CHADEMA ndio wamesababisha mgomo wa madaktari

Dec 11, 2010
3,321
6,328
TAARIFA za kiintelijensia zimebaini kuwa CHADEMA ndio wamesababisha mgomo wa madaktari, mgomo ambao umeendelea kwa siku kadhaa sasa na umehatarisha maisha ya wagonjwa wengi na umesababisha hata madaktari kuvuana uanachama kwenye chama chao cha madaktari.

CHADEMA ndio hao hao wamekuwa wanaratibu migomo mingi kwenye vyuo vikuu, ndio haohao wameratibu mgomo wa madereva wa malori kule Mbeya lakini pia ni CHADEMA walio hakikisha Naibu Waziri wa Afya anagoma kwenda kuonana na madaktari pale kwenye ule ukumbi walioandaa wao maana protokali na usalama wake ulikuwa hatarini.

Hawa CHADEMA hawafai, maana wanataka nchi isitawalike, Wanafanya haya wakijua kuwa Rais Kikwete yuko kwenye mkutano wa uchumi duniani na kule anakutana na kuongea ikiwa ni pamoja na kupiga picha na Bill Gates na matajiri wengine wa dunia ili watusaidie kujikwamua kutoka kwenye mkwamo wa njaa na uchumi mbovu.

CHADEMA ndio hawa hawa wamesababisha sasa hivi shilingi yetu imeshuka thamani maana muda mwingi wanautumia kuwasumbua watu waliokuwa wanajua matumizi ya shilingi na sasa wamekasirika na matokeo yake shilingi imeshuka thamani.

CHADEMA ni watu wabaya sana, maana baada ya mgomo huu wa madaktari wataandaa mgomo mwingine waliouahirisha na walimu mwaka jana, wanachowaza CHADEMA ni migomo tu ili serikali idorore na nchi isitawalike, CHADEMA ni chama cha fujo na maandamano.Chama hicho kimewezesha mgomo mpaka ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na kusababisha wale makada wenye magamba kugoma kuvua magamba yao! Hiki chama ni kibaya sana kinawanyima usingizi viongozi na makada wa chama cha magamba.

Watanzania mtambue kuwa CHADEMA ni chama kibaya sana maana ndicho kimesababisha minong'ono, eti Dk. Harrison Mwakyembe amewekewa SUMU! Nani amuue kiongozi huyo?

Mwakyembe hana tatizo kubwa anaugua tu mafua na hata ripoti yake ni CHADEMA hao hao ndio wameizua, maana wanajua kuwa ikiwekwa hadharani italeta tena mambo yake yenye harufu ya ki - Richmond.

CHADEMA ni watu wabaya sana, maana wamesababisha maisha magumu kwa kila Mtanzania, tofauti na ahadi za CCM kutaka kuwapa maisha bora kila Mtanzania, chama hicho kimesababisha mpaka umeme unatolewa kwa mgawo na unakatika katika mara kwa mara.

Tusiwaamini watu hawa, maana wanataka kuiondoa serikali iliyoko madarakani kwa maandamano kwa madai kuwa imeshindwa kuboresha huduma za msingi kwa Watanzania.

Nadhani sasa ni wakati muafaka kwa CHADEMA kimsababishe Rais Jakaya Kikwete agome kuingia IKULU, ili nchi iingie kwenye uchaguzi kabla ya mwaka 2015, kwakuwa huko kote kutakuwa mbali sana.

Hii ni siri yako! Hata yale mafuriko yaliyotokea jijini Dar es Salaam na kusababisha ndugu zetu kuhamia kwenye majumba ya nguvu kule Mabwepande, ni jamaa hawahawa wakiongozwa na makamanda wao. Hawa jamaa ni nuksi!

UPDATE:

Makala hii imenukuliwa na Tanzania Daima la 29 Jan 2012 bila kutoa source
 
Kwikwiwkwi yaani nimecheeeeeeeeeeka hadi utumbo ulioko tumboni unauma sasa imagine nimecheka vipi .

Chademaaaaaaaaaaaaaaaaaa wameangusha Uchumi wa Tanzania.

