CHADEMA: Tuko tayari kwa UKUTA 01/09/2016

Alice Gisa

Senior Member
Sep 6, 2014
172
417
TAMKO LA CHADEMA KANDA YA SERENGETI KUJIPANGA NA OPERATION UKUTA

1.0 Utangulizi.

Ndugu wanahabari,

Kwa Kurejea kikao cha kamati kuu ya CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA) ya tarehe 23-26/07/2016. Kilichofanyika Bahari beach Hotel, jijini Dar es Salaam. Na kwa kuzingatia Tamko lililotolewa na Mwenyekiti wa CHADEMA taifa Mhe Freeman Mbowe kwa niaba ya kamati kuu na CHADEMA nchi nzima.

Kanda ya Serengeti imewaiteni kuwajulisha tunavyoendelea kujipanga katika kufikia lengo kuu la operation UKUTA.

Kama ilivyoandaliwa na kamati kuu ya chama UKUTA maana yake ni UMOJA WA KUPAMBANA NA UDIKITETA TANZANIA. UKUTA ni operation yenye lengo kuu la kuzuia ubinywaji wa Demokrasia unaofanywa na Serikali ya awamu ya Tano. Na ijulikane Serikali hii haijabana Demokrasia kisiasa tu bali imekiuka hata misingi ya utawala bora.

Ndugu wanahabari.

Wote mnakumbuka tangu serikali ya awamu ya Tano ishike hatamu Rais aliitaka Mahakama kuu iwahukumu wafanyabiashara ambao wana kesi za kodi na kuhakikisha serikali inashinda kesi.

Wote mnakumbuka namna serikali ilivyo liingilia Bunge tukufu na kupanga kamati za Bunge kinyume na kanuni za Bunge.

Wote mnakumbuka Serikali ilivyofanya hujuma ya kuzuia matangazo ya Bunge kuwa ya moja kwa moja “live”.

Wote mmeshuhudia wabunge wa UKAWA wakinyanyaswa na kudhalilishwa Bungeni, wakati huo wabunge wetu wamekuwa wakiadhibiwa adhabu kubwa kubwa zenye lengo la kudhohofisha utendaji kazi wao kama wabunge.

Wote tumeshuhudia hotuba za upinzani zikifutwa bungeni bila kujali kanuni za Bunge lenyewe

Wote tumeshuhudia serikali ikiwafukuza wanachuo wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) bila taratibu zinazoelezeka.

Wote ni mashahidi namna serikali na jeshi la Police walivypinga marufuku mikutano ya hadhara ya vyama vya upinzani, wakaenda mbali kwa kuzuia hata makongamano na mikutano ya ndani. Wakati huo wakizuia wapinzani chama tawala wanafanya mikutano tena live kwenye Televition na maandamano juu.

Wote mmesikia namana wafanyabiashara wamepelekewa “bill” kubwa za kodi na kutaka wazilipe na wakilalama wanazuiliwa akaunti zao za benki.

Wote tunashuhuhia namana mashirika na makampuni yanavyopunguza wafanya kazi kwa kasi.

Wote tumesikia jinsi mabalozi na wanadiplomasia wa kimataifa kuzuiliwa kufanya kazi zao bila kibali maalum cha serikali hali inayodumaza shughuli za kidiplomasia nchini.

Wote tumesikia ukaguzi wavyeti unavyofanywa kimakanika baadhi ya taasisi mfano mashule walimu wamefanyiwa paredi na kisha wanafunzi kuitwa kuthibitisha utumishi wao.

Wote tumeona kule Arusha pale Mawakili wameanza kuunganishwa na wateja wao, sasa sijui serikali haitaki walalamikaji /watuhumiwa kuwa na mawakili mahakamni

Wote tunashuhudia mateso na unyanayasaji mkubwa unafanyika huko visiwani Zanzibar.

2.HATUA TULIZOCHUKUA SISI CHADEMA KANDA YA SERENGETI.

Ndugu Waandishi wa habari.

Kanda ya serengeti ni jumuisho la mikoa ya Mara, Shinyanga na Simiyu. Katika kutafakari kanda hii tulijikumbusaa hekima ya Dictator Mkubwa Bw Aldoph Hitler aliyewahi kusema “Where Diplomacy ends, War Begins” .Hivyo kwa muktadha huo ukiona mtu anakataa diplomacy (mashauriano) basi jua mtu huyo anajiandaa kwa ghasia au vita kabisa.

Sisi kanda ya Ziwa tumekuwa wahanga wakubwa wa vifo tangu serikali ya awamu ya tano ishike hatamu.

Wote nmnakumbuka mauaji cha kipenzi chetu Kamanda Alphonce Mawazo aliyekuwa Mwenyekiti wa Mkoa wa Geita, Mawazo aliuwa mchana kweupe na hadi leo hakuna hata mtuhumiwa. Serikali itambue sasa Kanda yetu tuko tayari kufa kama Mawazo tena kama hawataki kuruhusu haki zetu wajiandaae kutuua september moja tutakapoanza operation UKUTA.

Hadi leo Mkoani Simiyu tayari wenyeviti wetu wawili wa vijiji wameuawa wanyeviti hao walikua chachu ya mabadiliko, wameuawa kifo kama cha Mawazo. Hii inatukumbusha ushairi wa Almando Guebuza unaoitwa “if must die” serikali hii imetufikisha mahala tunaamini lazima tutauawa ndani ya miaka mitano. Hivyo siye tutachagua kufa kwenye maandamano.

