Elections 2010 CHADEMA wamekumbwa na pepo gani?

Shelute Mamu

Member
Mar 17, 2009
37
1
Jamani imenishangaza sana kuona kwamba Chama chenye nguvu, wasomi, sera nzuri leo wanaingia kwenye mtego wa CCM. Wameanza kwa kumtumia Mfadhili wa CCM kupewa fedha za msaada, Chadema wakachekelea, CCM wanawatia moyo kusema si dhambi mfadhili wao kufadhili na vyama vingine!! jana inatangazwa kwamba CCJ imevunjwa na wanaungana na Chadema, Kiongozi wa Chadema wanasema wanafurahia na kusema aliyeingia zamani na anayeingia leo wote ni sawa!!! Hivi Chadema hawalioni hili kwamba CCJ ni mamluki ambao wanakwenda kuimaliza Chadema jamani.

Kumbuka jinsi NCCR kilivyovuma sana na Mrema akiwa mstari wa mbele, alipofanikiwa kukisambaratisha akahamia kwingine. Hamuoni hili kwamba hawa wanatumiwa kuja kudhoofisha Chama? Tafadhali viongozi msije mkawaumiza wanachama wenu waaminifu ambao wamewaamini MNO. Ukiambiwa kitu changanya na akili zako.
 
CCJ wataimalizaje CHADEMA?
 
Katika hao wote walioingia hakuna mwenye ubavu wa kuiyumbisha chadema wote ni minors na wala hawatapewa uongozi wowote ndani ya chama makini chadema, kule nccr mageuzi kilichotokea ni kuwa walipokuja akina mrema viongozi wakajitoa na kuwaacha wageni mamluki waendeshe chama na matatizo yakajitokeza kama ulivyoona, chadema ni imara na viongozi makini wanafanya kila jambo kwa tahadhari.
 
wewe utakuwa umetumwa na CCM yaani tokea ujiunge March 2009 hii ndo POST yako ya kwanza, hebu twambie hizo pepo zilizowakumba chadema au ndo makamba anavyokwambia
 
Si tatizo kwa wanachama wapya kuingia CHADEMA hata kama wanatoka vyama vingine kwa kuwa hata wanachama wengi na hata viongozi wake walitoka CCM. Tatizo ni pale wanapopewa nafasi za uongozi bila kupitia taratibu za chama (CHADEMA) kama walivyofanya NCCR that time.
Kwa maoni yangu binafsi Mpendazoe sio kiongozi makini lakini hii haimaanishi kuwa hawezi kuwa na mchango mzuri ndani ya chama, kwani kujitoa kwake CCM hakukuwa strategic kisiasa na nionavyo mimi lengo lake ni kupata ubunge tu. Lakini haya ni mawazo yangu tu....
 
Mfalme wa Wafalme suala siyo mtu anapochangia basi ametumwa, mimi huo ni mtazamo wangu, na mtazamo wangu basi isiwe kuwa mtu ametumwa, eleza kama alivyoeleza PhD siyo lawama mheshimiwa ! hapa ni mahali pa kuelimishana siyo mahali pa kutafuta mchawi MFALME.
 
Mkuu kwa jinsi ulivyotoa mada yako haijajitoshereza kwani mtu kujiunga chadema sio kuwa na pepo, mwanachama yeyote anarusiwa kujiunga CHADEMA awe CCM, cuf etc
 
Hizi si taarifa za kupuuza hata kidogo. Mapaka leo sijajua nini kilitokea mpaka viongozi hawa wakashindwa kukamilisha uhakiki wa wanachama wao. Japo lawama zilikuwa kwa Msajili. Sasa wanachama wao wamewaambiaje, au wamewaacha watafute chama cha kujiunga?
Lisemwalo lipo kama halipo ..................
Hivi? hata kama ni Makamba katuma thread hii basi kuna jambo!:humble:
 
hoja rojorojo, kutoka kwa watu wa hovyo hovyo.
kamuulize Sabodo kwanini hakupeleka pesa yake TLP akaileta CHADEMA,
MBONA ccm Ilimpokea Warid Kabouru na kina Lamwai, iweje kosa kwa CCJ kuamia CHADEMA ?
Chadema wanakua wanachama wakawaida tu, wanaingia kwenye mchakato kama wanachama wengine, kwa taarifa yako , kuna wabunge kama 40 wa CCM wako mbioni kujiunga CHADEMA
 
Ndoto za Alinacha hizo! sisiemu hailingani na wengineo. Mto ni kawaida kuingia Baharini. Bahari ikiingia mtoni ni maafa
 
Waacheni wakubatie shuka wanaloona linawakinga mbu na baridi kumbe ki ukweli ni kaniki lililochoka linaloambukiza mafua. CHADEMA mwendo mdundo sauti za kina Makamba na wajukuu zake hazitatunyima usingizi bali zinatuongezea ari ya kutimiza kazi yetu ya kuwakomboa watanzania. Dalili ya siku njema huanzia asubuhi - tayari makada wao wameanza kumwaga support kwa CHADEMA, tayari wanasiasa wakongwe wanajiunga kuongeza nguvu ya ukombozi, ni werevu hao wameshasoma alama za nyakati.

Watanzania mnaoendela kuuchapa usingizi ndani ya sisiemu mkidhani bado ni usiku huku mmejifunika kaniki lenye vumbi na matobo, AMKENI kumekucha - tupeni kaniki mlilojifunika njooni huku mwenye Nuru ya kweli - CHADEMA ndiyo jibu la matatizo yetu.

Nimechoka kila siku kusikia malalamiko yenu, wakati nchi yenu ina kila aina na rasilimali - Kateni shauri sasa.
 
hoja rojorojo, kutoka kwa watu wa hovyo hovyo.
kamuulize Sabodo kwanini hakupeleka pesa yake TLP akaileta CHADEMA,
MBONA ccm Ilimpokea Warid Kabouru na kina Lamwai, iweje kosa kwa CCJ kuamia CHADEMA ?
Chadema wanakua wanachama wakawaida tu, wanaingia kwenye mchakato kama wanachama wengine, kwa taarifa yako , kuna wabunge kama 40 wa CCM wako mbioni kujiunga CHADEMA

Itakua Habari njema sana......
 
ili chama kikue kinahitaji wanachama na wanachama wanachama hao either watatoka chamakingine au wasio n chama chochote hivyo nitawashangaa mnaoona ajabu wanachama wa ccj kuhamia chadema
 
Jamani imenishangaza sana kuona kwamba Chama chenye nguvu, wasomi, sera nzuri leo wanaingia kwenye mtego wa CCM. Wameanza kwa kumtumia Mfadhili wa CCM kupewa fedha za msaada, Chadema wakachekelea, CCM wanawatia moyo kusema si dhambi mfadhili wao kufadhili na vyama vingine!! jana inatangazwa kwamba CCJ imevunjwa na wanaungana na Chadema, Kiongozi wa Chadema wanasema wanafurahia na kusema aliyeingia zamani na anayeingia leo wote ni sawa!!! Hivi Chadema hawalioni hili kwamba CCJ ni mamluki ambao wanakwenda kuimaliza Chadema jamani.

Kumbuka jinsi NCCR kilivyovuma sana na Mrema akiwa mstari wa mbele, alipofanikiwa kukisambaratisha akahamia kwingine. Hamuoni hili kwamba hawa wanatumiwa kuja kudhoofisha Chama? Tafadhali viongozi msije mkawaumiza wanachama wenu waaminifu ambao wamewaamini MNO. Ukiambiwa kitu changanya na akili zako.

Hata quotes unatumia za kulekule.....
 
Back
Top Bottom