Chadema waandaa bajeti kuikabili CCM

Luteni

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
2,274
302
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimemrejeshea cheo cha Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Zitto Kabwe, na kupanga mikakati ya kukabili CCM katika mikoa yote nchini.

Uamuzi huo ulifikiwa jana na Kamati Kuu ya Chadema, kwenye mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam ambapo walipanga bajeti ya kufanikisha mipango yao ya kujiimarisha mikoani.


Zitto alinyang'anywa cheo hicho Novemba mwaka jana kwa kile kilichoelezwa ni kwenda kinyume na uamuzi wa chama.


Habari kutoka ndani ya kikao hicho zilieleza kwamba uamuzi huo ulifikiwa baada ya mjadala mzito.


Baadhi ya wajumbe walimlaumu Zitto kwamba msimamo wake wa kutangaza hadharani kupitia vyombo vya habari kuwa hakubaliani na uamuzi wa chama kususia hotuba ya Rais Jakaya Kikwete, ulisababisha kukigawa chama.


My take:
Hongera NEC-Chadema kwa kutoa maamuzi ya busara na kufikia mwafaka juu ya jambo hili naamini vikao vyenu vilitawaliwa na kuongozwa na vichwa vyenye hekima na busara kubwa mmeonyesha ukomavu wa kisiasa.

Kinachotakiwa sasa muweke pembeni tofauti zenu na muanze kufanyakazi mliyotumwa na wananchi kumbukeni muda siku zote huwa hautoshi.
 
Naona ni haraka sana kufanya haya maamuzi ila tunajua Chadema wapo makini sana na wataendelea kumchunguza Zitto mpaka wawe na imani nae.

Tunaamini ni uamuzi wameuona ni mzuri na kuna sababu ambazo Zitto kajieleza kuonyesha "anaomba msamaha" kwa yote mabaya aliyoyaleta ndani ya chama kipindi hiki chote. Tunamtakia Zitto mema na akae akijua "Issue za Taifa ndio Priority Kubwa ya Chadema" Sisi kama wananchi tuendelee kumulika viongozi wengine wa Upinzani endapo wakawa wanatumiwa na CCM kuturudisha nyuma.

"This is a time move forward with mapinduzi hakuna kusimama tena na kuwapa muda CCM kuimaliza Tanzania"
 
huyu kijana mwenzetu naye umaarufu unamlemea. by the way hongera zao kwa kumaliza tofauti zao wasiwasi wangu isiwe kuwa zimeahirishwa tu
 
Hongereni NEC ya CDM. Mmeonyesha ukomavu wa kisiasa na hekima katika kushughulikia masuala magumu ya chama. Kutoa fursa nyingine kwa Zitto kukalia hicho kiti, ni uamuzi mzuri kwani hii imedhihirisha kuwa chama hakiendeshwi kwa visa au kukomoana, kama wanavyofanya wenzenu wa ccm.

Ushauri wangu kwa Zitto:
Kuanzia sasa jitahidi uishi kama mwanachama na kiongozi wa CDM na siyo mpenzi wa CDM. Kutoa tamko hadharani linalopingana na msimamo wa chama uliofikiwa ndani ya kikao halali ambacho hata wewe ulihudhuria, kunaleta mgawanyo na vurugu katika chama. Jambo lolote hata kama wakati wa majadiliano ulikuwa upande unaopinga, once likifikia ukingoni na kuhitimishwa kinyume na msimamo wako, kwa uwingi wa kura, basi huo ndio msimamo wa chama ambao siyo tu unatakiwa kuunga mkono bali kama kiongozi unatakiwa kwenda mbele zaidi kwa kuueneza kwa wanachama na wapenzi wa chama chako. Kwa staili hiyo, mtasonga mbele kama chama na kufikia malengo yenu kirahisi kwa faida ya chama na nchi, kwa ujumla.

