Nyahende Thomas
JF-Expert Member
- Nov 5, 2010
- 211
- 104
Ndugu wanaJF.
Kwa niaba ya uongozi wa Chadema kata ya Ukonga ninapenda kutumia fursa hii kuwakaribisha katika mkutano wa hadahara utakaofanyika jumapili hii tarehe 04/08/2013 kuanzia majira ya saa 8:00 mchana katika mtaa wa mazizini Kata ya Ukonga Jimbo la Ukonga. Mkutano utafanyika katika uwanja uliopo karibu kabisa na ofisi ya mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa mazizini.
Mgeni wa heshima ambaye pia atakuwa msemaji mkuu wa mkutano huo atakuwa mwenyekiti wa Taifa wa Baraza la vijana Chadema kamanda John Heche Suguta, akiambatana na vijana machachari wa CHASO mkoa wa Dar es salaam.
Nawakaribisheni wote mtakaokuwa na nafasi siku hiyo hasa wakazi wa Ukonga, Segerea, Kitunda, Pugu, Gongolamboto, Majohe, Kivule, Banana na maeneo mengine ya jirani mnakaribishwa sana ili tupate kujumuika kwa pamoja kujadiliana juu ya masuala mbalimbali yanayohusu mustakabali wa kata yetu ya Ukonga, Jimbo la Uchaguzi la Ukonga, mkoa wetu wa Dar es salaam pamoja na masuala mengine yanayoihusu nchi yetu kwa ujumla.
CHADEMA NGUVU YA UMMA.