CHADEMA wameshindwa kumuua nyani wameshamwangalia nyani usoni-Like the candle in the wind

Waberoya bwana, more theoretical than practical, more mswahili than technical....hivi we unadhani CCM walivyo ka nguruwe pori aliyejeruhiwa wanatafuta visingizio vya vyama vya kisiasa hususan Chadema kwa kila tatizo linalojitokeza nchini ili waweze kupata loophole ya kuwashughulikia viongozi wa Chadema kwa kesi za uhaini. Na hapo ndo watakuwa wamewamaliza Chadema. Ni kwa bahati nzuri sana Chadema wana viongozi wenye akili sana. Ni chama kichanga lakini nguvu zao si za bunduki, wala mahakama, wala pesa. Nguvu zao zipo kichwani. Hawafikirii kwa tumbo, wanafikiria kwa kichwa. Wanasoma majira na nyakati na wana data za kutoka jikoni hivyo ndugu Waberoya hawawezi kufata ushauri wako. Hiyo itakuwa suicidal move.

Ni jana tu nilikuwa Muhimbili, pale kwenye epicenter ya mgomo wa Madaktari. Kuna rafiki yangu tulisoma wote Mzumbe secondary so nilienda kumtembelea. Nikamuuliza swali hivi ni kwa nini ninyi madaktari katika madai yenu hamtaki kuongelea posho za wabunge kuiaibisha serikali kwamba hela wanazo isipokuwa ni walafi wendawazimu wabinafsi wasiowekeza kwenye vitu vya msingi? Akanijibu, akasema si kwamba hawafahamu hilo ila hawataki kabisa kuyafanya madai yao ya kisiasa. Wanataka kubaki disciplined kwenye fani yao kwamba madai yao yana msingi wa kitabibu na ni makosa kuingiza siasa kwenye utaalamu.

Ni kwa kigezo hicho pia Chadema hawapaswi kujipeleka kimbele mbele kwenye migomo inayoendelea. CCM ni watu hatari sana na wanataka kubaki madarakani hata ikiwa ni kwa vita. Wakipata evidence kidogo tu kwamba chama pinzani sana kwao kinafacilitate migomo basi kwao hawataangalia mantiki ya mgomo bali wataona ni mkakati wa Chadema nchi isitawalike na hiyo inatosha kufungua kesi ya uhaini, kuwasweka gerezani kina Slaa na kukifuta Chama kabisa. Ndio maana kwa wakati kama huu Chadema wapaswa kuwa wajanja kama nyoka lakini wapole kama njiwa.

Hoja zako nyingine za viongozi wa Chadema kukarimiwa Ikulu kumewapunguzia makali ni propaganda za kijinga zisizostahili kujibiwa. Mtu yeyote akienda Ikulu kwa appointment maalumu atakirimiwa tu -- pale kuna hela imetengwa kwa ajili hiyo so mi nashangaa watu wanaoshadadia upuuzi wa dizaini hii. Waberoya siwezi kuamini na wewe unaweza kuzisilimisha akili zako chini kabisa kiwango hiki.
 
smart ya kuvaa koti wakati chini hauna hata kifunika maungo yaani upo na suti ya kuzaliwa nayo huo nao waweza kuwa u smart? ebu wafanye jambo ambalo umma wa watanzania watakubali kuwa hawa jamaa ni smart sio kujifaraghua tu
Mkuu kufanya jambo kwa wananchi wa tanzania yahitaji maandalizi ya kutosha kutokana na ukweli kwamba wengi ni waoga, hawajui haki zao na ndiyo kinachotusumbua mimi na wewe kuzidi kupoteza muda ndani ya mitandao bila kujua kuwa sisi tayari tulishajinasua na hiyo hivyo watu wengine ilibidi tuwapelekee ujumbe na kuwaelimisha.

Naweza kukueleza tu kuwa siyo lazima CDM wapige kengele ndiyo tuwaunge mkono, hata zile alama/ishara/viashiria vya vitendo vinaibuka nchini bado havituamshi? Ndiyo maana nasema, viongozi wa CDM wako smart, kwani wanajaribu kila njia kuhakikisha "The game is over hata kwa nock-out kabla ya 2015" lakini bado inaonekana wabongo wengi wako slow kufanya maamuzi magumu kama serikali yao ya magamba.
 
Mkuu, umeandika mambo mengi sana ya kukilalamikia CHADEMA na viongozi wake.

Mkuu, wewe si ni m-Tz? Kwa nini usianzishe chama chako na kuyatekeleza hayo unayoyalalamikia badala ya kuwataka CHADEMA wakufanyie badala yako?

Wewe una akili kama ulivyojisifia mwenyewe, tumia basi hizo akili zako kuyafanya hayo ambayo CHADEMA wameshindwa.
Nadhani ungekuwa enzi zile za Mwl. Nyerere usingekubaliana naye kuusaka uhuru wa Tanganyika kwa mazungumzo. Ungetaka kuingia msituni na mtutu wa bunduki ili kumtoa mkoloni wakati uwezekano wa mazungumzo ulikuwepo.
 
Hatua hii ya kukutana Ikulu na JK, ilianzishwa na Chadema ambacho kilipinga muswada wa katiba mara mbili.

Chadema waliomba Appointement Ikulu, wakaruhusiwa walivyofika wakafanya mazungumzo na Rais JK, Kisha wakanywa juice,kahawa na Kashata, wakapiga picha na Rais na kuondoka.

Mie wasiwasi wangu unatokana na hii tabia ya kujifungia Ikulu kwa watu wachache na kufanya uamuzi wa watu wengi.

Hivi Chadema kwenda Ikulu, usiku kuzungumza na Rais, wananchi na wafuasi wa Chadema walihusishwa hadharani kuwa wanakwenda Ikulu kujadiliana na Rais?
Kwani Ritz una hasara gani sana sana kwako wewe ni poa bado CDM wakienda Ikulu pamoja na maghambas wenu mnapata muda wa kupumua!!!! Usijali si kila kitu kinachofanywa wewe ujue, zingine ni mbinu za kisiasa ili tukiibuka mabomu yawe machache kama hakuna kabisa!!!!!

 
Mlianza vizuri, mlikuwa mnapiga mbio vizuri nani amewaroga? Nani kawadanganya kuwa hoja zenu nzuri ambazo mlizipeleka ikulu pasi kupata baraka za wanachama wenu..zilibarikiwa? mkafika, mkakaa kwenye makochi na kunywa gahawa na hapo ile nguvu yenu ikapotea, ikatoweka..Ila tukio hili mlilipa sifa na sababu nyingi, “siasa za kisasa, siasa za urafiki, siasa za kutokuchukiana’’ bila ya nyie kujua…

Bila aibu ‘’aliyekuwa rais wa wananchi’’ ambaye akiwa msibani hamuangalii hata jirani yake!!akatamka ‘eti Mheshimiwa Rais watu wanasema mimi nakukwepa!! Nikukwepe kwa sababu gani??...ulivyosema sentensi hii Kikwete akafurahi akajibu ni maneno ya akina michuzi…saa ile roho mtakatifu wa woga na nidhamu ya kufa mtu akakushukia, ukawa mtu mpya..’coward’….Kikwete kwa mara ya kwanza tangu ameingia ikulu akalala usingizi akaota, chama kile kilichosemekana kinatisha kikawa mwisho wake saa ile!

Ni muumini wa siasa za kukaa chini na kuelewana , ni muumini wa siasa za hoja, ni muumini wa siasa za aina ya Lema, ni muumini wa saisa za akina Zito, Ni muumini wa siasa kali na za vurugu…..Lakini uumini upi utumike wapi ndipo huwa sieleweki! CCM hii si ya siasa za kukaa chini na kuelewana, ukifanya hivyo inakula kwako! Maalim Seif anajua hivyo!

CCM hii si chama tawala ni wakoloni weusi, kamwe hawako kwa ajili ya maslahi ya nchi hii…Sahau kuhusu Katiba,dola na kila aina ya vihonjo vinavyompa Rais mamlaka ya urais na utiisho wa urais. Rais akiwa hakubaliwi na kundi fulani dogo tena likiwa na support kubwa ya wananchi hana nguvu hizo, hana mamlaka hayo! Chadema mmeuza haki yenu na sasa mnashangaa wakati nafasi ya ukombozi ndio hii!

Ni Chadema nyie mliojipambanua kuwa ni wakombozi, japo mnatumia slogan ya ‘’nguvu ya umma’’ pengine ngau kwa muda mfupi mngetumia slogan ya Mtikila ‘’ saa ya ukombozi ni sasa’’ japo jamani mwee semeni jambo nchi itikisike…magazeti yauze!!

Chadema inahitaji akili kidogo tu kuwa mgomo wa madaktari ilikuwa ni funguo yenu ya Kikwete(the chief architect wa Richmond) kujiuzulu! Ilikuwa ni nafasi ya kuhamasisha waalimu, nafasi ya kuwaleta na kuwakumbuka wazee wa afrika mashariki….ni nyakati nzuri mngewakumbuka ‘’wahanga wa bodi ya mikopo’’ vyuo vikuu, nafasi ya kuwaunganisha vijana wa mbeya , arusha na DSM wanaojengewa masoko ambayo hawawezi kupanga.

Wakazi wa Mabwepande na kwingineko ndio ilikuwa nafasi… Niseme nini juu ya wananchi wa sehemu mbalimbali kwa nafasi zao ambao wamekata tamaa ya kudai haki zao kwa sababu tu ya vitisho kama vya Pinda? Hivi mkazi wa Gongo la Mboto ambaye analipwa fidia ya laki tano kwa nyumba ya vyumba nane asingekuwepo kwenye maamdamano? Btw mna orodha ya wanaodhulumiwa hapo ofisini kwenu?

Hivi wanaotoa sifa kwa chama hiki humu wanaona haya? Au mna mawazo ya kupiga kura mwaka 2015 na kushinda chini ya hao hao mnaowapa dhamana ya kubadili katiba (impossible within three years)!! Unrealistic!) kwa cizazi vingi jijavyo? Na aliyewaambia Katiba itafanikiwa kabla ya 2015 ni nani? Waizir wenu wa katiba ni nani? Anajua nchi zingine imechukua miaka mingapi?

Hivi lile wazo la kuwa piganieni kwanza tume ya uchaguzi nani aliliua? Au hamkunisikia japo kidunyu kuwa , if you are serious then sticky on changing election committee…tunataka tume yenye kila aina ya watu na inayosimamiwa na chombo huru!

Aliyewaroga kubadili katiba yote ni nani? 2015 ka...kuwa..waambieni wananchi CHADEMA itatoa mwanya wa CCM iendelee ili imalize mchakato wa katiba, by that time Mbowe atakuwa Tajiri kama Rostam!! Acha niseme! Maana kuna watu mnatoka povu kuitetea chadema ambayo lina wajanja fulani wanaotafuta pesa kwa nguvu zote…
Mbowe huyu na Kikwete watoto wa Night Club ambao wamewaingiza mkenge akina Slaa na akina Warioba, huku mkitoa statement kuwa Zito ndio eti aliyefanikisha mazungumzo!

Mkasema na kuanika uongo huu kwa watu ni dhambi!!
Chadema haina nguvu, kwani bado inajitafuna kashata na kucheua kahawa ya ikulu! Haina nguvu kwa aibu, kwani imepoteza nuru hii na utukufu huu! Chadema hii leo inagopa kusu-pport maandamano eti Mtaambiwa chama cha vurugu!

Chadema wanaogopa kumuua Nyani, wameishamwangalia usoni! Na kucheka naye? Na waumini wao wanawachekea na kujipa matumaini hewa kwa sababu hamna matumaini mengine…hawataki kuwaambiwa ukweli viongozi wao, eti wakisema ukweli watawaudhi na kuonekana wasaliti
Kama ambavyo chadema inavyoogopa maandamano na migomo leo hii kwani itamuudhi ‘mwenyeji wao’ kikwete ndivyo ambavyo chadema supporters wanaogopa kukosoa uongozi wao kwani watawaudhi eti wameonyesha mafanikio ya kuleta wabunge wengi sana-23!Au ni hivi….wakiandamana nani yuko tayari kwenda Jela?