Ushauri wangu kwa chama; CDM:
Chama kiendeshwe kupitia vikao halali. Wakati wa vikao, fursa itolewe ya kila mjumbe kuchangia au kutoa dukuduku lake kwa uhuru usiokuwa na mashaka. Ninachotaka kusema ni kwamba M/Kiti na Katibu wa vikao wasiingie kwenye vikao wakiwa tayari na wana majibu au msimamo kuhusu masuala yatakayojadiliwa na wajumbe wa kikao watambue na waridhike kuhusu mwenendo huo. Kusiwe na hali ya kutiliana shaka miongoni mwa wajumbe wa vikao. Vikao ndivyo viwe uwanja mpana wa wajumbe kumwaga yote yaliyomo mioyoni mwao, kwa uhuru. Staili hii wataalam wa pyschology wanaiita 'kutema nyongo'. Kwa hiyo, wajumbe wa vikao wapewe fursa ya kutema nyongo. Hii itasaidia sana kujenga umoja ndani ya chama kwani kila mjumbe atajisikia kuwa ana fursa sawa na mjumbe mwingine katika kufikia maamuzi ambayo utekelezaji wake ndiyo unaoendesha chama. Wenzenu wa ccm wametia kapuni utaratibu huu na matokeo yake ndiyo hayo tunayoyaona ndani ya chama na hata kwenye serikali yake. Kila mtu anaongea msimamo wake hadharani. Chama kinaishi kama genge la wahuni tu.

Kwa maslahi ya CDM, ninawiwa kusema ukweli hapa jamvini kuwa mimi nimekuwa mwanachama wa ccm kwa muda mrefu. Natambua umuhimu wa haya ninayoongea kwenye mustakabali wa chama na nimeshuhudia kwa macho yangu mwenyewe. Nisingependa CDM iingie kwenye mkumbo huo. ccm inakufa kifo cha asili kwa sababu ya kubeza michango ya wanachama wake katika kuendesha chama. Uhuru au fursa zinazotolewa na chama kwa wanachama na viongozi wake havitakiwi kutiliwa shaka na wanachama na viongozi husika. Kwa kuwa CDM ndicho chama mbadala kinachoonekana kufaa kwa watanzania kwa sasa, lazima tukosoe kwa nguvu zetu zote tunapoona makosa ya uendeshaji wake.

Mungu ibariki Tanzania,
Mungu ibariki Afrika.
 
Du Zitto kichwa sasa mambo yataenda vizuri, kwani alikuwa anawakilisha wengi, na mipango yake ni kuona mbali Hongereni Kamati kuu ya CDM kwa kumrudisha ulingoni.
 
fanya kazi zito,story story kuhusu urafiki wako na mkwere na akina zola, weka kapuni. Nakutakia kazi njema pia niwajibu wako kutushawishi ili turudishe iman yetu kwako.
 
Leon Bahati na Claud Mshana

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimemrejeshea cheo cha Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Zitto Kabwe, na kupanga mikakati ya kukabili CCM katika mikoa yote nchini.

Uamuzi huo ulifikiwa jana na Kamati Kuu ya Chadema, kwenye mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam ambapo walipanga bajeti ya kufanikisha mipango yao ya kujiimarisha mikoani.

Zitto alinyang'anywa cheo hicho Novemba mwaka jana kwa kile kilichoelezwa ni kwenda kinyume na uamuzi wa chama.

Habari kutoka ndani ya kikao hicho zilieleza kwamba uamuzi huo ulifikiwa baada ya mjadala mzito.

Baadhi ya wajumbe walimlaumu Zitto kwamba msimamo wake wa kutangaza hadharani kupitia vyombo vya habari hakubaliani na uamuzi wa chama kususia hotuba ya Rais Jakaya Kikwete, umesababisha kukigawa chama.

