Elections 2010 Chadema nayo itapewa label ya 'chama vurugu' na serikali ya CCM?

HAWATAWEZA KWANI NI ISHU KUBWA NAWASIWASI KUNA HATARI YA MTU KUACHA ROHO MAANA HATA HIZO CAMERA ZITAVUNJWA
cONQUEST-MWAKA HUU LAWAMA ZITAKUWA TELE ILA CCM DAIMA
 
HAWEZI MKUU MAISHA YAKE YATAKUWA HATARINI MAANA WANAHASIRA SANA CCM MWAKA HUU WANATUMIA MIJIHELA MINGI ILI KUFANIKISHA YAO SASA NANI ATAKUBALI ILE KWAKE.
cONQUEST-MWAMBIE WILLY GAMABA ATUONE SIE WAKEREKETWA TUMPE ISHU
 
Watu waliopata kuwa CCM na kutumika kwenye kampeni za namna hii utawajua tu. Wameshiriki kikamilifu kwenye hizo shughuli kwenye chaguzi zilizopita.:becky:
 
Hapo ndo ninapoona dalili zote za umwagaji damu mwaka huu. Kikwete amejitahidi kuwa mtu honesty katika mambo ya kujali haki na usawa wa watanzania. Ninawasiwasi kwamba atajiharibia record yake nzuri aliyoiweka katika muda wa miaka mitano kwa kuiacha nchi iingie vitani. Nina wasiwasi kwamba Kikwete atatengeneza historia mbaya kwa kuwa Rais pekee aliyeiingiza Tanzania katika machafuko. Naogopa kwamba Tanzania inaweza kujikuta inaingia katika kundi la nchi ambazo ni politically unstable na kuharibu sifa zote za kuwa kisiwa cha amani.

Kwa wale mlio karibu na Kikwete hebu jaribuni kumshauri ili awaachie watanzania waamue ni nani wa kuwaongoza, na aache kulazimisha mambo yasiyowezekana.
 
Hapo ndo ninapoona dalili zote za umwagaji damu mwaka huu. Kikwete amejitahidi kuwa mtu honesty katika mambo ya kujali haki na usawa wa watanzania. Ninawasiwasi kwamba atajiharibia record yake nzuri aliyoiweka katika muda wa miaka mitano kwa kuiacha nchi iingie vitani. Nina wasiwasi kwamba Kikwete atatengeneza historia mbaya kwa kuwa Rais pekee aliyeiingiza Tanzania katika machafuko. Naogopa kwamba Tanzania inaweza kujikuta inaingia katika kundi la nchi ambazo ni politically unstable na kuharibu sifa zote za kuwa kisiwa cha amani.

Kwa wale mlio karibu na Kikwete hebu jaribuni kumshauri ili awaachie watanzania waamue ni nani wa kuwaongoza, na aache kulazimisha mambo yasiyowezekana.

Hivi nyinyi watu historia ya nchi hii hamuijui au mnajifanya hamuijui? Wakati wa Mkapa watu washauliwa kule Zanzibar na pale Mwembechai. Sasa iweje leo itokee uchafuzi kwa sababu ya wazembe wachache watakaokataa kukubali matokeo na yeye aje kuwa "Rais wa kuingiza Tanzania kwenye machafuzi"? Mtu ambaye hajui historia ya Tanzania ya miaka 15 iliyopita atajua yaliyotokea wakati wa Nyerere? :becky:
 
Matayarisho hayo yamekamilika kwenye baadhi ya mikoa, na yanaendelea kutolewa kuwaanda vijana wa ccm kufanya vurugu kwenye uchaguzi.

CHADEMA wanao mkanda wa video ukionyesha, jinsi maandalizi yaho yalivyofanyika mkoani Kilimanjaro na walimkabidhi mkuu wa polisi wa mkoa ambaye hadi leo amekaa kimya.

Chadema ni lazima walinusuru taifa, kwa kutoa huo mkanda hadharani, ili watanzania waone matayarisho ya vijana wa ccm kuvurunga uchaguzi mkuu ujao.
 
Kuna viongozi wa Kiafrika wenye utu kama Kaunda ambao wakishindwa kwenye kura huachia madaraka kwa amani. Hao huheshimiwa sana. Wako wengine kama Mugabe ambao hupiga, galagaza na kuua wananchi ili mradi wabaki madarakani. Rais wetu wa sasa, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, ni kama Kaunda au ana mwelekeo wa kuwa kama Mugabe?

CCM is for peace, but only if it wins. Kwa vingine wamejitayarisha kuleta vurugu ili waendeleze ukiritimba wao wa madaraka. Lakini naamini hawatafanikiwa. Rais Kikwete atabidika kuachia madaraka kama alivyofanya Moi.

