Mzito Kabwela
JF-Expert Member
- Nov 28, 2009
- 18,857
- 7,615
Nimevumilia sana kutokusema but nimeshindwa sasa
inabidi niseme tu kilicho moyoni kwangu.
Kwa ufupi nashangazwa na busara za CHADEMA na Dk Slaa.
Mimi ni katika wale ambao nimesha give up na CCM.
Chochote watakachokifanya kikiwa kibaya sishangai na kikiwa kizuri
kwangu hakivutii.
Sasa nilitegemea CHADEMA wawe tofauti saana lakini
wanayoyafanya mimi naona kama hawapo serious kabisa.
1. La kwanza ni hili la kujaribu na kujibizana na watu wa CCM,
kwanza kwa nini chadema wana react na mambo ya CCM?
Mfano mkutano mkuu wa ccm na suala la kujivua gamba?
Kwa nini kwa mfano chadema walishindwa nini kudharau na
kutokuongea lolote, badala yake wakawa wanazungumzia
namna ya kupunguza gharama za maisha zinazopanda, na namna
ya kuwafaidisha watanzania na zoezi la mjadala wa katiba mpya?
2. Kwa nini wasizungumze ni vipi katiba mpya itawasaidia watanzania
kupambana na rushwa, ufisadi na matatizo mengine?
3. Imeandikwa kwenye media kuwa, watuhumiwa wa ufisadi
watawatumia viongozi wa vyama vya upinzani kumtukana Kikwete
na familia yake, na siku haipiti Dk Slaa anaanzisha madai ya Ridhiwani?
Imean hata kama yuko right,what about the wrong time?
kwa nini now wakati inatangazwa maadui wa Kikwete watakitumia chama cha upinzani?
4. Tazama hili la Nape na CHADEMA, nani anaefaidika kama sio
watuhumiwa wa ufisadi, maana sasa hawazungumzwi wao.
attention imehama kutoka kwao. Kwa msaada wa Dk Slaaa.
5. Hivi hata kama Nape alitaka kujiunga HADEMA au CCJ, kumuumbua huko
kunaleta faida au hasara kwa CHADEMA?
6. watu wengine walio CCM nao wangependa kuondoka, wanaonaje?
Hivi CHADEMA hawawezi kuzungumza kuhusu mustakabali wa tanzania bila
kuzungumzia CCM kwa jazba?
Mimi nakuwa dissapointed na CHADEMA.
Kwa sababu hata wakati wa uchaguzi, Mbowe na wenzie wa CHADEMA
walinishangaza walipomlalamikia Kikwete kufanya kampeni baada ya muda rasmi
kupita, badala ya CHADEMA kupinga hiyo sheria ya kipuuzi ya kuweka limit ya masaa ya kampeni.
i411 said:Mimi nakubaliana kabisa na The Boss niwakati sasa CDM wawe wanatoa changamoto kwa serikali kuimarisha uchumi wetu na si kutupiana maneno. Yaani uongozi mzima wanatupiana maneno na kila mtu anaowarushia mfupa.
Mimi nazani wamuachie Mtikila kwa vile yeye ni kama anashinda mahakamani huko anaweza shinda mafisadi na kutupa updates. Viongozi wengine wawe mfano bora huko bungeni na kuiwajibisha serikali katika kutoa zile huduma tunazolipia kama umeme.
Waweke kama sera tukikosa umeme siku kazaa watufulani wajiuzuru manake watakuwa wameshindwa kutupa kipaumbele na kueka miundo mbinu ya vitu kama emegency power supply.
Hivi ndo tunaweza zuia ufisadi usitokeee kama wa Richmond. Walikiwa wanasema wanatupatia umeme wakati tulikua tunateseka tuu na mgao miaka nenda rudi. Kama kungekua na sera za kuwajibisha watu na wengine kujiuzuru tungewashutukia mapema, sio kushituka wakati tumeshaingia hasara mabilioni na watu tulishawachoka sasa na wanaendelea kudunda wana nyumba, magari na mabank akaunti yao yamenona siye tukitaabika na bado twa taabika.
You are very right mkuu.... kinachoendelea sasa kinatukumbusha - "MCHIMBA KISIMA, KAINGIA MWENYEWE" while it is important kwa chadema kuendelea kuanika uovu wa mafisadi, nadhani umefika wakati wa chama ku-mordenize, strategize na reform potentials ni nyingi sana
Kweli kabisa CHADEMA inabidi ishughulike na mambo ya wananchi kuendelea kujibizana na CCM ni kupoteza attention ya mambo ya msingi nakuunga mkono mkuu THE BOSS
Siasa za chuki siyo nzuri, kwani wewe waweza kufurahia kwa kupandikiza chuki ukidhani ndio upenyo wa kutokea lakini siku chuki ikiiva na ikalipuka hata mwenyewe utakuwa mhanga.
Chadema inatembea nchi nzima kupandikiza chuki kwa wananchi juu ya serikali yao, wanaweza kuona wako sawa lakini siyo sawa, kwani hata kama njia hiyo ikiweza kuwaingiza madarakani basi zile sentensi zao za nchi haitawaliki nadhani kipindi hicho ndio itakuwa wakati wake muafaka.
Uchaguzi uliopita kenya Laila alikuwa anakubalika sana lakini kaa na wakenya usikilize kama bado ana vote. The Boss nimekubali post yako iko kiuzalendo zaidi. Thanks Boss
Nakubaliana na mtoa mada kuna mambo ya msingi ambayo CHADEMA wanaweza kuzungumza zaidi ya CCM na ufisadi.
Sijaona PWENTI hata moja ........kama mmetumwa na Msekwa kamwambie CHADEMA ndio kwaaaaaaaaaaaanza kumekucha!