Jerry Slaa umetudharau sana wana Ukonga

Mzito Kabwela

JF-Expert Member
Nov 28, 2009
18,857
7,618
Katika makosa ambayo Chama Cha Mapinduzi chini ya aliyekuwa Mwenyekiti taifa mwaka 2020 iliyafanya ni kumpendekeza Jerry Slaa kuwa mbunge wa Ukonga.

CCM ilijipa Certificate ya kukataliwa moja kwa moja na wana Ukonga kwa kutuletea huyu mbunge mwenye dharau, kiburi, majivuno na asiyejua wala kushughulika na kero za wananchi wa ukonga.

Ni katika kipindi chake wakati alipokuwa Meya, alizuia na kutumia ushawishi wake ili barabara za Banana hadi Kivule kupitia Kitunda isiwekwe lami. Sasa hivi barabara hizi ni mbovu kuliko kawaida.

Ni katika kipindi chake kama Mbunge haoni umuhimu wa barabara ya kutoka Ukonga Mombasa hadi Mbondole kuwekwa lami na ukimuuliza anajibu kwa jeuri, Mtajijua! Eti kwa kuwa mwaka 2015 ukonga walichagua mpinzani basi anawakomesha ili wasirudie tena. Mbunge wa namna hii anafanya wananchi waichukie serikali bila sababu.

Ni katika kipindi chake kama Mbunge barabara ya kutoka Pugu mpaka Viwege haina lami na hakuna mpango wowote wa kuweka lami siku za karibuni.

Huyu huyu Jerry Slaa haishi kwenye jimbo la ukonga. Pamoja na kuwa makazi yake na muda wake mwingi anakuwa hapa Dar es Salaam lakini hakai kabisa kwenye jimbo la ukonga.

Huyu huyu Slaa hafanyi mikutano na wananchi. Ukiachilia mikutano ya hadhara aliyokuwa anafanya wakati anaomba kura mwaka 2020 hajafanya mkutano hata mmoja na wananchi angalau hata kama kwenye hizi barabara mbovu yeye hapitishi gari lake wala havuti hewa iliyojaa vumbi basi asikilize tu kero za wananchi, hajawahi na hataki kusikia wala hataki kukutana nao.

Mtu pekee aliyebakia kutuokoa wananchi wa Ukonga hasa tunaokaa Kivule, Kitunda, Majohe, Halisi, Hospitali ya Amana mpya, Viwege, Mbondole na maeneo yanayozunguka maeneo hayo tajwa ni Rais SAMIA SULUHU HASSAN.

Mheshimiwa Rais ule mradi wa DMDP ambao umesababisha maeneo kama yombo, buza na kwingine Dar es salaam kupata barabara za lami, Mradi ambao Jerry Slaa alikataa usifike kwenye maeneo mengi ya ukonga alipokuwa Meya ukaishia kujenga barabara ya Kampala University na Markaz tunaomba Mheshimiwa kwa mamlaka yako tukumbuke wana ukonga.

Tumechoka kula na kuogelea kwenye vumbi.
 
Huyo Mtoto Jeri hana bajeti ya kujenga hizo barabara.
Hili swala la kwenda kuiomba serikali ni kutufanya sisi wananchi ni wapuuzi.
MFUMO WA KUCHAGUA MTU KWA AJILI YA KUIOMBA SERIKALI UMEPITWA NA WAKATI.

TUWE NA MFUMO MPYA AMBAO KILA MBUNGE ATAKUWA NA UWEZO WA KUYATUMIA MAPATO YANAYOTOKA KATIKA MAENEO YAO NA KUWEPO NA MUNICIPAL BONDS ILI KUJENGA MIUNDOMBINO KAMA HIYO YA BARABARA NK.
 
Katika makosa ambayo Chama Cha Mapinduzi chini ya aliyekuwa Mwenyekiti taifa mwaka 2020 iliyafanya ni kumpendekeza Jerry Slaa kuwa mbunge wa Ukonga.