Kuweko na Documentaion Officer wa CHADEMA. Aweke ushahidi kuhusu wanaoleta vurugu ili baadaye wafikishwe kwenye vyombo vya sheria. Kuwe na orodha ya makamanda wa polisi ambao wameamuru Watanzania wapigwe. Hao wataajibishwa sana mara baada ya UKOMBOZI.

Wananchi mliopo Tanzania saidieni kupiga picha za vijana na polisi wanachochea vurugu. Zitatumika kuwafikisha kwenye mkono wa sheria mwakani.

Je, Ndugu Ali Mkumbwa alipoandika maoni yake ya mhariri "UKWELI ni kwamba Dr. Slaa hatakuwa Rais" alikuwa anaju nini? Alijua mipango ya CCM ya kuleta machafuzi? Amehusika nayo?
 
HAWATAWEZA KWANI NI ISHU KUBWA NAWASIWASI KUNA HATARI YA MTU KUACHA ROHO MAANA HATA HIZO CAMERA ZITAVUNJWA
cONQUEST-MWAKA HUU LAWAMA ZITAKUWA TELE ILA CCM DAIMA

HAWEZI MKUU MAISHA YAKE YATAKUWA HATARINI MAANA WANAHASIRA SANA CCM MWAKA HUU WANATUMIA MIJIHELA MINGI ILI KUFANIKISHA YAO SASA NANI ATAKUBALI ILE KWAKE.
cONQUEST-MWAMBIE WILLY GAMABA ATUONE SIE WAKEREKETWA TUMPE ISHU
Nimependa namna unavyowasilisha hoja. hizo bold zina maana kubwa ktk uelewa wangu

Wanajamvi nawaomba mlioko kwenye maeneo mahususi msizipuuzie hizi taarifa. Lazima Tanzania ibaki ktk utulivvu na amani huku haki ikitendeka. Upuuzi wa watawala wa kiafrika hupelekea akina mama na watoto kuwa displaced mpaka nafsi zao.
 
headline_bullet.jpg
Mgombea wa CUF Musoma anusurika kifo
headline_bullet.jpg
Skafu ya CCM yamponza kijana huko Vunjo
headline_bullet.jpg
Z`bar mmoja apigwa akitoka mkutano wa Shein



CUF%2820%29.jpg

Chama Cha Wananchi (CUF)

Mikutano ya kampeni inayoendelea sehemu mbalimbali nchini, imeripotiwa kutawaliwa na vurugu kwa baadhi ya wagombea na wafuasi wa vyama vya siasa kushambuliwa.

Katika tukio la kwanza Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF) wilaya ya Musoma Mjini, Didi Msira Koko, amenusurika kufa baada ya kupigwa na watu wasiojulikana.

Hata hivyo, Didi anasema kuna mazingira yanayoashiria kwamba shambulizi hilo lina uhusiano wa kisiasa, huku akielekeza shutuma zake kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Tukio hilo dhidi ya Koko ambaye pia ni mgombea udiwani wa kata ya Iringo katika Manispaa ya Musoma, lilitokea juzi jioni.

Koko amelazwa kwenye wodi namba mbili katika Hospitali ya Mkoa wa Mara mjini hapa.
Akizungumza na NIPASHE jana, alisema alivamiwa Septemba 25, mwaka huu wakati akitembea kwenye barabara ya Nyerere, muda mfupi baada ya kumalizika mkutano wa kampeni za CCM uliohutubiwa na mgombea urais wa chama hicho, Rais Jakaya Kikwete.

Kamanda wa Polisi mkoani Mara, Robert Boaz, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo wakati akizungunza na NIPASHE kwa njia ya simu.

Boas alisema polisi inaendelea na uchunguzi kuhusiana na tukio hilo, huku akionya kwamba halipaswi kuhusishwa na masuala ya siasa.

Hata hivyo Koko akizungumzia tukio hilo akiwa hospitalini hapo, alisema aliitwa na kundi la watu aliowafahamu na baada kuwafikia, walianza kumvuta shati na kumpiga.

Alisema aliokolewa na miongoni mwa wananchi waliokuwa wakitoka katika mkutano huo.
Alidai kuwa watu waliompiga walikuwa vijana waliovaa sare za CCM na alimtambua mmoja kuwa ni ndugu wa mgombea ubunge wa CCM jimbo la Musoma mjini.

Koko alisema wakati wananchi hao walipofika kumuokoa, alikuwa ameshapigwa, kupoteza nguvu na kurushwa mtaroni huku akiwa ameumia kichwani, mguu wa kulia na sehemu mbali mbali za mwili wake.