Leo tunaongea hapa baadhi ya watumishi wa umma waliokuwa wanatuunga mkono wamefukuzwa kazi, wengine wamesimamishwa na mmoja amefungwa kabisa. Mwalimu mmoja amefungwa kifungo cha miaka miwili huko, wilayani Meatu Mwl huyu amehukumiwa kutokana na ushiriki wake katika uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2014.

Siyo mwalimu huyo tu Bali hata madiwani wetu na wabunge wanakesi nyingi, tarehe 27/07/2016. Diwani wetu huko wilaya Rorya amefungwa mwaka mmoja jela.

Makamanda wa CHADEMA SI WAMEFUNGWA JELA TU yupo mmoja aliyekuwa mwenyekiti wa kijiiji katika kata moja wilayani Meatu amefungwa KUNYONGWA na sisi tunaamini alijumuishwa katika kesi ya mauaji kutokana na kuikatalia CCM kutoa ushahidi wa kumtia hatiani aliyekuwa mbunge wa Meatu Mh. Opulukwa.

Kwa hofu kubwa na fitina tunayofanyiwa sisi WATANZANIA ambao kwa haki yetu ya kikatiba tuliamua kujiunga na vyama vya upinzani hasa CHADEMA tumeuona mpango huu wa operation UKUTA kuwa njia ya sahihi ya kuokoa taifa letu kuangukia mikono isiyo salama.

Hivyo uongozi wa kanda na mikoa katika kanda yetu umeazimia kuwa na vikao vya kimkakati kufanikisha adhima ya maandamano September Moja 2016.

Tulishamaliza kujipanga na kupangana katika mikoa ya kanda yetu tar 30/7/2016 tulifanya Shinyanga 3.08.2016 Mara na Mkoa wa Simiyu ilikuwa tarehe 05/08/2016. Sasa tunaendelea kujipanga katika kata 384 za kanda yetu ya serengeti tumeanza na kata za Mkoa wa Shinyanga ambapo tutagawa bendera 275000 ili kufikia Tar 30/8/2016 kila mwanachama,watanzaniana wapenziwote wa CHADEMA Waanze kupeperusha Bendera.

Tunawaambia viongozi wetu wa mikoa, majimbo na kata ya kuwa wakati wa kudhihirisha nani mwanamabadiliko na nani msaliti utaanza september 1,2016.

MSIOGOPE MAKAMANDA.

Nzemo RP

Katibu wa Kanda- Serengeti.
 
Wote mliona mbunge sugu alivyolidharau mbunge kwa kuonyesha dole la kati na upewa kaadhabu kadogo na naibu spika.

Wote mlisikia mbunge msingwa alivyotukana matusi makubwa akiwa ITV ma adhabu hakupewa na adhabu kupewa itv.
Hayo ni machache ambayo yalisahaulika kwenye kakikao uchwara huko serengeti
Vijan tupo imara kuubomoa ukuta wa tofali mbichi utakaojengwa
 
Nipende kutoa mwaliko kwa police wote nchini katika mikutano na maandamano ya ukuta
Iwe kwa shari au kwa amani kama tunavyofanya sisi wapenda demokrasia na tunaochukia udicteta katika nchi

Karibuni sana ndani ya ukuta

UKUTA ndio habari ya tanzania hauzuiliki
 
Hii mikwara tu,na hata mleta uzi ameutoa kiuchochezi haswa!
Huyu naye jibu...
Ninyi tunawajua,mnapambania matumbo yenu.
 
Mnawanyima usingizi wenzio wanawaza wajipange vp kupambana na UKUTA nchi nzima, pambana makamanda! Tuko pamaoja hata km tuko nje ya nchi. Huku niliko democrasi ni asilimia 100,kila chama cha siasa kina haki sawa kulingana na katiba ya nchi, kweli nchi za kiafrika bado tuna safari ndefu sn kuwafikia hawa wenzetu!
 
Wote mliona mbunge sugu alivyolidharau mbunge kwa kuonyesha dole la kati na upewa kaadhabu kadogo na naibu spika.

Wote mlisikia mbunge msingwa alivyotukana matusi makubwa akiwa ITV ma adhabu hakupewa na adhabu kupewa itv.
Hayo ni machache ambayo yalisahaulika kwenye kakikao uchwara huko serengeti
Vijan tupo imara kuubomoa ukuta wa tofali mbichi utakaojengwa

Ninyi endeleeni kushangilia wakati wenzetu wanauwawa na kunyanyaswa huku mikoani.

Sie tulioko katika mikono ya dhuruma hatutaacha kupambana.
 
Amani ikitoweka nchi hii, au hata damu ya mtu mmoja kumwagika basi serikali na JPM hawatokwepa lawama kwa maana sheria na katiba ya nchi viko wazi kabisa juu ya haki ya kufanya siasa kupitia mikutano kwa vyama vya siasa!
 
Jamani chonde chonde na UKUTA....naona mahakama ya ICC inakuja na sijui kama tunao kina Kibatala na Tundu Lissu wengi.Tuongeeni yaishe.....nyiye viongozi wa dini muko wapi...????hasa wale wa kamati ya Amani.....hatupendi sura zenu kwenye TV....Tunataka mayendo yenu ya kimaliza hili la Ukuta salama.
 
Back
Top Bottom