CHADEMA, Tusiuogope ukweli, tukubali kukosolewa

richone

Senior Member
Apr 3, 2012
146
35
Nawaombeni sana kama mnampenda Nasari kwa moyo wa dhati mwambieni ukweli, kwa kufanya hivyo mtakuwa mmemjenga na mmemsaidia.

Siwezi kukubali kumpamba Nasari ilihali najua kuwa ni kweli kachemka!!ni kweli alikurupuka kuzungumza kauli ile. Anachotakiwa kuelewa ni kwamba kila atakachoongea Nassari kina impact kwa jamii, hivyo basi wote waliomkosoa naungana nao weather wawe wana nia njema au mbaya mimi ninawaunga mkono kwani kauli aliyoitoa hakuipima, ni vizuri Nasari akawa makini kwa kauli yoyote atakayoitoa ajue inauzito kwa jamii kama kiongozi na asikurupuke kuufurahisha umma kwani ataaibika na hii itaweza kuharibu sura na taswira nzuri ya chama chetu hivyo kwa wapenda haki wote tuungane kwa hili tumrekebishe Nasari kwa nia Nzuri kabisa.

CHADEMA viongozi wake ni makini sii watu wa kukurupuka na wanachama wake ni watu makini pia. tusiwashambulie wale wanaompinga kwani hawa wanamsaidia huyu kijana wake.

Viongozi wake wakuu pia naamini hawajaifurahia kauli ile hivyo tukemee tumpime kama atarudia tena naamini yeye atajifunza na akiwa muungwana ataomba samahani kwa kauli yake, kwani CHADEMA haina nia wala mpango wa kuigawa nchi, na viongozi wa CHADEMA hawana mawazo ya kitoto.
 
Mkuu richone Mbona unarudia habari ambayo imeshakuwa na thread zaidi ya kumi humu jamvin kama huna cha kupost soma za wenzako tena wenzako wameelezea vizuri na wakashauri vizuri au hii topic imekua ni fashion mpya hapa jamvin . Nenda huko gamba mkubwa wewe kamshauri lusinde
 
Nawaombeni sana kama mnampenda Nasari kwa moyo wa dhati mwambieni ukweli, kwa kufanya hivyo mtakuwa mmemjenga na mmemsaidia.......
Wasamehe bure mkuu, maana wankumbuka walikotoka!
Kidumu chama cha CHADEMA, zidumu fikra za Nassari!!!
 
Mkuu richone Mbona unarudia habari ambayo imeshakuwa na thread zaidi ya kumi humu jamvin kama huna cha kupost soma za wenzako tena wenzako wameelezea vizuri na wakashauri vizuri au hii topic imekua ni fashion mpya hapa jamvin . Nenda huko gamba mkubwa wewe kamshauri lusinde

Nasary ni janga la kitaifa,

Hii habari hata ikirudiwa mara 100 ni sawa , yule bwana mdogo ni hatari sana anataka kuwagawa nyie wadanganyika.
 
Huna jipya we mwenda wazimu,una tuletea mambo ya kuku akinya,kanya bata akinya kaharisha.wapo waku mregebisha Nasari sio wewe,wewe kamregebishe Lusinde.
 
Naona umuhimu wa CHADEMA kujitofautisha na CCM eti kwakuwa na`ccm wanatukana basi na sisi CHADEMA tutukane hiyo sii sawa na mimi mwenyewe ni mwanaCHADEMA pia sipendi kushabikia hili swala ila naona kwasababu rafiki zangu na wanaCHADEMA wenzangu wamepigwa upofu nao wanataka kuchagua Upofu nimelazimika kuandika ili tuwe katika njia sahihi.CCM ni wasema hovyo sidhani kama ni sahihi kwa wanaCHADEMA nao kuwa wasema hovyo. Nasisitiza viongozi CHADEMA na wana chama wake ni watu makini mnno na kila watoapo kauli zao huwa wanazipima nashauri Nasari apime kauloi zake.
 
ninachoshindwa kuelewa ni kwa nini hii thread inaongezeka humu jamvini wakati mbowe alilitolea maelezo hili swala palepale na bado nassari mwenyewe keshaliongelea hili swala na zaidi vyombo husika vinalifanyia kazi.Mbona lusinde alitoa matusi ya nguoni na bado viongozi wake wakamuunga mkono hatukushauri namna hii
 