Chadema hawa hawa wana ratibu safari nyingi sana za JK nje Nchi anatumia tu sisi tunakufa.

Chadema wamembana Pinda hadi kaongeza posho kwa wabunge wengi wa CCM mle mjengoni.
 
Ni kweli mkuu wasivyo na ufahamu lazima wako biz kujaribu ku link huu mgomo na cdm ili mwisho wa mwezi hotuba ijae japo kurasa moja maana hawana jipya.
 
kama ndo wenyewe wamemsababisha dr hamis kigwangala(MB) naye aungane na madaktari wenzie kugoma basi wanaweza kumgomesha vasco da gama kwenda kazin white house. Ila angekuwepo makamba angeshatoa tamko la wachochezi ni akina nani. Juz tu MSD wamemwaga dawa zilizoexpire wakati mtwara panadol tu ni mtihani.
 
Ungeongeza CHADEMA ndiyo imegoma kuwalipa Intern Doctors na ndiyo imekataa kutoa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya Juu! Foolish!
 
mwanzoni nilidhani unakisema cdm, lakini baada ya kusoma mpaka mwisho, kumbe unasend msg kwa magamba kwa jinsi walivyo na mawazo mgando. Its true, some magamba politicians will come up with this conclusion.
 
Ni hawa CHADEMA wanaosababisha hazina ya serikali kukaukiwa...ni hawa CHADEMA ndio wanasababisha umeme wa mgao na mvua kutonyesha,ni hawa CHADEMA ndio wanasababisha raisi aonekane hafai kule kwenye mkutano wa Davos..ni hawa CDM ni hawa CDM yes!!
 
aaaah mkuu!kumbe chadema wanaweza?na kama wanaweza kuratibu migomo ya wasomi then wana uwezo mkubwa wa kuendesha serikali!
 
Mkuu mleta thread; ni vizuri unapo-copy na ku-paste kazi za watu uka-acknowledge source. Hii post yako ume-copy neno kwa neno toka Gazeti la Tanzania Daima la leo 29th January 2012. Plagiarism haikubaliki tena ni ufisadi kama ufisadi mwingine; just acknowledge tu source inatosha.

"Habari" yenyewe hii hapa: CHADEMA ndio wamesababisha mgomo wa madaktari

Kama sijakosea uzi kama huu ulikuwa hapa jana ila ukahamishiwa kwenye jukwaa la udaku, labda hao TZ DAIMA ndo wali copy & paste.
 
Kama sijakosea uzi kama huu ulikuwa hapa jana ila ukahamishiwa kwenye jukwaa la udaku, labda hao TZ DAIMA ndo wali copy & paste.

Ndugu hakuna la maana uliloongea kuhusiana na hoja husika. Hoja ya msingi ni "acknowledgement". Kama Tanzania Daima nao wame-copy & paste bila ku-acknowledge haihalalishi mwingine kufanya hivyo hivyo! Otherwise, hata kama hoja yenyewe ilikuwa humu JF still mwinge anapoi-copy anapaswa pia ku-acknowledge. Mkuu fikiria kwa mapana.
 
Jamani tusiishie kusoma kichwa cha Thread tu. Tusome ujumbe na kutafakari. Naomna watu wamedakia nakuanza kuponda mtoa mada. Tofauti na tulivyowazoea kauli za watala wa nchi hii kuhusiana na migomo inayotekea nchini, mgomo huu wa madaktali haujahusishwa na CHADEMA. Nimejiuliza sana kulikoni ila sijapata majibu. Msg ya mtoa mada inalenga kuonyesha kuwa baada ya kuelemewa watawala hawa sasa wameanza kuelewa. Wemeshagundua kuwa mkakati wa kutuhumu CDM ili kujinasua na matatizo ya wananchi hakukisaidii chama chao CCM bali unakiangamiza pamoja na serikali yake.

Kwa kujua ama kutoa Viongozi wa CCM na serikali wameijenga CHADEMA kwa kuitambulisha kama mtetezi wa wananchi.
 
Back
Top Bottom