kazuramimba
Senior Member
- Jun 14, 2011
- 126
- 57
Kiukweli mimi nimekwisha choshwa kabisa na hawa CCM yaani sina hamu nao hata kidogo.Nimekuwa nikiwaona CDM kama mkombozi wa hili jahazi ambalo linakaribia kuzama.Lakini nimeanza kupata wasiwasi kuwa huenda hadi tutakapo fika 2015 Chadema ikajikuta haina jipya kwa wananchi. Tuweni wakweli maandamano ya CHADEMA hasa kanda ya ziwa yalikuwa yakipinga malipo ya DOWANS hili ni kosa kubwa sana ambalo CDM walifanya nionavyo mimi walitakiwa wapinge kila kitu hadi mitambo ya kampuni hii ya kifisadi sasa magamba wamewapiga kanzu kwenye kuminanane wakiwa hawajui la kufanya huku Bi clinton akifunga goli kwa kisigino sasa hatutakaa tusikie jina la Dowans tena!lakini pia swala la katiba limekua kama ajenda ya CCM wamejidai wanalishuhulikia huku wakija na miswada japo kuwa imekuwa hairidhishi . Si ajabu CCM Wakaanza kuwajibishana wakati huohuo tukasikia mapacha watatu wakijiuzulu kama alivyofanya makamba! Nionavyo CCM wamesha anza kujibu hoja za chadema kimyakimya na taratibu wameanza kujitoa kwenye mashimo waliokuwa wamejitumbukiza CDM wasiposhtuka 2015 watajikuta hawana pakusimamia.sijui nyie mnasemaje.