CHADEMA wana kazi kubwa ya kuwapata Katibu Mkuu na Mgombea Urais 2020

Chadema haifanyi mambo kwa mkurupuko,kila mwaka munaibuka na hoja dhaifu.........mulisema kitakufa kabla ya uchaguzi ulioisha, uchaguzi umeisha na waliotabiri chadema itakufa ndio na ubunge wamekosa......we subiri utasikia kishindo cha katibu mkuu na mgombea hiyo 2020
 
Inachekesha eti CCM wanatamani upinzani imara. Sasa mabao ya mkono ya nini? Mbona hamtaki hata wakutane kusalimiana? Yanatoka rohoni kweli?
Tatizo lenu kila atakayewaambia ukweli mnamuita mCCM, dalili za mvua ni mawingu endelea kujifunika gunia jeusi.
 
Inachekesha eti CCM wanatamani upinzani imara. Sasa mabao ya mkono ya nini? Mbona hamtaki hata wakutane kusalimiana? Yanatoka rohoni kweli?
Kama kweli upinzani imara mnauhitaji tusingeyaona tuliyowahi kuyaona tangu kule Igunga na kuendelea!Mna wasiwasi na hofu maana hamjui anayechukua nafasi atakuja kivipi .Hazina za watendaji zipo Tele
 
Si kuna TX toka CCM kama walivyo mpata mgombania Urais. Kuna yule aliekuwa KATIBU WA EAC ni TX Mzuri sana toka CCM
 
Chadema haifanyi mambo kwa mkurupuko,kila mwaka munaibuka na hoja dhaifu.........mulisema kitakufa kabla ya uchaguzi ulioisha, uchaguzi umeisha na waliotabiri chadema itakufa ndio na ubunge wamekosa......we subiri utasikia kishindo cha katibu mkuu na mgombea hiyo 2020
Mbona kimekufa mkuu kimebaki kule kwa wakwepa kodi
 
Ulisahau, vituko alianza uchaguzi wa serikali za mitaa akasema CDM ikipata mitaa 10 tu atatembea uchi. Biashara ikapita mitaa zaidi ya maelfu akapitea kimya, ukaja uchaguzi mkuu akasema abaona ACT kuwa chama cha upinzani bungeni, kimepata kiti kimoja na kwa msaada wa CCM yenyewe. Nadhani ifike kipindi thread zake tuwe tunampuuzia Kabisa, kwangu mimi hii ya mwisho kuchangia ujinga wake.
 
Wanaye tayari. Lowassa ndie katibu mkuu. Uone anavyo toa maagizo ya kuinarisha chama. Na mipango ya kufikia 2020.
 
[QUOTI="Lizaboni, post: 14973728, member: 138049"]Kwa kawaida si kuwa nawaongelea bali naandika facts za ndani ya chama hicho[/QUOTE]
Mada iliyo mezani, mkulu anajua kiingreza? Kama anajua mbona kawakimbia mabalozi ndani ya ikulu lakini kaweza kwenda singida kwenye sherehe za ccm zilizojaa mipasho ya kiswahili!?
 
Wadau, amani iwe kwenu.

Ni dhahiri kwamba Uchaguzi Mkuu wa 2015 umemalizika. Kumalizika kwa uchaguzi Mkuu wa 2015 kunatoa fursa kwa vyama vya siasa kujipanga kwa ajili ya uchaguzi ujao.

Mpaka sasa, ni chama cha Mapinduzi pekee ndicho hakina ombwe la Uongozi. Labda wanafuatia ACT. Ila kwa CHADEMA na CUF wao wana shughuli pevu ya kujaza mapengo yaliyoachwa wazi kutokana na viongozi wake wakuu kuachia ngazi baada ya kubakwa kwa mfumo wa kumpata mgombea Urais kupitia UKAWA.

Hata hivyo, CHADEMA wana kazi kubwa mbili mbele yao. Kwanza kumpata Katibu Mkuu ili kujaza nafasi iliyoachwa wazi baada ya Dk Slaa kujiuzulu mwishoni mwa mwezi Julai 2015. Kwa mujibu wa Katiba ya CHADEMA, nafasi hiyo ilipaswa kujazwa ndani ya siku tisini. Hata hivyo mpaka sasa, nafasi hiyo ipo wazi na taarifa zilizopo ni kwamba CHADEMA wamekosa mtu mwenye sifa za kukaribia sifa za Dr Slaa. Kutokana na kukosa mtu ndani ya CHADEMA, chama hicho kikawa na wazo la kumteua Frederick Sumaye kushika nafasi hiyo. Hata hivyo, mapendekezo hayo yanakataliwa na baadhi ya Mahafidhina.

Kazi ya pili ni ya kumpata Mgombea Urais. Ni dhahiri kwamba Edward Lowasa hatakuwa mgombea Urais wa CHADEMA kwa mwaka 2020. Kwani mpaka sasa, imedhihiri kuwa mwanasiasa huyo ameshapoteza mvuto na mwelekeo. Ndani ya CHADEMA mpaka sasa hakuna figure hata moja ya kuivusha CHADEMA 2020. Jicho lao limeangaza tena kwa Sumaye. Hata hivyo, bado hali ni tete kwani Sumaye hana umaarufu wa kumzidi Lowasa. Hivyo kama Lowasa alipigwa kirahisi na Magufuli, sijui kwa Sumaye hali itakuwaje.

Pupa, ulafi na tamaa ya Mbowe ndiyo imewafikisha hapa CHADEMA.
toka mkwele awaombee mkumbukwe basi umekuwa zaidi ya kichaa! fanya kazi halali la sivyo tutasikia umepata bwana
 
Back
Top Bottom