CHADEMA na siasa za sizitaki mbichi hizi

AUGUSTINO CHIWINGA

JF-Expert Member
Apr 23, 2017
220
689
CHADEMA NA SIASA ZA SIZITAKI MBICHI HIZI

Wenye umri sawa na wangu tutakuwa tunakumbuka hadithi ya mnyama Sungura ambaye aliona ndizi mbivu mtini ,na kila alipojaribu kuzirukia alishindwa na alipochoka akasema ati ndizi zile ni mbichi hazitaki tena.

Kisa hicho ndivyo unavyoweza kukifananisha na msimamo waliouweka Chadema kwamba hawatoshiriki uchaguzi wowote utakaosimamiwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa madai ya kwamba Tume hiyo huwa haiwatangazi wao washindi.

Chadema wameshindwa kuwashawishi wananchi wawachague kutokana na ubovu wa na udhaifu wa chama chao hivyo wameamua kuisingizia Tume ya Uchaguzi kwamba ndiyo inayowabania kupata ushindi katika Chaguzi mbalimbali.

Udhaifu mmoja walionao ni kuelekeza nguvu kubwa kumjadili Rais Magufuli badala ya kupambana na CCM ambayo ni taasisi.
Wao wanajidanganya kwa kumshambulia Mh.Magufuli na kumbatiza majina mabaya ,wananchi wataacha kukichagua Chama Cha Mapinduzi wakati wananchi wanaona kazi nzuri ya kutukuka ya kuleta maendeleo inayofanywa na Mh.Rais Magufuli.
Matokeo yake kila uchaguzi wameangukia pua halafu wanaanza kumtafuta mchawi wakati mchawi ni wao wenyewe.

Chadema haikuundwa kuwa chama cha siasa, hakina misingi na sifa ya kukifanya kiitwe chama cha Siasa na ndio maana inashindwa kupambana na Chama Cha Mapinduzi ambacho kina misingi na sifa timilifu ya kuitwa Chama cha Siasa.

Mtu akiitaja CCM akilini mwake anaona Itikadi ya Ujamaa na Kujitegemea ,anaona viongozi wake wakizunguka huku na huku wakishughulika na shida za wananchi huku wakisisitiza maendeleo lakini ikitajwa Chadema akilini mwake zinamjia picha za jinsi viongozi wake wanavyopinga maendeleo,wakijadili watu badala ya masuala na kutoa kauli mbalimbali za uchochezi.Hivyo hakuna Mwananchi mwenye akili timamu atakayekichagua chama cha namna hiyo asilani abadani.Chama ambacho kimeshindwa kuonesha njia mbadala lazima kishindwe katika uchaguzi.

Kuilaumu Tume ya Uchaguzi ni sababu nyepesi kabisa zinazoweza kutolewa tu na chama ambacho kinaelekea kufa.
Uchaguzi umefanyika katika mazingira ya uwazi na haki, wananchi wamepiga kura kwa uhuru halafu matokeo yamekuja kinyume na walivyotegemea wanalaumu tume.
Chadema wanatafuta kichaka cha kujicha baada ya kuzidiwa hoja na sera makini na Chama Cha Mapinduzi jukwaani.

Kuitupia lawama Tume ya uchaguzi ni kufilisika kisiasa ni sawa sawa na yule Sungura aliyesema sizitaki mbichi hizi baada ya kushindwa kuzifikia ndizi, kwani ni tume hiyohiyo ndio ilimtangaza Mbowe kuwa Mbunge wa Hai ,Peter Msigwa kuwa Mbunge wa Iringa mjini ,God bless Lema Kuwa Mbunge wa Arusha Mjini na wabunge wengineo na madiwani kadhaa.
Sasa iweje leo waje kuilaumu baada ya kushindwa kufurukuta katika sanduku la kura.
Tatizo Chadema wanaingia katika uchaguzi wakiwa na matokeo yao tayari mfukoni na wakishashindwa tu basi huwa wanaokoteza vijisababu vya kuwaaminisha wafuasi wao kwamba hawajatendewa haki.Hii sio sahihi kabisa Chadema isijifanye kwamba ina hatimiliki ya kushinda kila Chaguzi.

Uchaguzi ni mchakato wa Kidemokrasia kuna kupata na kukosa na ukikosa mpongeze yule aliyepata kisha ujipange upya na sio kuanza kutupa lawama maana yake unatuambia kuwa wewe bado hujakomaa kisiasa.

CCM inashinda kutokana na mageuzi makubwa iliyoyafanya wananachi sasa wameongeza imani kwa CCM Mpya na sio kwa kubebwa na Tume ya uchaguzi au chombo chochote cha Dola.

Augustino Chiwinga.
Dar Es Salaam,
0659438889
 
Da! Unatisha.Mpaka namba ya simu.
 
Back
Top Bottom