CHADEMA watoa mkono wa pole kwa wahanga wa mafuriko

Bitabo

JF-Expert Member
Sep 27, 2011
1,900
687
Mchana huu nilikuwa napita pale sinza vatican bondeni nikakuta msafara wa magari ya CDM wakiwa na Aikael. Sikuweza kusimama ila nimeona pickup zikiwa na mizigo ya vyakula kwa ajili wa wahanga wa mafuriko maeneo yale
 
walienda maeneo ya uzuri darajani mkuu ...kutoa pole kwa walioathirika na mafuriko
 
KUB vipi habari za CDM kulipotiwa na mpita njia si tuna Kurungezi ya Habari na anakinga salary nzuri tu. K wa nini wapita njia watuhabarishe hisia tu, kama vipi piga chini graduates tupo mitaani Kiongozi. Hata kama mtu wako lakini kazi hafanyi achana nae, hafai kuingia nae Ikulu.
Mchana huu nilikuwa napita pale sinza vatican bondeni nikakuta msafara wa magari ya CDM wakiwa na Aikael. Sikuweza kusimama ila nimeona pickup zikiwa na mizigo ya vyakula kwa ajili wa wahanga wa mafuriko maeneo yale
 
KUB vipi habari za CDM kulipotiwa na mpita njia si tuna Kurungezi ya Habari na anakinga salary nzuri tu. K wa nini wapita njia watuhabarishe hisia tu, kama vipi piga chini graduates tupo mitaani Kiongozi. Hata kama mtu wako lakini kazi hafanyi achana nae, hafai kuingia nae Ikulu.
Usikurupuke acha hasira jamaa wapo so strategic hope muda si mrefu utona taarifa but pia si kila taarifa itolewe na kurugenzi ya habari acha watu nao waone waseme' kama maafa huwezi tangaza umetoa msaada this is just like a sadaka.
 
Mchana huu nilikuwa napita pale sinza vatican bondeni nikakuta msafara wa magari ya CDM wakiwa na Aikael. Sikuweza kusimama ila nimeona pickup zikiwa na mizigo ya vyakula kwa ajili wa wahanga wa mafuriko maeneo yale

Bila shaka ulikuwa unamaanisha 'waathirika' wa mafuriko. Wahanga wale jamaa wanaojiua pamoja na maadui wao.
 
CUF nao hawajapeleka na NCCR VIPI KWANI WAKIONA CDM WAMEFANYA JAMBO HAWACHELEWI KUIGA
 
ccm wametoa sh milion 4 huku chadema wametoa milion 24 cuf nccr bado hawajawasilisha
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kimetoa msaada wa vyakula na vitu mbalimbali vyenye thamani ya Shilingi
Milioni 25 kwa Wahanga wa Mafuriko katika Jiji la Dar es Salaam. Viongozi wa Chadema wakiongozwa na Mwenyekiti wao Freeman Mbowe pamoja na Naibu Katibu Mkuu Zitto Kabwe walitembelea Makambi yote ya Jiji la Dar na kutoa msaada wa Vitu Mbalimbali.

Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe amesema zoezi hili litaendelea leo baadae kwa kutembele nyumba mojamoja za wale ambao wako mbali na Makambi ili kuwapa Msaada kidogo waliojaliwa.

Kwa habari zaidi tembelea Chadema TV: www.chadema.tv
 
Inaonesha how CDM walivyocommited 25m. 4m waliotoa ccm inatosha kwa waathirika wote? 25m ni sawa na $15,822 ni kiasi kikubwa kuliko $3000 zilizopelekwa kwa wajapan. Nimetoa haya maelezo kwa sababu kuna mtu alihoji hapa.
 
CHADEMA watembelea wananchi walioathirika na mafuriko DSM na kupewa hali halisi ya madhara yaliyowakumba wakaazi wa maeneo ya mafuriko na kupatiwa taarifa za kitaalamu za afya na miundo mbinu ilivyoathirika.

Pia CHADEMA wametoa kiasi cha T sh. 25 Milioni kama mchango wake kwa wahanga wa mafuriko DSM.

Tazama video ya ziara hiyo ktk YOUTUBE - CHADEMATV - chadema taoa msaadakwa wahabga wa mafuriko
 
Pongezi zao wote waliojitolea kwa hali, mali, na dua kwa ajili ya wenzetu walioathirika na mafuriko. Kwa tasisi za kisiasa, CHADEMA waliotoa T.Shs. 25,000,000/= (milioni ishirini na tano) na CCM T.Shs. 4,000,000/= (milioni nne) wameonesha mfano kwamba kumbe linapotokea tatizo la kitaifa SOTE NI WAMOJA bila kujali itikadi zetu.

Hata hivyo, kutokana na hali tete ya UFISADI uliotamalaki serikalini na kutokana na AGIZO la Mh. Rais na viongozi wengine mbalimbali wa serkali kuwataka wananchi husika wahame, nilitegemea CHADEMA waende mbali kidogo na kama hawakufanya hivyo nawashauri:-

(i) Kuitaka serikali, na kimsingi huu ni wajibu wake, kuhakikisha wananchi wote waliopoteza makazi yao wanapatiwa makazi mapya na serikali katika maeneo salama. Haitoshi tu kusema hameni au kuwapatia viwanja "maporini" bila kuwezeshwa na ukizangatia hali halisi ya wananchi kiuchumi. Tafadhali toeni tamko linaloeleweka.

(ii) Endapo wananchi kweli watahama maeneo yao "natabiri" mafisadi na "wawekezaji" watapatiwa maeneo husika mara moja tena kwa kasi ya ajabu. CHADEMA na taasisi nyingine mnao wajibu wa kulitaka Bunge (bahati mbaya hatuna Bunge makini zaidi ya umakini kwenye posho) kutunga sheria kali ya KUHIFADHI MAENEO HUSIKA DHIDI YA UVAMIZI WA MAFISADI.

(iii) Endapo Bunge litashindwa kutunga sheria na serikali kuuza maeneo husika mnao wajibu wa kuuambia umma mapema nini cha kufanya leo na kama ikishindikana leo basi hapo baadaye endapo mtapata ridhaa ya kushika dola. Hili ni muhimu na kusiwe na mzaha. Inapaswa kueleweka tangu sasa kwamba SHERIA ZOTE ZA KIPUUZI zitakazomilikisha maeneo haya kwa mafisadi ZITATENGULIWA ili kila fisadi aelewe hivyo kungali mapema.

Nawasilisha kwa CHADEMA na taasisi nyingine makini za kiraia.
 
Wazaramo ndo wajue nani aliye nao wakati wote. CCM wanaowavisha t-shirt mpauko miaka mitano huku ikiwasahau sikuzote hizo au vinginevyo.
Hawa waswahili wanachosha sana.
 
Back
Top Bottom