Nimekuwa nikifuatilia kwa makini mwenendo wa viongozi wa CHADEMA na wafuasi wake na kugundua ni wagumu mno kukubali kukosolewa pale Chama kinapo kuwa kimekwenda visivyo.
Viongozi wa CHADEMA karibuni wamebebeshwa mzigo wa kuzuka kwa vurugu kwenye mikutano mingi na kusababisha mauaji.Hizi ni shutuma nzito,lakini pro-CHADEMA wengi wamekuwa wakikabili yeyote atakaye-challenge uhusika wa CHADEMA katika haya kwa dhihaka,matusi na kejeli.
Hata mambo kadhaa yaliyo ikumba na kuitikisa CHADEMA hujibiwa kwa dhihaka,kejeli na hata matusi toka kwa pro-CHADEMA wengi na hata viongozi mara nyingine.
Mimi kama miongoni mwa mashabiki wa CHADEMA nakuwa na wasiwasi kwa mwenendo huu,CHADEMA itakapo shika dola si itageuka kipofu na kuwa mbaya kuliko CCM?
Nashauri pro-CHADEMA tugeuze mtazamo na kuitazama CHADEMA kwa mtazamo chanya na kujibu hoja kwa hoja na wala si matusi,dhihaka na kebehi.Hii haijengi bali inabomoa chama.
Viongozi wa CHADEMA nao wawe responsible kwa kutupeleka watanzania kuelekea Tanzania tuitakayo!
TANZANIA,nakupenda sana.
 
Mkuu hayo ungeyapeleka makao makuu au kwenye vikao rasmi vya Chama sio ulete hapa jamvini kishabiki sasa uanafaidika na nini kuiweka hapa au kuongeza idadi ya post? Hizo ni tabia za magamba sasa umepost nenda kwa nape ukachukue chako
 
Hivi kwanini katika picha zote za vurugu za Nyololo Mufindi Dr. Slaa haonekani? Yeye alijificha wapi wakati aliwaambia mashabiki wake waje wasiogope kitu mpaka kieleweke?
 
Mkuu hayo ungeyapeleka makao makuu au kwenye vikao rasmi vya Chama sio ulete hapa jamvini kishabiki sasa uanafaidika na nini kuiweka hapa au kuongeza idadi ya post? Hizo ni tabia za magamba sasa umepost nenda kwa nape ukachukue chako

Kama mtu anaye itakia mema nchi yangu na CHADEMA sina budi kuweka haya katika public kwa manufaa yetu sote.
 
Nimekuwa nikifuatilia kwa makini mwenendo wa viongozi wa CHADEMA na wafuasi wake na kugundua ni wagumu mno kukubali kukosolewa pale Chama kinapo kuwa kimekwenda visivyo.
Viongozi wa CHADEMA karibuni wamebebeshwa mzigo wa kuzuka kwa vurugu kwenye mikutano mingi na kusababisha mauaji.Hizi ni shutuma nzito,lakini pro-CHADEMA wengi wamekuwa wakikabili yeyote atakaye-challenge uhusika wa CHADEMA katika haya kwa dhihaka,matusi na kejeli.
Hata mambo kadhaa yaliyo ikumba na kuitikisa CHADEMA hujibiwa kwa dhihaka,kejeli na hata matusi toka kwa pro-CHADEMA wengi na hata viongozi mara nyingine.
Mimi kama miongoni mwa mashabiki wa CHADEMA nakuwa na wasiwasi kwa mwenendo huu,CHADEMA itakapo shika dola si itageuka kipofu na kuwa mbaya kuliko CCM?
Nashauri pro-CHADEMA tugeuze mtazamo na kuitazama CHADEMA kwa mtazamo chanya na kujibu hoja kwa hoja na wala si matusi,dhihaka na kebehi.Hii haijengi bali inabomoa chama.
Viongozi wa CHADEMA nao wawe responsible kwa kutupeleka watanzania kuelekea Tanzania tuitakayo!
TANZANIA,nakupenda sana.
Mkuu kwenye mikutano yao chadema ni watulivu mno. Wangejaribu kufanya maandamano kama waliyofanya waislam leo bila kibali kudai wenzao waachiwe waliovunja sheria halali ya nchi ya kuhesabiwa, ingemwagika damu nyingi sana...jiulize kwanini
 
Back
Top Bottom