CHADEMA wasipo kuwa makini yanaweza ya kawapata kama ya NCCR ya Mrema 2015

Tukundane

JF-Expert Member
Apr 17, 2012
11,455
8,247
Cdm ni chama ambacho kimetokea kupendwa na wananchi wengi hasa vijana na wasomi wengi hivyo kuaminika kuwa huwenda ndio chama pekee chenye wasomi wengi kuliko chama chochote tz na kimekuwa tishio kubwa kwa ccm.

Kutokana nakupata wanachama wengi vijana wa mijini, vijijini, wazee na umati mkubwa unaohudhuria mikutano yao imejengeka imani kwa baadhi ya wanacdm kuwa wanaweza kuishinda CCM kirahisi wakati si kweli.

Ieleweke kwamba wapenzi wengi wa cdm ni vijana walioko shuleni na wengine ndio wamehitimu elimu zao hivyo walio wengi hawana shahada za kupigia kura. Kinachotakiwa kwa cdm ni kuhakikisha kuwa wafuwasi wao wanajiandikisha kwenye daftari la wapiga kura pindi mda utakapo fika hadi vijijini.

Kuwa na wapenzi wengi kwenye chama na umati mkubwa kwenye mikutano yenu bila kuwa na wapiga kura hakutoshi kuiondoa CCM madarakani. Ambayo haiko tayari kuachia madaraka kizembe. Bila hivyo CHADEMA watajikuta wanalambishwa mchanga na CCM ambayo ina mtaji mkubwa wa wazee na kutoka vijijini kama ilivyo fanywa NCCR ya Mrema.
 
Usifananishe NCCR ya Mrema na CDM au nenda Arumeru utajifunza kitu...
 
Wewe hauko Tanzania.

Wazee gani na vijiji vya wapi unaposema ni mtaji wa ccm kuishinda CHADEMA?

Hao vijana wasiokuwa na shahada za kupigia kura umewaona wapi?

Btw, CHADEMA ni chama kilicho makini sana, siasa zake hazifanani katu na siasa za NCCR iwe ya Mrema ama ya Mbatia.
 
We mleta thread ni Mbwiga na kilaza mkubwa! Hebu tutolee ujuha wako hapa. Ebooooo!
 
kwa taarifa yako hata daftar la wapiga kura mwakani linaweza likajaa watu zaid ya mil 42 kwa sababu watu wanataka mabadiliko upo?
 
Nakubaliana na wewe wanafunzi hasa wa chuo hawapigi kura, kazi yao kubwa ni kulalamika na kunung'unika tu angalia hivi majuzi uchaguzi wa DARUSO hawapigi kura.

Mi nashindwa kuelewa inaelekea elimu bado haijawakomboa, maneno tu, CHADEMA wachukue tahadhari sana na hawa wasomi wa vyeti na wasiojiandikisha na wasiopiga kura
 
Nakubaliana na wewe wanafunzi hasa wa chuo hawapigi kura, kazi yao kubwa ni kulalamika na kunung'unika2 angalia hivi majuzi uchaguzi wa DARUSO hawapigi kura, Mi nashindwa kuelewa inaelekea elimu bado haijawakomboa, maneno 2, CDM wachukue tahadhari sana na hawa wasomi wa vyeti na wasiojiandikisha na wasiopiga kura
No, CDM wachukue tahadhari sana na Tume ya Uchaguzi yenye wasomi wa vyeti na wasiotumia maarifa na uaminifu wakati wa kuendesha zoezi la kupiga kura!
 
Mkuu, naomba usiishie kwenye mitandao peke yake, cdm wanahamasisha sana watu wajiandikishe kupiga kura wakati wa kuboresha daftari ukifika. Kwa thread hii, unajionesha wazi kwamba hujawahi kwenda kwenye mikutano yao!
Mwisho naomba nikukumbushe tu kwamba, huna haja ya kusubiri cdm kuhamasisha vijana au yeyote akajiandikishe. Kama unataka mabadiliko ya kweli kwa nchi yako, chukua jukumu hilo kwa kuhamasisha marafiki, ndugu, wake, watoto, jamaa na washkaji zako wakajiandikishe kupiga kura na kuzitunza shahada zao!
Ni hayo tu!
 
Nakubaliana na wewe wanafunzi hasa wa chuo hawapigi kura, kazi yao kubwa ni kulalamika na kunung'unika tu angalia hivi majuzi uchaguzi wa DARUSO hawapigi kura.

Mi nashindwa kuelewa inaelekea elimu bado haijawakomboa, maneno tu, CHADEMA wachukue tahadhari sana na hawa wasomi wa vyeti na wasiojiandikisha na wasiopiga kura

Usifananishe na 2010 ambayo kweli watu waliamini hata wakijiandikisha ccm itachukua, lakini kwasasa wameerevuka tathmini ya kwanza ni juhudi tunazozifanya kwenda kwenye mikutano ya CDM, na uhamasisho kwenye midahalo ya moja kwa moja fb na hata forum kama hii
 
mleta hoja, kwa kadri ya uelewa wangu,kaleta angalizo la kifalsafa kwamba adhaniaye amesimama aangalie asianguke na tena CDM tusibweteke tuzidishe mapambano maana CCM wanarusha mateke kama ya mbogo au farasi aneyeelekea mautini,ni pigo la hatari hilo.
Big up,falsafa hii ifanyiwe kazi kuelekea 2015
 
mwaka unaoutaja hakukuwa na nccr bali kulikuwa na mrema na ccm na kama si mwalimu ccm ilishakula mwereka wa mrema.
kumbuka mwalimu aliiokoa ccm mdomoni mwa maalim seif.
2015 wakamfufue mwalimu aje awachomoe tena katika meno ya chadema.
 
We mleta thread ni Mbwiga na kilaza mkubwa! Hebu tutolee ujuha wako hapa. Ebooooo!
Hii kali mtu anae kupaushauri wakukuwezesha wewe kushinda anakuwa juha ukae ukielewa kuwa palipo na ushindani hata kushindwa kupo isipokukuwa hutakiwa kukiri kushindwa ilikuepuka kumpa adui yako nafasi.tz hii ni kubwa kama hayaniliyo yaeleza kwako hayapo basi niliko nimeyaona siyo vizuri kushikilia moja tu la ushindi bila kuendelea kuuongezea mbinu ushindi huo unao utafuta vinginevyo utajikuta unashindwa na adui ulie kuwa unategemea kumshinda.mtu anapotoa ushauri haina maana kuwa haitakii mema cdm la asha ninamna tu ya kujaribu kuliokoa taifa letu.kwani wengi tumepigika tunahitaji ukombozi wa kweli.
 
We mleta thread ni Mbwiga na kilaza mkubwa! Hebu tutolee ujuha wako hapa. Ebooooo!
Hii kali mtu anae kupaushauri wakukuwezesha wewe kushinda anakuwa juha ukae ukielewa kuwa palipo na ushindani hata kushindwa kupo isipokukuwa hutakiwa kukiri kushindwa ilikuepuka kumpa adui yako nafasi.tz hii ni kubwa kama hayaniliyo yaeleza kwako hayapo basi niliko nimeyaona siyo vizuri kushikilia moja tu la ushindi bila kuendelea kuuongezea mbinu ushindi huo unao utafuta vinginevyo utajikuta unashindwa na adui ulie kuwa unategemea kumshinda.mtu anapotoa ushauri haina maana kuwa haitakii mema cdm la asha ninamna tu ya kujaribu kulikoa taifa letu.kwani wengi tumepigika tunahitaji ukombozi wa kweli.
 
Cdm ni chama ambacho kimetokea kupendwa na wananchi wengi hasa vijana na wasomi wengi hivyo kuaminika kuwa huwenda ndio chama pekee chenye wasomi wengi kuliko chama chochote tz na kimekuwa tishio kubwa kwa ccm.

Kutokana nakupata wanachama wengi vijana wa mijini, vijijini, wazee na umati mkubwa unaohudhuria mikutano yao imejengeka imani kwa baadhi ya wanacdm kuwa wanaweza kuishinda CCM kirahisi wakati si kweli.

Ieleweke kwamba wapenzi wengi wa cdm ni vijana walioko shuleni na wengine ndio wamehitimu elimu zao hivyo walio wengi hawana shahada za kupigia kura. Kinachotakiwa kwa cdm ni kuhakikisha kuwa wafuwasi wao wanajiandikisha kwenye daftari la wapiga kura pindi mda utakapo fika hadi vijijini.

Kuwa na wapenzi wengi kwenye chama na umati mkubwa kwenye mikutano yenu bila kuwa na wapiga kura hakutoshi kuiondoa CCM madarakani. Ambayo haiko tayari kuachia madaraka kizembe. Bila hivyo CHADEMA watajikuta wanalambishwa mchanga na CCM ambayo ina mtaji mkubwa wa wazee na kutoka vijijini kama ilivyo fanywa NCCR ya Mrema.
usiogope, huu moto ni mkubwa.
 
Back
Top Bottom