Zitto alinyang'anywa cheo hicho kutokana na msimamo wake wa kutounga mkono uamuzi uliopitishwa na wabunge wa chama hicho wa kususia hotuba ya Rais Jakaya Kikwete kwa kutoka nje ya Bunge.

Zitto na wabunge wengine hakuingia bungeni siku hiyo na aliweka msimamo wake waziwazi kwenye vyombo vya habari kwamba ingawa chama kimekubaliana hivyo, yeye binafsi haungi mkono.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, Zitto pamoja na kurejeshewa cheo hicho, alionywa kwa maelezo kwamba hakupaswa kutangaza msimamo wake hadharani.

Chanzo hicho kilieleza kwamba wajumbe walimuonya wakisema angeweza kukaa kimya na kubakia na msimamo wake na hali hiyo isingekiaibisha chama.

Jambo jingine lililozungumza katika kikao hicho ni mgawanyiko ndani ya chama ambao umesababisha kukosa baadhi ya majimbo kwenye uchaguzi uliopita.

Walisema mgawanyiko ndani ya chama hicho ulisababisha wakose majimbo mengi mkoani Kigoma wakati walikuwa na nguvu kubwa ya kisiasa.

Majimbo matano ambayo chama hicho ilikuwa iyachukue, walisema yalinyakuliwa na NCCR-Mageuzi na wao kuambulia moja tu.

Walitoa mfano kwa jimbo Kigoma Kusini ambalo kama sio kumumfukuza ndani ya chama, David Kafulila, wangeweza kulinyakua.

Kafulila ambaye alionyesha kuwa na ushawishi mkubwa kwenye jimbo hilo baada ya kufukuzwa Chadema alihamia NCCR na kushinda kiti hicho.

Awali katika kikao hicho, ambacho kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Habari wa Chadema, Erasto Tumbo,kitajadili masuala mbalimbali yanayohusu chama hicho, ikiwa ni pamoja na kujadili agenda zilizojadiliwa katika kikao kilichotangulia.

Tumbo alisema jijini Dar es Salaam jana kuwa, agenda kubwa ya kikao hicho, ambacho alisema watatoa tamko baada ya kumalizika, kitajadili mpango mkakati wa Chadema kwa mwaka 2011.

Katika kikao cha Kamati Kuu kilichofanyika Septemba, 2010, suala la uteuzi wa nafasi za viti maalum kwa wabunge wa chama hicho ambalo lilizua malalamiko ya kuwepo kwa upendeleo, hatua iliyofanya viongozi waandamizi wa chama hicho kwa nyakati tofauti kulitolea ufafanuzi suala hilo.

Kwa mujibu wa taarifa ya vigezo hivyo vya uteuzi wa wabunge iliyotolewa na Dk Kitila Mkumbo, ambaye alikuwa mwenyekiti wa uteuzi huo, mgombea yeyote ambaye aliwahi kushika wadhifa wa ubunge aliwekewa alama 10 ambacho ni kigezo kimojawapo kati ya sita.

Dk Mkumbo aliongeza kuwa kigezo kingine kilichotumika ni cha uzoefu wa uongozi nje ya siasa, ambacho nacho alifafanua kuwa kilikuwa kimegawanywa katika madaraja mbalimbali.

Kwa Mujibu wa Dk Mkumbo, njia hizo zilitumika ili kuondoa malalamiko mbalimbali yaliyokuwepo, ikiwa ni pamoja na kuwepo kwa upendeleo wa watu wanaotoka Kanda ya Kaskazini.

Kamati kuu ya chama hicho ilikutana Septemba 25, 2010 kujadili suala hilo lakini haikuweza kufikia muafaka na hivyo kulazimika kuendelea na mkuatano huo Septemba 26.

Mkutano huo ulishindwa kumaliza ajenda zake baada ya makundi kuibuka juu ya njia ya kuwapata wabunge hao.

Makundi hayo yalidaiwa kuegemea vigogo wawili wazito ndani ya chama hicho, jambo ambalo liliipasua pia meza kuu na kuiweka katika mazingira magumu katika kuokoa jahazi.

