zomba
JF-Expert Member
- Nov 27, 2007
- 17,240
- 3,910
Nimekuwa nikifuatilia kwa makini mwenendo wa viongozi wa CHADEMA na wafuasi wake na kugundua ni wagumu mno kukubali kukosolewa pale Chama kinapo kuwa kimekwenda visivyo.
Viongozi wa CHADEMA karibuni wamebebeshwa mzigo wa kuzuka kwa vurugu kwenye mikutano mingi na kusababisha mauaji.Hizi ni shutuma nzito,lakini pro-CHADEMA wengi wamekuwa wakikabili yeyote atakaye-challenge uhusika wa CHADEMA katika haya kwa dhihaka,matusi na kejeli.
Hata mambo kadhaa yaliyo ikumba na kuitikisa CHADEMA hujibiwa kwa dhihaka,kejeli na hata matusi toka kwa pro-CHADEMA wengi na hata viongozi mara nyingine.
Mimi kama miongoni mwa mashabiki wa CHADEMA nakuwa na wasiwasi kwa mwenendo huu,CHADEMA itakapo shika dola si itageuka kipofu na kuwa mbaya kuliko CCM?
Nashauri pro-CHADEMA tugeuze mtazamo na kuitazama CHADEMA kwa mtazamo chanya na kujibu hoja kwa hoja na wala si matusi,dhihaka na kebehi.Hii haijengi bali inabomoa chama.
Viongozi wa CHADEMA nao wawe responsible kwa kutupeleka watanzania kuelekea Tanzania tuitakayo!
TANZANIA,nakupenda sana.
Umeona eeh? tazama wanavyotokwa na povu!