"Baada msafara wa Jakaya (mgombea wa urais wa CCM) kupita, mimi nilikwenda kupanda pikipiki ya Mwenyekiti wangu wa vijana, Kido nikaitwa na (anamtaja jina),” alisema.

Aliongeza: “kwa vile ninamfahamu walikuwa vijana wengi pale, nilipofika wakaanza kunihoji kwa nini nimehudhuria mkutano wa Rais Kikwete na niseme kama ninazikubali sera za CCM,” alisema.
Alisema kuona hivyo aliwapuuza na kutaka kuondoka, ghafla alikabwa na kuangushwa chini na kuanza kupigwa.

Alisema baada ya kuokolewa na wananchi, gari la polisi lilifika na kumchukua hadi kituoni cha polisi alipopewa fomu namba tatu ya matibabu (PF 3) na kupata msaada wa kufikishwa hospitalini hapo.
Alisema wakati huo alikuwa hawezi kutembea baada ya mguu wa kulia kuumizwa vibaya.

Akizungumzia tukio hilo, mgombea ubunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Vicent Nyerere, aliiomba polisi kuchukua hatua dhidi ya watu wanaojihusisha na uhalifu wa aina hiyo.
"Nimelalamika majukwaani kuwa wenzetu wa CCM wanaendesha mafunzo ya kijeshi kwa vijana wao ili kufanya fujo katika uchaguzi, sasa tumeanza kuona matokeo yake, ni vema polisi ikachukua hatua ili uchaguzi huu uwe huru na haki,"alisema.

Mkoani Kilimanjaro, vijana wanaosadikiwa kuwa wafuasi wa chama chaTLP, wanadaiwa kufanya vurugu na kumjeruhi mfuasi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Makale Joseph, mkazi wa Himo mkoani humo.
Tukio hilo lilitokea Septemba 22, mwaka huu, wakati mgombea ubunge katika jimbo la Vunjo kwa tiketi ya TLP, Agustino Mrema, akifungua tawi la chama hicho katika eneo la Njia panda.

Mwenyekiti wa kijiji cha Himo, Hussein Jamal, alisema Joseph alivamiwa na kushambuliwa na wafuasi wa TLP baada ya kutelemka kwenye gari, akiwa ameshika skafu ya CCM.

Jamal alizungumza na NIPASHE katika zahanati ya Koggy iliyopo mji mdogo wa Himo ambapo majeruhi alitibiwa,

“Huyu bwana alikuwa akitokea kwenye shughuli zake, alipofika Njia Panda akatelemka kwenye gari akiwa ameshikilia kitambaa cha CCM, kumbe Mrema alikuwa katika eneo lile akizindua tawi ,ndipo vijana wanaosadikiwa kuwa wa TLP wakaanza kumshambulia,”alisema.

Alisema Mrema amekuwa akifanya mikutano mahala popote kwenye mikusanyiko ya watu, bila kufuata utaratibu wa ratiba, hali inayoyosababisha vurugu kutokana na ukosefu wa ulinzi.
Naye Joseph alisema baada ya kutelemka kutoka kwenye gari alianza kujifuta vumbi kwa kutumia skafu ya CCM, ndipo vijana hao wakamvamia na kuanza kumpiga.

“Walikuja vijana zaidi ya nane wakanivamia na kutaka kunipora kitambaa, baada ya kukataa wakaanza kunipiga ndio matokeo yake wameniumiza kichwani, nimeshonwa nyuzi tatu,”alisema.
Pia aliseka katika vurugu hizo aliporwa simu na fedha taslimu Sh 40,000.
Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Musa Samizi alifika katika zahanati hiyo kumuona majeruhi, lakini hakuwa tayari kuzungumza suala hilo.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kilimanjaro, Lucas Ng’hoboko alisema hana taarifa za tukio hilo.
Hata hivyo alisema matukio ya vurugu za mara kwa mara, yameripotiwa kutokea kwa wafuasi wa CCM na TLP jimboni humo.

Alitoa mfano wa vurugu hizo ni pamoja na wafuasi hao kupigana baada ya kuzuka kwa mvutano baina yao, saa chache kabla ya mgombea urais wa CCM, Jakaya Kikwete kuwasili eneo hilo kwa ajili ya mkutano wa kampeni hivi karibuni.

Vurugu hizo zilitokea baada ya wafuasi wa TLP kupandisha bango kubwa linalomnadi Mrema (Lyatonga) katika lango la kuingilia mjini humo.

Kutokana na hali hiyo, wafuasi wa CCM waliwazuia na kuwalazimisha kulishusha, ndipo vurugu zilipotokea.

Kisiwani Zanzibar, wanachama wawili wa CCM wamejeruhiwa kwa kupigwa mawe katika eneo la Mtoni Unguja, walipokuwa wakitoka katika mkutano wa kampeni uliohutubiwa na mgombea urais wa Zanzibar kupitia chama hicho, Dk. Ali Mohammed Shein.



CHANZO: NIPASHE
 
SIAMINI KAMA YUPO MMOJA WETU ALIE KAMA MIMI ATAWEZA KUFANYA JAMBO ILA PLS WANA JF NIPATIENI MAWASILIANO YA WANA CHADEMA TOP NIWAPE ISHU FULANI NAONA HIYO ITAWASAIDIA SANA,
cONQUEST-CCM HAWANA SERA BALI NI WIZI MTUPU NA SERA YAO KUU MWAKA HUU NI BORA DAMU ITOKE NA KITI TUKALIE
 
Habari nilizozipata kutoka source ya kuaminika zinasema kuwa CCM wameandaa watu wanaotumwa kila jimbo linaloonekana tishio kwao.
Majimbo haya wanawatuma maaskari pamoja na wana CCM watakaovalia nguo za polisi. Hawa wanasambazwa kila jimbo lenye upinzani wa kutisha. Kutakuwepo na vikundi vitakavyofanya vurugu kana kwamba ni wa chama pinzani kisha askari hawa bandia watatumia mwanya wa vurugu hizo kuingia katika vituo " kutoa ulinzi" lakini kwa ajili ya nia ya kuchakachua.
MWENYE SIKIO NA ASIKIE.
CHADEMA NAAMINI TAARIFA WANAZO NA TAFADHALI. WANANCHI WAELEWESHWE NA KILA DALILI INAJIONYESHA KUWA CCM INATAKA KUWAIGA WAKENYA.
USHAURI WANGU KWA KIKWETE. NI AHERI UIACHE NCHI IKIWA NA SIFA YA AMANI NA UTULIVU KULIKO JINA JEMA LIHARIBIKIE MIKONONI MWAKO. MAASKARI WETU MSIKUBALI KUWARUHUSU WANAOVALIA MAVAZI YENU WASIO ASKARI KWELI.
NI WAKATI WA USALAMA WA TAIFA KUAMUA KUWA USALAMA WA TAIFA BADALA YA USALAMA WA KIKWETE AU CCM.
 
Nami pia nimesikia watasababisha vurugu then police watawapigia simu police wawakamate mawakala wote wanaogombana. Hapo ndipo wataingiza kura za siri.
 
CCM wana uchu wa kubaki madarakani usio na kifani. Wamehodhi madaraka miaka yote hii bila kuweza kuleta maendeleo; sasa miaka 5 mingine ya nini?

Rais Kikwete akiachia madaraka bila vurugu, kama walivyofanya Kaunda na Moi, atabaki Rais Mstaafu, na ataheshimika. Kama atataka kuendelea kututawala kwa nguvu, naamini hataweza. Wananchi wamemchoka mno!
 
Kwa sasa chadema wanatakiwa wachangamke wasikubali kuzubaishwa kwa majini ya sheikh yahaya nasikia katuma majini kwa kila kiongozi .Tafadhali litumieni kubwa kuliko majina yote kusamabaratisha ma-pepo mtashinda wote tunasali sana kwa jina mungu baba mueza yote ili tushinde
 
Kwa sasa chadema wanatakiwa wachangamke wasikubali kuzubaishwa kwa majini ya sheikh yahaya nasikia katuma majini kwa kila kiongozi .Tafadhali litumieni kubwa kuliko majina yote kusamabaratisha ma-pepo mtashinda wote tunasali sana kwa jina mungu baba mueza yote ili tushinde

Mbona mdau kama umetoka nje ya mada!
Anyway, CCM wana kila mbinu kuhakikisha wanashinda.
Hilo silishangai.
 
Mbinu ya upinzania sasa iwe ni kuwasahwishi hawa askari waliotumwa waache kutumika kama machine kwani athari na uchunguzi wa umaskini wa Tanzania unawagusa hata wao na familia zao kwani kuiba kura kwao wanaofaidi ni kundi la mafisadi wachache nao wanateseka kuiba kura hali inayoweza kusababisha hata vifo kwao wakati mafisadi kama akina Rostam, Chenge etc yanakula bata na mambo yakiharikika yanawageuka
 
uanjua hawa ccm wanatapatapa...dawa yao na sisi kuendelea na msimamo tu...tunataka mabadiliko...hivyo vyote ni mbio za sakafuni tu..ipo siku...nayo inakuja kama taa ing'arayo ikimulika mafisadi na waovu...watalia na kusaga meno!!
 
Cha msingi ni kuwa watulivu tuu ili wakianzisha fujo mnawachunia watajiona wajinga
 
Back
Top Bottom