CHADEMA yaandika historia kwa kushinda ndani ya ngome ya CCM

Mbelwa Germano

JF-Expert Member
May 7, 2011
789
289
Yamezungumzwa mengi kuhusu Mkoa wa Tanga na Kukubalika kwa CHADEMA. Zimejengwa propaganda nyingi dhidi ya CHADEMA kuwa ni chama cha WAKRISTO,WACHAGA na Kanda ya Kaskazini (Tanga Excluded). Baadhi yakaenda mbali zaidi kukiita chama cha Kigaidi. Haya yote nimakuzi ya chama kuelekea kupewa mamlaka kamili ya kuongoza Watanzania.

Tarehe 24.03.2013 kulikuwa na Uchaguzi wa na Vijiji Wilaya ya Lushoto yenye majimbo matatu: Lushoto, Mlalo na Bumbuli. Baadhi ya watu wanaweza wakaona uchaguzi huu hauna maana sana lakini ukweli ni kwamba uchaguzi huu ni ISHARA ya kukubalika kwa CHADEMA katika ngazi ya chini kabisa ya chama (ngazi ya msingi).

Kwa mara ya Kwanza Wasambaa,Wapare, Wambugu n.k. wakadhibitisha kwamba CHADEMA sio chama cha WAKRISTO, WACHAGA na Kanda ya Kaskazini (Tanga Excluded), BALI ni Chama Cha Watanzania. Kwa mara ya Kwanza wakathuibitisha sio Mitaji ya Chama cha Mapinduzi. Mapinduzi: Kutumia nguvu kukitoa kitu Halali na kuweka kitu kisicho halali.

Yafutayo ni matokeo ya Uchaguzi wa tarehe 24.03.2013:

Jimbo la Lushoto:


  1. Milungui: CCM-60 CDM-140
  2. Kongei: CCM Imeshinda
  3. Masange:CCM-99 CDM-66

Jimbo la Mlalo:


  1. Nywelo: CCM-172 CDM-198
  2. Mkunki: CHADEMA imeshinda
  3. Tema: Uchaguzi umevurugika
Idadi ya kura ya Mgombea wa CCM na CDM hazi-match na idadi ya watu waliopiga kura,310, kuna tofauti ya kura 51
CCM-137
CDM-115
Haribika - 7
Jumla: 259
Jumla ya kura zilizopigwa ni 310
310-259=51

Jimbo la Bumbuli


  1. Kiluai: CCM-106 CDM-96
  2. Tamota: CCM-115 CDM-71
  3. Kwekitui: CDM imeshinda, uchaguzi umevurugwa, Kurudiwa tarehe 31.03.2013
  4. Wanga: CCM-88 CDM-159
  5. Kwemisambia: CCM-141 CDM-33

Nitaendelea kuwahabarisha, kwenye maeneo mengine.

Jumla ya vijiji vilivyokuwa na uchaguzi wa marudio ni 23

Kijiji cha Kiviricha,jimbo la Bumbuli

Mtendaji wa kijiji amemuengua Mgombea wa CHADEMA bila kutoa taarifa rasmi ya kimaandishi na kufuata kanuni na taratibu za uchaguzi.

Mavumbi, Kwadoe, Kisiwani......

CUF haikusimamisha Wagombea toka vijiji vyote ambavyo kumefanyika uchaguzi

Sasa ukombozi unaanza kuonekana ,mara kwa mara huwa nasema ukombozi wa Taifa hili utaanzia Mkoani Tanga,
CHADEMA kimeshinda vijiji ambavyo havijawahi kushinda upinzani tangu upinzani uanze na CUF kuwepo maeneo hayo ya Wilaya ya LUSHOTO TANGA,kipindi hicho chote.

Mwaka 2015 ndio mwaka wa ukombozi wa Taifa hili.

Vijiji vi-4 na cha tano tunachukua muda si mrefu na vingine uchaguzi utarudiwa ni Mbio za ukombozi wa Taifa hili, Chaguzi za wenyeviti wa Vijiji
ulofanyika ni ishara sasa hata huku Tanga Wananchi wameanza kutambua haki zao za msingi, Taifa CHADEMA ongezeni nguvu
Vijijini ili 2015 ushindi uwe wa kimbunga.

Hakika mabadiliko yanakuja.
 
Kimeshinda nini? Tuletee taarifa kamili kama ni uchaguzi wa kijiji au vijiji tuambie CHADEMA tumeshinda viti vingapi maana si wote tupo Lushoto!
 