Hivi uongozi wa chadema leo hii ukaenda jela,mnajua athari zinazotokea kwa familia chache sana zinazokiunda chama hiki, Fikiria chama ambacho viongozi ni mtu, mkwe, shemeji, mpwa, mama, mtoto, mjomba, shangazi na girlfriends….halafu wakakamatwa na kuwekwa ndani!! Chama kinakufa….

Watanzania this is just a reminder, you have to put your trust kwenye realistic! Hakuna ukombozi kwenye ballot box…..ILA nchi ingetikisika kwa migomo mingi iliyoasisiwa na chama hiki mnachokiabudu, basi leo Chadema kingeishi kama next ruling party! Sio kwa hali ya sasa ambayo wako kama hawako, huku madakatri wakirudi na na kureport makazini huku hawafanyi lolote…wamekosa support, wamekosa nguvu ya wale waliotegemewa kuwa suppport, Wale waliosema wanaweza!

Kesho mtataka madaktari wawa support kwenye maandamano yenu yalee! Never! Madaktari hawatakuwepo! Funny! Siasa inalipa jamani,kwani wachungaji wangapi wanasema wanaponyesha na kumbe sio? Au lawyers wangapi wanasema utashinda kesi hali akijua utashindwa? Kwa nini chadema isiseme wazi kuwa ni NGO na kijiwe cha jobless na opportunist ili tutafute tumaini lingine?

Kwa sisi wenye akili ‘’najisifu ngaa kidogo’’ kwa nini tusisifie CCM kwa siasa zake za kuharibu nguvu na bongo ya wapinzani kwa utashi wa wapinzani wenyewe? Whoever said CCM is a group of idiot and moron was wrong, Is a group of smart people who are brilliant and can play with people’s mind for their own benefit! Yes chadema has been played and they are now like ‘candle in the wind’

Mbowe and Kikwete at their best!
Waberoya umejaribu lakini ujue kuwa unaongelea watu walio makini si watu kukurupuka bila malengo au shabaha!!! Tuliza boli the storm is not yet over!!!!!!!!!

 
CHADEMA ujumbe kuu humu iko very clear:

... CCM hii si ya siasa za KUKAA MEZANI KUONGEA - Waberoya somo imeeleweka mkuu!!Hata mimi sikukubaliana na rafiki yangu Zitto kwa pendekezo lake hili (japo ni lenye nia njema) kwa kuwa naelewa fika hata siku moja CCM hawatokaa waelewe lugha hii.

CDM, status coante tafadhali; mambo mchaka mchaka!
 
Very impressing na ngumu kidogo flow nzuri content ila mi nadhani lile swala la uumini kuwa muumini wa siasa zote ila si hizo za huyo jamaa yetu wa Arusha ni shiiiiiiiiida Meku!
 
Hapa natakiwa kufikiria vizuri, ukizingatia kuna kauli katoa ZITTO huko bungeni juu ya posho imeniacha
naweweseka. I will be back Wabe, lazima kuna point hapa
 
Mkuu, umeandika mambo mengi sana ya kukilalamikia CHADEMA na viongozi wake.

Mkuu, wewe si ni m-Tz? Kwa nini usianzishe chama chako na kuyatekeleza hayo unayoyalalamikia badala ya kuwataka CHADEMA wakufanyie badala yako?

Wewe una akili kama ulivyojisifia mwenyewe, tumia basi hizo akili zako kuyafanya hayo ambayo CHADEMA wameshindwa.
Nadhani ungekuwa enzi zile za Mwl. Nyerere usingekubaliana naye kuusaka uhuru wa Tanganyika kwa mazungumzo. Ungetaka kuingia msituni na mtutu wa bunduki ili kumtoa mkoloni wakati uwezekano wa mazungumzo ulikuwepo.

unapomlalamikia Kikwete unatakiwa ujute kwa nini nawe si rais!! unamlalamikia baba ni kosa kwani kwa nini wewe haukuwa baba? tunapoilaumu CCM ni kwa nini hatukuwa CCM wengine? au wasilotenda kwa nini tusitende sisi!!!
 