CCM ilijipa Certificate ya kukataliwa moja kwa moja na wana Ukonga kwa kutuletea huyu mbunge mwenye dharau, kiburi, majivuno na asiyejua wala kushughulika na kero za wananchi wa ukonga.

Ni katika kipindi chake wakati alipokuwa Meya, alizuia na kutumia ushawishi wake ili barabara za Banana hadi Kivule kupitia Kitunda isiwekwe lami. Sasa hivi barabara hizi ni mbovu kuliko kawaida.

Ni katika kipindi chake kama Mbunge haoni umuhimu wa barabara ya kutoka Ukonga Mombasa hadi Mbondole kuwekwa lami na ukimuuliza anajibu kwa jeuri, Mtajijua! Eti kwa kuwa mwaka 2015 ukonga walichagua mpinzani basi anawakomesha ili wasirudie tena. Mbunge wa namna hii anafanya wananchi waichukie serikali bila sababu.

Ni katika kipindi chake kama Mbunge barabara ya kutoka Pugu mpaka Viwege haina lami na hakuna mpango wowote wa kuweka lami siku za karibuni.

Huyu huyu Jerry Slaa haishi kwenye jimbo la ukonga. Pamoja na kuwa makazi yake na muda wake mwingi anakuwa hapa Dar es Salaam lakini hakai kabisa kwenye jimbo la ukonga.

Huyu huyu Slaa hafanyi mikutano na wananchi. Ukiachilia mikutano ya hadhara aliyokuwa anafanya wakati anaomba kura mwaka 2020 hajafanya mkutano hata mmoja na wananchi angalau hata kama kwenye hizi barabara mbovu yeye hapitishi gari lake wala havuti hewa iliyojaa vumbi basi asikilize tu kero za wananchi, hajawahi na hataki kusikia wala hataki kukutana nao.

Mtu pekee aliyebakia kutuokoa wananchi wa Ukonga hasa tunaokaa Kivule, Kitunda, Majohe, Halisi, Hospitali ya Amana mpya, Viwege, Mbondole na maeneo yanayozunguka maeneo hayo tajwa ni Rais SAMIA SULUHU HASSAN.

Mheshimiwa Rais ule mradi wa DMDP ambao umesababisha maeneo kama yombo, buza na kwingine Dar es salaam kupata barabara za lami, Mradi ambao Jerry Slaa alikataa usifike kwenye maeneo mengi ya ukonga alipokuwa Meya ukaishia kujenga barabara ya Kampala University na Markaz tunaomba Mheshimiwa kwa mamlaka yako tukumbuke wana ukonga.

Tumechoka kula na kuogelea kwenye vumbi.
CCM mbele kwa mbele
 
Nilikuja kivule kipindi barabara ya Banana kivule haijajengwa na ulikuwa msimu wa mvua aiseee ilikuwa balaaa! Kweli Ukonga barabara ziongezwe.
 
Hiyo barabara ikijengwa itatusaidia wengi Sana pia itakuwa mkombozi Kwa watu tunaoishi maeneo ya jirani mwaka Jana nilipita barabara hiyo aisee unaweza unafikiri upo vitani congo
 
Ila ukonga hawana bahati ya kuwa na wabunge haha
Alikuwepo mwana mama mmja mbunge wao sahv RIP dah alikuwa na majibu na nyodo sana kwa wapiga kura wake

Ova
Kama Jerry! Jerry ana dharau sijawahi kuona aisee. Ni kama sisi wana Ukonga ni wafanyakazi wake ametuajiri sio sisi wapigakura. 2025 sio mbali tuombe uhai
 
Uchaguzi umeshahujumiwa. Sasa hivi wabunge wa CCM wanaweza kipindi cha kampeni akaenda hata serengeti kula bata na akashinda 100%.
2025 anapita na hii ndiyo ajenda yao kubwa kuanzia balozi wa mtaa, mwenyekiti wa mtaa - NEC itakuwa CCM kwa njia yoyote ile iwe kwa ubaya au kwa uzuri na hii ilianza kipindi cha Magu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom