mbona huo ni uwazi usiopingika kabisa,siku zote huwa nasema Tendwa ni mwanachama mwaminifu wa ccm, japo anajifanya yuko balanced, ni kimeo kabisa huyu mzee. kwa hakika anastahili kutolewa pale, kawekwa kwa maslahi ya chama kuliko ya taifa. siku zote amekuwa msemaji wa ccm kama vile yeye ni Tambwe Hiza au makamba. sipendi kabisa mwenendo wa kazee haka hakatufai kabisa
hata kuwe na sorce kipindi hiki hatudanganyikikuna source mbadala?
Ahsante kwa kulielewa hilo,Kwamba mwanaharakati wa LHRC alisema jambo na kukataa jina lake kutajwa? Naamini ni uongo mkubwa kuliko ule wa Pinda bungeni kuhusu issue za arusha. Sijamuona mwanaharaka wa LHRC muoga hivyo na aliyepwaya hivyo.
Na hapo ni kama huyo Mwanaharakati ameisoma. Anaogopa nini kutajwa jina kama anaamini anachokisema?
Mikwala ya DOG hiyo hivi kuna mtu anae iogopa Chadema?! Mbona Arusha mlitulia tu na hakuna mlichofanikiwa!
they are all the part of that corrupted system, na kwasasa matumbo yanawawasha sana sijui hata kama wanapata usingiziNimeshangaa sana kauli hii kutoka kwa Tendwa kuchelewa namna hii, biliv me or not isingekuwa hii homa ya maandamano Egypt, Tunisia na sasa Libya ungewasikia woote akina Werema, Makamba, Tambwe singing the same tune!
These guys are just out of time, Out of touch na Hawarekebishiki wala kujirekebisha! wamegota hawajui kinachoendelea wala wanachofanya wao ni kumfurahisha JK tu!
Ndiposa inabidi tuje na tafasiri mpya ya "Mwanaharakati"
Nimepapenda hapo kwenye red, activist tena kutoka LHRC ataki atajwe jina???, ufanywe utafiti labda daily news wamekutana na mfagizi wa LHRC.
Huo ni uongo mtakatifu kabisa, hakuna mwanaharakati yeyote hapo
hiyo habari imepikwa ndani ya ofisi yao
na watakoma mwaka huu maana natumaini hawalali kwa pressure
Kama Tendwa anaheshimu utawala wa sheria kwanini alimuongezea JK muda wa kampeni? Viongozi wetu ni wanafiki sana. Ikifikia kipindi maisha magumu kila kona watu hawataelewa utawala wa sheria.