Chama hicho hatimaye kilipitisha majina ya wabunge 105 wa viti maalum, huku kikiwaacha wanachama 42 walioshindwa kukidhi vigezo vilivyowekwa.


Majina hayo hayakuwekwa hadharani na badala yake yalipelekwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), ambapo baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 31 ambapo Chadema ilisimamisha wagombea wa majimbo 185, na kufanikiwa kutwaa majimbo 25, na kupata viti maalum 23.
 
Bajeti ya Chadema ili ieleweke kwa wapigakura iwe shirikishi kwa kwenda kuwauliza wapigakura majimboni wanataka bajeti ya namna gani............................isiwe ni bajeti ya matakwa ya wataalamu tu..........................kama bajeti za CCM ambazo kodi zake sasa zinatishia ukuaji wa uchumi kwa kuwa mzigo kwa wazalishaji wadogo wadogo......................................................
 
Weldone Chadema lakini kama ni kweli mtarajiwa mchumba wa Zitto ana undugu na Mkwere itabidi Chama kikae kiangalie upya nafasi hiyo
 
Cha muhimu ni mawazo ya hao kwenye mkutano/kikao ku converge na kufikia consesus! kila la kheri
 
Weldone Chadema lakini kama ni kweli mtarajiwa mchumba wa Zitto ana undugu na Mkwere itabidi Chama kikae kiangalie upya nafasi hiyo

sio mbaya...mkwere akimaliza muda wake 2015 tutamrudisha kundini
 
NEC-Chadema ... ulifikiwa jana na Kamati Kuu ya Chadema
Kamati Kuu ya CHADEMA ndio inaitwa NEC?

CHADEMA hawana Halmashauri Kuu kama CCM, tuache kuiga iga visivyoigika!
 
Weldone Chadema lakini kama ni kweli mtarajiwa mchumba wa Zitto ana undugu na Mkwere itabidi Chama kikae kiangalie upya nafasi hiyo

Acha umbea wewe, mbona Slaa mke wake alikuwa diwani ccm na yeye alikuwa katibu chadema na naibu kiongozi wa kambi ya upinzani kwenye bunge la 9?
 
nimefurahia sana uamuzi huu, kwani wale wapaka matope wa CHADEMA sasa mmewapunguza maneno. walizidi sana kuleta chokochoko mambo yasiyowahusu kwa lengo la kuvuruga chama
 
HONGERA CHADEMA! Ujumbe wangu ni kuwa, kwa maamuzi hayo, ni ushindi kwa Chama na sio mtu fulani. Ushauri wangu kwa Zitto ni kuwa, aache tabia ya kuongea sana na vyombo vya habari kwa kujibu hoja za ndani ya chama. Hiyo inampunguzia umaarufu kwa jamii na hata imani.

Hata kama anajua anajua yeye ni lulu kokote, bado suala la imani litaenda nae kokote. Ushauri wangu kwa Mbowe na huyo Zitto ni kuwa, ili CDM isonge mbele ilipoishia mwaka huu, wote wawili wakubali kumwachia Slaa kuwa mgombea tena 2015.

Kung'ang'ania kwenu kugombea ndio mtakigawa chama sababu nyote mmetawaliwa na jazba na mnaona ushindi wa mwingine itakuwa kama dhalilisho kwa mwingine. Pamoja na kwamba kugombea ni demokrasia kwa kila mtu, lakini kuna mazingira inabidi uamuzi tofauti ufanyike kunusuru mpasuko.

Kuhusu Zitto kwamba mtarajiwa wake ana undugu na mkuu wa got, eti ndio wakose imani nae, huo ni upuuzi sababu kama ndio hivyo basi wabunge wa vyama tofauti wasingekuwa marafiki, au watu waache kuoana sababu ya hisia za itikadi?. Wa-TZ Tuache kufika pale walipofikaga CCM na CUF visiwani kutohudhuria misibani au hata kuoana kwa hisia za itikadi tofauti. Lakini leo wako wapi?? Waliosita kuoa wanajuta kupoteza wachumba kwa itikadi tu!

