CHADEMA: Watanzania tusiwanyanyapae wenye ulemavu

JK wapi Bajaj za kuwabeba wajawazito....Ccm wanamizaha sana.
 
Oh cdm wakorofi,wahaini,serikali itakosa maneno safari hii. Mwanzo kikwete kawaita baraza la usalama wa taifa kupitisha mil.8.5 za kuwalipa waliowapiga kwa mabomu gongo la mboto,leo hii mlemavu aliyeumba na Mungu anapewa msaada ulioandaliwa ndani ya masaa. Una thamani 6.3 mil. Hii ni mara mia ya ile ya jk ya mabomu. Mi sina la kusema naomba kila neno zuri duniani limwendee MBOWE ,SLAA(dr.) pamoja na Chadema. Namshukuru Mungu.
 
kikwete alisema 2014 atawanunulia bajaji wajawazito wa vijijini.
Duuuh tunaye rais kiraka ile mbaya
 
Hongera CDM kwa msaada mnono kwa huyo mlemavu ila naomba kuuliza. Hivi Bukoba kuna mlemavu mmoja tu?? na kama ni mmoja sawa ila ninavyokumbuka yule mdada albino aliyekatwa mikono yote yuko hai na yuko hapo hapo bukoba mbona hajapewa msaada? au huyo ni ndugu yake shemeji????

yupi uyo mkuu? Bukoba au biharamulo? Mkuu albino yupi uyo?tuweke wazi basi!!
 
yupi uyo mkuu? Bukoba au biharamulo? Mkuu albino yupi uyo?tuweke wazi basi!!

Ni mdada fulani alionekana mara nyingi kwenye TV zoote akielezea jinsi jamaa walivyo mkata mikono yake yote miwili. nafikiri yupo bukoba. jina limenitoka, ila mara ya mwisho alikua KCMC kwa ajili ya mikono bandia ila hakuwezekana.
 
MNYONGE MNYONGENI HAKI YAKE MPENI

Rais Kikwete Ampatia Mlemavu Bajaj


Rais Jakaya Kikwete akikabidhi usafiri aina ya Bajaji kwa mwanamke ambaye ni mlemavu anaefahamika kwa jina la Sara Mageni Sanga aliyekaa chini katika kijiji cha Lupalilo, Wilayani Makete, mkoa wa Iringa jana jioni. Pembeni ya Rais kwa upande wa kulia ni mkuu wa mkoa wa Iringa Bwana Mohamed Abdulaziz



Source: Rais Kikwete Ampatia Mlemavu Bajaj « MTAA KWA MTAA

Akawa amemaliza hapo?
Hela ya mafuta anatoa wapi?
Vipi kuhusu chakula?

Don't give me a fish,but teach me how to fish!
Kwanini asinge mfungulia kibanda /duka kwa hiyo hela alonunua bajaji?
 
Back
Top Bottom