma vyote vikae kuteua Msajili wa vyama ili kupunguza watu wenye mawazo hayo pale waanaapowekwa na watawala ama chama kinachotawala. Na katiba mpya itabidi iweke taasisi ya usajili badala ya ofisi kama ilivyo sasa.
 
Wewe jamaa kila siku unalalamika humu JF unapigwa ban za kuonea sasa ulichoandika hapa si upuuzi tu.
Kwani wewe hukuona huyo kapewa source lakini bado anasema sio reliable anataka gazeti la uhuru!!!!! Hayo ndio majibu ya watu kama hao
 
Mkuu achana na huyo mtu, anasema pale anapoona upinzani hasa CDM wanasonga mbele, namshangaa kazi yake ni kusajili vyaama na siyo mlezi wa vyama kama anavyojisadikisha. Na sijui ofisi hii mtu anatakiwa kukaa muda gani, inafaa sasa vyma vyote vikae kuteua Msajili wa vyama ili kupunguza watu wenye mawazo hayo pale waanaapowekwa na watawala ama chama kinachotawala. Na katiba mpya itabidi iweke taasisi ya usajili badala ya ofisi kama ilivyo sasa.

Ni kweli tupu mkuu...
 
Back
Top Bottom