mzee wa wino
Member
- Jan 19, 2012
- 5
- 0
sasa tuwafanyie nn chadema? Kama hali ndo hiyo?
Mzee E Mtei.
Ni vizuri kama ungeibandika hiyo makala hapa jamvini unajua sisi wengine tulishalidharau Tanzania daima siku nyingi hasa baada ya kusoma makala nyingi zilizokuwa na muelekeo wa kuwatetea mafisadi.
Kama WanaJF wanavyofahamu, mimi binafsi nilihusika sana na uasisi wa CHADEMA, na licha ya kwamba niliachia uenyekiti (taifa) tangu 1998 nimeendelea kuwa mjumbe wa Kamati Kuu. Nimefarijika sana na hatua na mwenendo wa hiki chama ktk miaka hii ya karibuni. Mzee Mtei ni mzee mwenye furaha sana kutokana na mafanikio ya chama alichokiasisi.
Lakini nimefadhaishwa sana na makala iliyoandikwa na "Wanabidii" ktk Gazeti la TzDaima la jana Jumapili ikizusha eti Chadema ndio kimesababisha mgomo wa madaktari!! Madaktari wamegoma kutokana maslahi duni, wakati viongozi wengi, wakiwemo Wabunge wanajiongezea posho!!
Madai mengine ni kwamba CDM wamesababisha thamani ya Shilingi kushuka na kuleta mfumko wa bei. Eti Mheshimiwa Rais wetu anakutana na Bill Gates huko Davos, na huyu tajiri wa Kimerikani atatusaidia! Lazima tutambue matatizo ya mfumko wa bei yatatatuliwa na sisi wenyewe kisiasa kwa kushusha au kuondoa kodi katika bidhaa muhimu na kuzalisha kwa wingi.
Makala hii imeendelea kutoa lawama likuki kwamba CDM ndio tunasababisha taabu na matatizo ya WaTz., hata kwamba minong'ono ya viongozi wa CCM kulishwa sumu ni sisi tumeanzisha! Pale hawa "Wanabidii" walipofikia kulaumu eti Chadema ndio walisababisha mafuriko yaliyolikumba jiji la Dar es Salaam, ndipo nilipofikia uamuzu kwamba nishauri Makala hii ipuuzwe!!
Nimeandika jibu hili kwa hii Makala, kwa vile najua Watanzania wengi wanasoma Tanzania Daima na huenda wengi wao wakadhani kuna chembe ya ukweli. Hakuna!!! Chadema ni chama makini, kinachoongozwa na WaTz wazalendo, wenye kupenda nchi yao. Wanajali matatizo na adha zinazowakabili wananchi na wananuia kwa dhati kukabiliana nazo kwa umakini,ujasiri na uzalendo. Ni lazima uongozi wa nchi upige vita rushwa na ubadhirifu wa fedha za umma unaofanywa na baadhi yao.
Kauli mbiu yetu ni HAKUNA KULALA, MPAKA KIELEWEKE!!!!!!.
Edwin Mtei.
ikisomwa na mtu mwenye upeo ataipambanua lakini je ikitokea imesomwana mtu wa tofauti na hapo nini madhara yake....Wadau Mwandishi anaibeza serikali, hamanishi kwamba chadema ni chama kibaya.
Pale hawa "Wanabidii" walipofikia kulaumu eti Chadema ndio walisababisha mafuriko yaliyolikumba jiji la Dar es Salaam, ndipo nilipofikia uamuzu kwamba nishauri Makala hii ipuuzwe!!
Edwin Mtei.
ikisomwa na mtu mwenye upeo ataipambanua lakini je ikitokea imesomwana mtu wa tofauti na hapo nini madhara yake....