Wakuu, mleta mada hapo juu nilivyomwelewa ni kuwa kulikuwa na uchaguzi wa marudio na ingawa hajasema ni jumla ya vijiji vingapi, amesema CHADEMA tumeshinda viti vitano. Amesema bado kuna uchaguzi unarudiwa sehemu zingine.


HABARI NZURI SANA HII.
 
sasa hii ndo nini umeandika? au kuna mtu kaedit thread yako. tuambie chadema imefanya nini huko?. mia
 
Mkuu philip LULINDA
najua una furaha sana ya ushindi lakini naomba ujitahidi kutulia na kuleta habari iliyokamilika kwa kueleza yafuatayo: Uchaguzi ni wa nini? ulifanyika lini? ulihusisha vijiji vingapi? kati ya hivyo CHADEMA wameshinda vingapi na CCM washinda vingapi? halafu tutajie majina ya vijiji ili wenyeji wa huko walioko mbali wajue ukombozi umefika.

Nashukuru sana mkuu philip LULINDA
 
Wakuu, mleta mada hapo juu nilivyomwelewa ni kuwa kulikuwa na uchaguzi wa marudio na ingawa hajasema ni jumla ya vijiji vingapi, amesema CHADEMA tumeshinda viti vitano. Amesema bado kuna uchaguzi unarudiwa sehemu zingine.


HABARI NZURI SANA HII.


kamanda ukiona mtu anabeza mkakati ulofany ujue ana itikadi fulani hawa wengine ni Magamba ambao walizoea kuaona CCM inabaki madarakaini, Kwa sasa Sisi majembe tumezamilia hadi waondoke meaka 2015 hakuna kulala
Mawazo yako kamanda mazuri na tuunge mkono kuokoa Taifa hili.
 
Sasa ukombozi unaanza kuonekana ,mara kwa mara huwa nasema ukombozi wa Taifa hili utaanzia Mkoani Tanga,
Chadema kimeshinda vijiji ambavyo havijawahi kushinda upinzani tangu upinzani uanze na CUF kuwepo maeneo hayo ya Wilaya ya LUSHOTO TANGA,kipindi hicho chote. Mwaka 2015 ndio mwaka wa ukombozi wa Taifa hili.
Vijiji vitano na vingine uchaguzi utarudiwa ni Mbio za ukombozi wa Taifa hili, Chaguzi za wenyeviti wa Vijiji
ulofanyika ni ni ishara sasa hata huku Tanga Wanachi wameanza kutambua haki zao za msingi,
Hakika mabadiriko yanakuja.
Naomba kuwakilisha hili kwenu.
Mkuu taarifa yako hujaiweka sawa.Tunaomba utuambie uchaguzi huo ulihusu jumla ya vijiji vingapi nanCHADEMA wameshinda vingapi na CCM wameshinda vingapi?

Na jee hivo vijiji vitano vinarudia uchaguzi?

Usibishane na watu toa ufafanuzi.Kama huna taarifa kamili bado unaweza ukasema tukakuelewa tu.
 
halafu eti ni senior member, uandishi ndio huo

Naona ujio wa Kinana umemwaga vijana wengi mitandaoni kukitetea chama/serikali.Kila thread ikiletwa upo! Hauna kazi nyingine wewe? Wapiga kura wengi ni maskini wa kutupwa ambao hawana access ya internet badilini strategy hii haiwasaidii
 
vijana wa nape kwa kurukia threads.....ni ajira tosha kwao hapa jf.

Nikweli hawa ni wale vijana wa Mwiguru na nape lakini naamini hawa Nchemba na Nape sanasana Mwiguru 2015 atakuwa analisikia bunge Redioni na kwenye video tu Iramba Magharibi hawamtaki na mimi ntaongoza kampeni kwa vijana wa Singida Mwiguru Nchemba wasimchague.
 
Nikweli hawa ni wale vijana wa Mwiguru na nape lakini naamini hawa Nchemba na Nape sanasana Mwiguru 2015 atakuwa analisikia bunge Redioni na kwenye video tu Iramba Magharibi hawamtaki na mimi ntaongoza kampeni kwa vijana wa Singida Mwiguru Nchemba wasimchague.
wewe utaongoza kampeni mwiguru asichaguliwe we ni shemeji yake kitila mkumbo au utakuwa kampeni meneja wa kitila mkumbo wakati huo.
 
hongera sana kaka kwa jitihada zilizopelekea ushindi. siku zote maneno yatabaki kuwa maneno na hali halisi itabakia kama ilivyo. wale wa chama tawala wanaojiendesha kama chama cha upinzani waachwe wajifunze kuwa wapinzani. aluta continua
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom