CHADEMA wanani dissapoint kwa kweli

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
49,110
115,886
Nimevumilia sana kutokusema but nimeshindwa sasa
inabidi niseme tu kilicho moyoni kwangu.

Kwa ufupi nashangazwa na busara za CHADEMA na Dk Slaa.

Mimi ni katika wale ambao nimesha give up na CCM.
Chochote watakachokifanya kikiwa kibaya sishangai na kikiwa kizuri
kwangu hakivutii.

Sasa nilitegemea CHADEMA wawe tofauti saana lakini
wanayoyafanya mimi naona kama hawapo serious kabisa.

1. La kwanza ni hili la kujaribu na kujibizana na watu wa CCM,
kwanza kwa nini chadema wana react na mambo ya CCM?
Mfano mkutano mkuu wa ccm na suala la kujivua gamba?

Kwa nini kwa mfano chadema walishindwa nini kudharau na
kutokuongea lolote, badala yake wakawa wanazungumzia
namna ya kupunguza gharama za maisha zinazopanda, na namna
ya kuwafaidisha watanzania na zoezi la mjadala wa katiba mpya?

2. Kwa nini wasizungumze ni vipi katiba mpya itawasaidia watanzania
kupambana na rushwa, ufisadi na matatizo mengine?

3. Imeandikwa kwenye media kuwa, watuhumiwa wa ufisadi
watawatumia viongozi wa vyama vya upinzani kumtukana Kikwete
na familia yake, na siku haipiti Dk Slaa anaanzisha madai ya Ridhiwani?

Imean hata kama yuko right,what about the wrong time?
kwa nini now wakati inatangazwa maadui wa Kikwete watakitumia chama cha upinzani?

4. Tazama hili la Nape na CHADEMA, nani anaefaidika kama sio
watuhumiwa wa ufisadi, maana sasa hawazungumzwi wao.
attention imehama kutoka kwao. Kwa msaada wa Dk Slaaa.

5. Hivi hata kama Nape alitaka kujiunga HADEMA au CCJ, kumuumbua huko
kunaleta faida au hasara kwa CHADEMA?

6. watu wengine walio CCM nao wangependa kuondoka, wanaonaje?


Hivi CHADEMA hawawezi kuzungumza kuhusu mustakabali wa tanzania bila
kuzungumzia CCM kwa jazba?

Mimi nakuwa dissapointed na CHADEMA.

Kwa sababu hata wakati wa uchaguzi, Mbowe na wenzie wa CHADEMA
walinishangaza walipomlalamikia Kikwete kufanya kampeni baada ya muda rasmi
kupita, badala ya CHADEMA kupinga hiyo sheria ya kipuuzi ya kuweka limit ya masaa ya kampeni.
 
Labda wana technique kama ya USA kumuondoa kwanza mwanzilishi wa ugaidi.. na kwa case hii wanataka kwanza ku-deal na mzazi wa mafisadi.
 
Tuliambiwa tusiwachague wanaonekana wakati wa uchaguzi tuu. Tukasema sawa tukawapa CCM japo tunajua "hatukuwapa" bali walijipa kura zetu wenyewe...

Nimekaa kidogo kila nikisafiri kila mkoa sasa ni CHADEMA CHADEMA CHADEMA.... Yaani kama unapenda CCM waweza ugua ule ugonjwa wa ukichakaa kama malaria sugu.


Sasa nimeshangaaa CCM wamekiri kuwa CHADEMA si chama cha msimu na wanaomba jamii iwaonee huruma wao kwa kupiga mbiu CHADEMA ni cha kidini(waislamu na wakristo) na ukabila(makabila kama 120 hivi). Maana wakati tunaenda kupiga kura waliochagua CHADEMA kwa wingi nimesikia ni wasukuma kule Shinyanga na Mwanza. CHADEMA chama cha kikabila cha wasukuma. Baadae nikaambiwa na Mbeya nikagundua kumbe hiki ni cha kikabila wasafwa, wanyakyusa na wengine.

Nikaendelea na safari yangu kama kawaida nchi nzima. Kufika kibaha nikaambiwa Mgombea wa CHADEMA alishinda akachakachuliwa kwa kuwa mgombea wa CCM Silvestry Koka pale mjini ni mkristo halafu Habibu wa CHADEMA ni muislamu. Wakadai kuwa "eti" pale kibaha kuna waislamu wengi kwa hiyo walimchagua Habibu kwa kuwa ni muislamu. Nikagundua kumbe CCM wanaposema CHADEMA cha kidini kumbe kweli maana huyu mgombea muislamu alipata kwa sababu hiyo.

Cossortium de facto le pressee'..... Hoja haiwezi kuwa hoja mpaka ujiridhishe kwanza
Nawasilisha.
 
Mimi nakubaliana kabisa na The Boss niwakati sasa CDM wawe wanatoa changamoto kwa serikali kuimarisha uchumi wetu na si kutupiana maneno. Yaani uongozi mzima wanatupiana maneno na kila mtu anaowarushia mfupa.

Mimi nazani wamuachie Mtikila kwa vile yeye ni kama anashinda mahakamani huko anaweza shinda mafisadi na kutupa updates. Viongozi wengine wawe mfano bora huko bungeni na kuiwajibisha serikali katika kutoa zile huduma tunazolipia kama umeme.

Waweke kama sera tukikosa umeme siku kazaa watufulani wajiuzuru manake watakuwa wameshindwa kutupa kipaumbele na kueka miundo mbinu ya vitu kama emegency power supply.

Hivi ndo tunaweza zuia ufisadi usitokeee kama wa Richmond. Walikiwa wanasema wanatupatia umeme wakati tulikua tunateseka tuu na mgao miaka nenda rudi. Kama kungekua na sera za kuwajibisha watu na wengine kujiuzuru tungewashutukia mapema, sio kushituka wakati tumeshaingia hasara mabilioni na watu tulishawachoka sasa na wanaendelea kudunda wana nyumba, magari na mabank akaunti yao yamenona siye tukitaabika na bado twa taabika.
 
You are very right mkuu.... kinachoendelea sasa kinatukumbusha - "MCHIMBA KISIMA, KAINGIA MWENYEWE"

while it is important kwa chadema kuendelea kuanika uovu wa mafisadi, nadhani umefika wakati wa chama ku-mordenize, strategize na reform

potentials ni nyingi sana
 
CCM wanakivuta CHADEMA kwenye malumbano, hii inasababisha CHADEMA i-withdraw attention kwenye mambo muhimu.

CHADEMA walivyoanza suala la katiba yakaja mabomu ya gongo la mboto, walivyokuja na dowans isilipwe akajitokeza babu wa Samunge, sasa wanahubiri ugumu wa maisha huku kuna kuvuana magamba CCM.
 
Hivi ukiwa vitani, akitokea mwenye panga utamwacha sbb wewe unamtafuta mwenye bunduki? Niwakumbushe kidogo, wakati ule wa uchaguzi mkuu Makamba alikuja na story ya unyumba wa Dk.Slaaa na upadri wake alipopigwa lile dongo la kumpa mimba mwanafunzi akawa mpole akafunga mdomo hatukumsikia tena.

Akaibuka Six na kupinga hoja ya elimu bure eti haiwezekani akaambiwa yeye si msafi na ni fisadi kama wenzake akakumbushwa ile ofisi ya spika ya millioni 500 kule jimboni kwake akawa mpole akanyamaza.

Akaibuka Kinana, akapewa dozi yake kuhusu ufisadi wa zile meli zake na akaambiwa makombora mengine bado akatulia akaanza kuongea sera personal attack akaacha.

Akaibuka Shimbo, akapewa dozi yake ya tenda za kifisadi alizopewa na JK nae hatukumsikia tena. Kilichoponza Riz1 ni yeye na gazeti lake kumsakama kuisakama CDM kapewa dozi yake katulia.

Huyu Nape kajiingiza mwenyewe safari hii Dk katulia Marando na Mpendazoe wakampa dozi yake. Nape kashakuwa mpole baada ya hapo maandamano na kuwaeleza wananchi ukweli yako pale pale.
 
CCM wanakivuta CHADEMA kwenye malumbano, hii inasababisha CHADEMA i-withdraw attention kwenye mambo muhimu.

CHADEMA walivyoanza suala la katiba yakaja mabomu ya gongo la mboto, walivyokuja na dowans isilipwe akajitokeza babu wa Samunge, sasa wanahubiri ugumu wa maisha huku kuna kuvuana magamba CCM.

Mkuu wakati mwingine huwezi kushambulia tu bila kudefend, CCM walianza kutamba kuwa chama kimebadilika ilikuwa ni muhimu kwa CDM kuwakumbusha kuwa nyoka hata kama akivua gamba atabaki kuwa nyoka....Na huyu dogo Nape alianzisha yeye personal attck na kejeli kwa CDM ilikuwa ni muhimu kumjibu..baada ya hili bomu la Mpendazoe nape ataonekana ni msaliti ndani ya chama na ile imani kwa wenzake itakwisha, ndo maana unaona Chiligati na Mukama hawaatack personal za mtu, Nape anatakiwa alinganishe sera na kuwaonyesha wananchi jinsi sera zao zilivyo bora kuliko za chadema yeye anafanya personal attack...hiyo dozi iliyopata itamnyamazisha na kuwa CDM advantage sbb upande wa CCM kila mtu ataogopa kujiweka front
 
Kweli kabisa CHADEMA inabidi ishughulike na mambo ya wananchi kuendelea kujibizana na CCM ni kupoteza attention ya mambo ya msingi nakuunga mkono mkuu THE BOSS
 
Me nashangaa sana huu utamaduni wa watanzania kutokupenda kukosolewa au kuambiwa ukweli pale inapobidi. Naiona hii hali hata humu ndani JF Kila mtu akipost mada ya kuikosoa CHADEMA basi atatukanwa na kuitwa mtoto wa mafisadi.

People inabidi mjifunze kudigest different ideas. Inabidi tujenge utamaduni wa kukubali kutokubaliana. JUST BECAUSE NAIKOSOA CHADEMA IT DOESNT MEAN MIMI NI CCM, I CAN BE INDEPENDENT.

Katika chaguzi nyingi duniani wanaoamua mshindi ni watu kama mimi because sina chama so i can vote to chama chochote ambacho kina sera nzuri. Tofauti na watu ambao wenyewe ni wapenzi wa vyama, hata vyama vyao vikifanya madudu wanavipigia kura tu.

MAPENZI HULETA UPOFU, I dont support CCM 4 any mean kwani najua 80% ya matatizo yanayolikabili taifa letu yamesababishwa nao, na kama wangekuwa na gut wangeweza kuyamaliza yote.

The same time siwez tu kuisuport CHADEMA sababu tu ni chama cha upinzani kikuu wakati kuna madudu kibao nawaona wakifanya.

CHADEMA INABIDI WABADILIKE, UMAARUFU WAO UMEKUJA GHAFLA MNO AND THATS BAD, inabidi wafanye reform kubwa sana katika utawala na kurecruit watu.

ASIKWAMBIE MTU VINGINE, UKWELI NI KUWA NGUVU YA CHAMA CHOCHOTE CHA SIASA INAANZIA KWENYE MATAWI YA NYUMBA KUMI KUMI. HUKO NDIO KWA KUINVEST NA KUMWAGA MAPESA, NA SIO MAANDAMANO NA MIKUTANO ISIYO NA TIJA.

CHADEMA wafukuzeni CCM kimya kimya bila makelele kwa kukijenga chama katika nyumba kumi kumi.

Msinitukane wazee ni maoni tu.
 
Broda,

Getting dissapointed is not the best way to level the ground!

How many times have you been available to suggest, advise, or give opinion, and then some staff from cdm rejected the stuff?

There are so many ways by which one could systematically channel upward his/her vision, or grievances, and the concerned takin proper reaction, and or answer on applicabilities!

Kama tuna ushauri, mbali ya kuuweka hapa ni vizuri tukau-PM kwa wakubwa hao (maana ni members)ili waupate ushaurri huo kwa uhakika, ambapo katika hali ya kawaida si rahisi mtu akasoma kila post!

Otherwise the advise is highly a material!
 
Siasa za chuki siyo nzuri, kwani wewe waweza kufurahia kwa kupandikiza chuki ukidhani ndio upenyo wa kutokea lakini siku chuki ikiiva na ikalipuka hata mwenyewe utakuwa mhanga.

Chadema inatembea nchi nzima kupandikiza chuki kwa wananchi juu ya serikali yao, wanaweza kuona wako sawa lakini siyo sawa, kwani hata kama njia hiyo ikiweza kuwaingiza madarakani basi zile sentensi zao za nchi haitawaliki nadhani kipindi hicho ndio itakuwa wakati wake muafaka.

Uchaguzi uliopita kenya Laila alikuwa anakubalika sana lakini kaa na wakenya usikilize kama bado ana vote. The Boss nimekubali post yako iko kiuzalendo zaidi. Thanks Boss
 
The Boss siasa ina vionjo vyake, usifikiri CCM ni wajinga kutafuta mavuvuzelaaa! Kuna logic,

  1. Ni kumfanya mtu aliyekubalika na jamii aonekane hafai, ataonekanje hafai kama si kuzungumzia mambo yake binafsi ya sirini? Umesahau uchaguzi uliopita mke wa Slaa alizua gumzo?
  2. Sera na mipango vyote viko wazi, hivyo pamoja na kuwaeleza wananchi ni strategy zipi zitatumika kuwakwamua katika dimbwi la umaskini uliotopea lakini bado vijembe vinabaki kuwa ni chorus ya siasa bila kusemana kidogo mambo hajaendi.
 
CCM imetangulia mbele CDM inafukuza nyuma na hili ni ujinga au umbumbu wa Chadema kutokujua siasa! Wameacha Concentration ya agenda zao na kuwa na agenda za mlipuko! Leo Ridhiwani,kesho CCJ na Nape,magamba ya CCM,Tutapiga kura ya maoni kumuondoa JK,sukari ishuke bei,Mh Sugu atakua Mbunge wa Kyela,mshahara wa Dr Slaa umebalikiwa na Kamati kuu,CCM haina ubavu wa kuwaondoa mafisadi,Magari mabovu ya Mbowe ni lazima chadema inunue............porojo kibao!
 
Back
Top Bottom