Weborya,

Nimesikitishwa na lugha uliyotumia isiyo ya kistaarabu.Lakini naomba niweke wazi na wanaJF wasikie kwamba wewe umepotosha mada yako nzima kwa lengo moja tu.Unampiga vita mwenyekiti wa CDM Freeman Mbowe.Ni majuzi tu kuna watu walileta hoja hapa kwamba Mbowe hatakiwi kupata credit yoyote kwenye mazungumzo ya Ikulu kwa sababu hakushirikishwa.Leo wewe unasema ni mpango wake.Mkuu acheni hizo!!

Unajaribu kuleta kila aina ya fitna ili ionekane Mbowe ameshindwa uongozi kwa sababu unajua uchaguzi mkuu wa CDM umekaribia.Lakini nikuhakikishie kwamba wanachama wa CDM wako imara sasa hivi kuliko wakati mwingine wowote na hawatafanya makosa katika uchaguzi ndani ya chama.

Unapiga vita mazungumzo ya CDM na rais kuhusu mjadala wa katiba.Sasa ulitaka CDM waanzishe vita? Halafu wewe ndiye ungekuwa mtu wa kwanza kukimbilia hapa JF kuilaani.

Niwaombe viongozi wa CDM wawe makini na watu aina ya Weborya ambao kwa sasa wanapanga kila hila kuivuruga CDM mbele ya jamii.Aina hii ya watu ndiyo jua likiwaka wanalaani na mvua ikinyesha wanalaani.Ni watu wa ajabu na hovyo kabisa.

Weborya nikushauri tu.Tafuta kazi ya kufanya.Mambo ya kuja JF na kupiga fitna na majungu CDM hayatakusaidia,sanasana utazidi kujidhalilisha.Na ndio maana kwenye thread kama hii utashabikiwa sana na wale maadui wa CDM walioko JF.

Nakuapia kamwe hutafanikiwa katika fitna zako hizi.

Na tusubiri tuone!!

kijana nimekupita miaka minne nimeona mengi, kati ya hayo ni kuwa Mbowe na Kikwete ni marafiki, kwani nani asiyejua?

mengine yote hujajibu hoja!
 
Waberoya this is 2012, bado tu umekomaa na CDM ulishashauriwa huko nyuma "leave them alone"

Mbona niliufuata ule ushauri wenu? nikarudisha kadi yenu kwa bajaj! naandika kwa uchungu kwani ni wajasiriamali wazuri na hasa kuwadanganya watu ''Leave Tanzanians alone''

 
Mkuu kufanya jambo kwa wananchi wa tanzania yahitaji maandalizi ya kutosha kutokana na ukweli kwamba wengi ni waoga, hawajui haki zao na ndiyo kinachotusumbua mimi na wewe kuzidi kupoteza muda ndani ya mitandao bila kujua kuwa sisi tayari tulishajinasua na hiyo hivyo watu wengine ilibidi tuwapelekee ujumbe na kuwaelimisha.

Naweza kukueleza tu kuwa siyo lazima CDM wapige kengele ndiyo tuwaunge mkono, hata zile alama/ishara/viashiria vya vitendo vinaibuka nchini bado havituamshi? Ndiyo maana nasema, viongozi wa CDM wako smart, kwani wanajaribu kila njia kuhakikisha "The game is over hata kwa nock-out kabla ya 2015" lakini bado inaonekana wabongo wengi wako slow kufanya maamuzi magumu kama serikali yao ya magamba.

You have tried!!
 
Wabe,

Maneno mazuri sana ila ni kwenye theory tu. Inavyokuja kwenye Practical, vyama vya Siasa au wapigania uhuru/haki inabidi wawe wamegawanyika katika sehemu mbili. Upande mmoja unaongea mezani na upande wa pili unapigana msituni.

Ungelilaumu Chadema kwa kutokuwa na wapiganaji wa msituni . Chadema kama chama cha siasa, kazi yao inatakiwa kuwa mezani na kuongea. Kuwa Ikulu na kuongea. Kuwa bungeni na kuongea.

