Chadema watowa kichapo cha mbwa mwizi kwa wanaccm.ccm nan wamtowa nundu mwanatakukuru

Tukundane

JF-Expert Member
Apr 17, 2012
11,455
8,249
Wanachama wa chadema waliwashambulia wanachama wa ccm kwa marungu na kuwajeruhi kwa kuwakata kwapanga usiku wa tarehe 28 kuamkia tarehe29.baada ya kuwafuma wakiwa wanazunguka kila nyumba ya mpiga kura majira ya usiku na kumuhonga kila mpiga kura kiasi cha tsh10000/=.chadema waliamuwa kufanya msako baada ya kutonywa kuwa ccm wanatumia njia hiyo ili waweze kushinda nafasi ya udiwani ambayo ilikuwa inashindaniwa katika kata ya mpapa wilayani mbozi. pia walikamatwa walinzi wa chama hicho na kupigwa kipigo cha mbwa mwizi na kuwapora fedha zote zilizo kuwa zinatumika kuwahonga wapiga kura.wakati huohuo wanachama wa ccm walimtowa nundu mtumishi wa takukuru akiwa kwenye shughuli za kikazi baada ya kuingia kwenye kambi ya wanaccm.
 
Saaaaaaaaaafiiiiiiiiiiii saaana tumerudia enzi yetu ile ya upinzani-ngumi baada yakuona kumbe wenzetu wakifanya fujo policcm wanafurahia sasa ngoja tuwaonyeshe kuwa sisi ni Noma kwa ngumi na ustaarabu ni msisitizo wa viongozi wetu ambao ccm wanautumia vibaya sasa kama mbwai mbwai tuone nani atakaye salimu amri m.a.t.a.k.o yao nyinyiemu
 
:A S 41:Mimi siwaelewi watz watatufikisha wapi, hivi hawa wanaopewa hongo hawawezi kuwatosa kwa kutowapigia kura halafu ikawa fundisho kwa rushwa?
 
CCM hawajaenda kushitaki polisi?

swala la kwenda polisi lilikuwa halikwepeki.hasa kwa wale waliojeruhiwa kwa mapanga kwa ajili ya kupata pf3 ikiwa ni pamoja na mtumishi wa takukuru alietolewa nundu kwa kupigwa jiwe na wanaccm.walipojaribu kuwa shinikiza polisi wawafungulie kesi ili wanachadema wakamatwe.walishauriwa na polisi kutokufunguwa kesi kwa vile waliopigwa walikuwa siyo wakazi wa kata husika pia ilikuwa ni usiku.mazingira ambayo yangewapa wapinzani wao kuwahoji kuwa wao siyo wa kazi wakata hiyo na ilikuwa ni usiku hivyo walikwenda kufanya nini.kitendo ambacho kingeimarisha ushahidi wa chadema kuwa walifumwa wakitowa rushwa kwa wapiga kura.
 
Lakini baada ya uchaguzi matokeo ya udiwani yalikuwaje tunaomba utujuze!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

ccm waliibuka kidedea kwa kura 900 dhidi ya kura 375 za mgombea wa chadema.huku kulikuwa na wapiga kura 2000 ambao karibu wote walihongwa na ccm.
 
Umekurupuka mkuu wangu!!wapi huko?

sija kurupuka mkuu wangu labda hujanipata vizuri.nimesema kuwa kata ya mpapa wilayani mbozi.kwa nyongeza wilaya ya mbozi iko mkoani mbeya.ambako kulifanyika chaguzi katika kata 2 ya mpapa na muyovizi na zote zimechukuliwa na ccm.anaetuhumiwa kumwaga fedha katika kata hizo ni Mwigulu nchemba ambae alifika kufunga kampeni katika maeneo hayo tarehe 27 na usiku huo huo wa kuamkia tarehe 28 siku ya kupiga kura fedha zilimwaga kuliko siku za kawaida.ingawa hapo juu nimeandika kuwa ilikuwa usiku wa kuamkia tarehe 29 sahihi ni tarehe 27 kuamkia siku ya uchaguzi tarehe 28.asante kwa kunifanya nikumbuke na kosa nililo lifanya.
 
Back
Top Bottom