CHADEMA wadai CCM kuwahujumu

Sumasuma

JF-Expert Member
Jun 23, 2011
342
110
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimelaani vifendo vya fujo vilivyodaiwa kufanywa na wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Februari 7, mwaka huu wakati wakirudi kutoka kwenye mikutano yao ya kampeni katika Shehia ya Mgeni Haji.

Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Zanzibar, Bw. Hamad Mussa Yussuf aliyasema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo Zanzibar.

Alisema, wapo baadhi ya wanachama wa chama cha mapinduzi ambao wamekuwa wakifanya fujo dhidi ya chama hicho wakati wakurudi kwenye mikutano ya kampeni.

Alisema, tukio hilo limetokea wakiwa wanarudi kwenye kampeni ndipo msafara wa gari lao liliposhambuliwa kwa mawe na kupasuliwa kioo cha mbele katika gari lao la matangazo pamoja na kuwatolea matusi viongozi wao wa tawi la Kiboje Manzese.

"Vitendo hivi vinafanywa kwa makusudi na wafuasi wa vyama vya upinzani kwa maelekezo ya viongozi wao na vina lengo la kuleta vurugu na fujo katika uchaguzi wa Jimbo hili la Uzini,"alisema

Alisema, hawataweza kuvumilia vitendo vyovyote vya 'kihuni' na fujo vitavyoendelea kufanywa na vyama vyovyote vya kisiasa dhidi yao.

Bw.Hamad alisema, taarifa za matukio yote hayo tayari wameyaripoti kwenye vyombo husika pamoja na kwa msimamizi wa uchaguzi jimboni humo katika Wilaya ya Kati na kwa Kamanda wa polisi.

Alisema, wanatarajia hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya wahusika pamoja na viongozi wao wote, hata hivyo alidai pindi madai yao hayo yatapopuuzwa na kutochukuliwa hatua yoyote hawataweza kuvumilia.

"Tuna imani na Tume ya Uchaguzi pamoja na Jeshi la Polisi, lakini wataposhindwa kuwachukulia hatua inayofaa kwa haya hatuwezi kukaa kimya," alidai.

Hata hivyo alitoa mwito kwa wanachama wao wawe watulivu katika kipindi hiki cha kampeni ili siku ya uchaguzi waweze kushiriki kuchagua Mwakilishi wanayemtaka bila vitisho na fujo ya aina yoyote.:A S 465:
 
kwakuwa wewe si mgeni wa siasa za tanzania na hasa katika chaguzi ndogo,hilo halipaswi kukushangaza
 
Kila chenye mwanzo hakikosi kuwa na mwisho!! Mwisho wa kuwadhulumu wananchi haki yao ya kupata viongozi wanaowataka umefika, cha mhimu ni kutambua hilo na kuchukua hatua.
 
Kawaida ya ccm, ukiona hivyo kuna mazuri yanayofanwa na CDM na wanafanya kila mbinu kuwachafulia waonekane hawafai.
 
Mawe mnajipiga wenyewe Chadema halafu asubuhi mnawahi habari maelezo! Dr Slaa acha siasa zako za kishamba
 
Mawe mnajipiga wenyewe Chadema halafu asubuhi mnawahi habari maelezo! Dr Slaa acha siasa zako za kishamba

Mkuu cdm ni tofauti na ccm waliojichomea nyumba zao igunga na kujimwagia tindikali kisha kuwapakazia cdm, ingekuwa cdm wametenda kosa hilo wangeshakamatwa wahusika lakini ikiwa wahalifu ni kutoka ccm polisi wanapata kigugumimizi wakijifanya hawawajui hasa wanapokuwa viongozi waandamizi wa chama hata wanapokutwa na silaha waliyotumia, hayo tuliyashudia huku kwetu Igunga.
 
Mawe mnajipiga wenyewe Chadema halafu asubuhi mnawahi habari maelezo! Dr Slaa acha siasa zako za kishamba
wala hufai kuwa mlengo wa kati,kwenye hiyo post umeona jina la Slaa?utakufa na presha bure juu ya dk slaa lakini ujue ndo rais wako huyo 2015
 
Kila chenye mwanzo hakikosi kuwa na mwisho!! Mwisho wa kuwadhulumu wananchi haki yao ya kupata viongozi wanaowataka umefika, cha mhimu ni kutambua hilo na kuchukua hatua.

Kweli kabisa na hata uchaguzi umekwisha.

Tambo za Chadema zimeishia kupata chini ya 5%.

Je inawezekana mtu kudhulumiwa gani na kuangukia 5%.

nafikiri Chadema walihitaji kusoma alama za nyakati kama walivyofanya wenzao wa CUF.

Sijui Ritz huko Tanzania atakwenda uchi kutoka Posta mpaka Bunyokwa?

 
Back
Top Bottom