Kwa hali tuliyonayo Tanzania, neno WAPIGANAJI WA MSITUNI sina maana watu wachukue silaha na kuingia kweli msituni kama mtani wangu kutoka Dodoma alivyosema. Chadema kama wapinzani, wanaweza kuwa wapo nyuma ya migomo mikubwa Tanzania ingawa officially hawakiri hata sehemu moja kuwa wana uhusiano wowote na migomo.

Kama Mandela angelichukua Silaha na kwenda kupigana moja kwa moja, walimlima risasi na mchezo ukaisha. Vijana wake waligawanyika huku wengine wakifanya siasa na kuishi Mazimbwe na wengine wakisomea vita na kuishi Kongwa. Msumbiji, Zimbabwe, Angola nk nako ilikuwa hivyohivyo. Wakati kulikuwa na ANC, upande mwingine kulikuwa na wale Wauwaji wa Umkhonto we sizwe au Spear of the National na kweli wameuwa sana watu weupe South Africa wakati wa ubaguzi wa rangi.

Chadema kama chama wakijipeleka mbelembele kichwakichwa kama unavyotaka wewe, wanazushiwa Vangi la kutaka kupindua nchi na hapo mechi inakuwa imekwisha. Hiyo ingelifaa tu kama nchi ingelikuwa INATAWALIWA NA NCHI/WATU WENGINE. Kwa mfano tuseme South Africa inatawala Tanzania na watu wanataka kugoma, hapo sasa Chadema wanajiingiza moja kwa moja kwani hawa jamaa wakiondoka, basi itabidi chama kingine kitawale.

Unaweza kuwa sawa kwa upande mmoja wa shilingi ila kumbuka shilingi ina pande tatu/ au zaidi? Kinachotakiwa kwa sasa ni sisi wananchi kwenda kuwasaidia Waganga katika mgomo wao na ikibidi Waalimu na taasisi nyingine ziungane kugoma na kupinga nyongeza za posho, kupanda kwa bei na maisha kwa ujumla. Chadema wawepo ila kwa siri sana.

ukubwa dawa,

kuna tofauti sana ya JF-GT na JF-Kata,

Big up, the 'thing' here ni kujadili, na umefanya hivyo

malizia basi na hoja zangu zingine ili nikupate vizuri
 
Mkuu Yaya, nimjuavyo Ndg Waberoya kwa miaka hii yote huwa si mtu wa kumuingiza kwenye nembo ya 'KUKILALAMIKI' CHADEMA.

Hoja zilizoainishwa kwenye taarifa yke zinasimama na kujitegemea kabisa sawa na hoja zake Ngunguli Mwanakijiji hata bila kuhitajika yeye kuyakazia zaidi.

Na kwa kuwa CHADEMA siku zote ni wasikivu na wafuatiliaji wa mambo kwa umakini wake, soon we gonna see a review of TACTICS as the superordinate goal ans set of strategies remain as vibrnt as ever.

Katika hili naweka shilingi yangu ya mwisho kati yangu na umasikini wa kutupwa - ondoa wasiwasi katika hilo mkuu!!
 
kijana nimekupita miaka minne nimeona mengi, kati ya hayo ni kuwa Mbowe na Kikwete ni marafiki, kwani nani asiyejua?

mengine yote hujajibu hoja!

Kwa hiyo wakiwa marafiki wewe inakuuma nini? Na wakiwa maadui unafaidi nini? Wewe hujui kazi ya shetani wa kuzimu ni kufitinisha watu?
 
Mbona niliufuata ule ushauri wenu? nikarudisha kadi yenu kwa bajaj! naandika kwa uchungu kwani ni wajasiriamali wazuri na hasa kuwadanganya watu ''Leave Tanzanians alone''


Ushauri wenu na kadi yenu na nani???????? Tatizo unafikiri CHADEMA to be right, they have to do what you, urself think is right. It's not about Tanzanians it's just u and u and u. Get over it and move on broda!!!!!
 
Back
Top Bottom