Watu wanakula kuku pamoja ndani ya SMZ. So tofauti za itikadi kichama ziishie kwenye siasa tu sababu mwisho wa siku sisi wote ni ndugu ndani ya jamii.
 
HONGERA CHADEMA! Ujumbe wangu ni kuwa, kwa maamuzi hayo, ni ushindi kwa Chama na sio mtu fulani. Ushauri wangu kwa Zitto ni kuwa, aache tabia ya kuongea sana na vyombo vya habari kwa kujibu hoja za ndani ya chama. Hiyo inampunguzia umaarufu kwa jamii na hata imani. Hata kama anajua anajua yeye ni lulu kokote, bado suala la imani litaenda nae kokote.

Ushauri wangu kwa Mbowe na huyo Zitto ni kuwa, ili CDM isonge mbele ilipoishia mwaka huu, wote wawili wakubali kumwachia Slaa kuwa mgombea tena 2015. Kung'ang'ania kwenu kugombea ndio mtakigawa chama sababu nyote mmetawaliwa na jazba na mnaona ushindi wa mwingine itakuwa kama dhalilisho kwa mwingine. Pamoja na kwamba kugombea ni demokrasia kwa kila mtu, lakini kuna mazingira inabidi uamuzi tofauti ufanyike kunusuru mpasuko.

Kuhusu Zitto kwamba mtarajiwa wake ana undugu na mkuu wa got, eti ndio wakose imani nae, huo ni upuuzi sababu kama ndio hivyo basi wabunge wa vyama tofauti wasingekuwa marafiki, au watu waache kuoana sababu ya hisia za itikadi?. Wa-TZ Tuache kufika pale walipofikaga CCM na CUF visiwani kutohudhuria misibani au hata kuoana kwa hisia za itikadi tofauti. Lakini leo wako wapi??

Waliosita kuoa wanajuta kupoteza wachumba kwa itikadi tu! Watu wanakula kuku pamoja ndani ya SMZ. So tofauti za itikadi kichama ziishie kwenye siasa tu sababu mwisho wa siku sisi wote ni ndugu ndani ya jamii.
 
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimemrejeshea cheo cha Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Zitto Kabwe, na kupanga mikakati ya kukabili CCM katika mikoa yote nchini.

Uamuzi huo ulifikiwa jana na Kamati Kuu ya Chadema, kwenye mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam ambapo walipanga bajeti ya kufanikisha mipango yao ya kujiimarisha mikoani.


Zitto alinyang'anywa cheo hicho Novemba mwaka jana kwa kile kilichoelezwa ni kwenda kinyume na uamuzi wa chama.


Habari kutoka ndani ya kikao hicho zilieleza kwamba uamuzi huo ulifikiwa baada ya mjadala mzito.


Baadhi ya wajumbe walimlaumu Zitto kwamba msimamo wake wa kutangaza hadharani kupitia vyombo vya habari kuwa hakubaliani na uamuzi wa chama kususia hotuba ya Rais Jakaya Kikwete, ulisababisha kukigawa chama.


My take:
Hongera NEC-Chadema kwa kutoa maamuzi ya busara na kufikia mwafaka juu ya jambo hili naamini vikao vyenu vilitawaliwa na kuongozwa na vichwa vyenye hekima na busara kubwa mmeonyesha ukomavu wa kisiasa.

Kinachotakiwa sasa muweke pembeni tofauti zenu na muanze kufanyakazi mliyotumwa na wananchi kumbukeni muda siku zote huwa hautoshi.

Demokrasia Africa ni ngumu bora wengine tujikite kwenye maswala ya jamii
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom