Vancomycin
Senior Member
- Jan 7, 2011
- 171
- 111
Katika kudhihirisha kuwa CHADEMA ni chama makini na ni chama ambacho kina sera zenye mashiko serikali ya CCM imekuwa inaendeleza utekelezaji wa sera za chama hicho ambazo mgombea wake wa urais Dr.W Slaa alikuwa akizinadi katika kampeni zake za kugombea urais.
1.Dr.Slaa katika kampeni zake alieleza adhma yake ya kuunda baraza dogo lenye tija ambapo CCM imetekeleza hilo kwa kiasi chake kwa kupunguza ukubwa wa bara hilo
2.Katika ilani ya uchaguzi ya chadema ilieleza bayana mpango wake wa kubadili katiba mbali ya kuwa hoja hii ni ya muda mrefu na mgombea wake kukosa urais wabunge wake waligomea hotuba ya rais mbali ya kejeli na matusi waliyopata walisimamia kile walichoamini CCM inatekeleza hilo kwa kuanzisha mchakato wa katiba mpya ambayo kila mtu anaifurahia.
3.Leo UVCCM wamekuja na jingine la kuvunjwa kwa bodi ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu na kuunda bodi ya mikopo yenye tija jambo ambalo limezungumzwa kwenye ilani ya uchaguzi ya CHADEMA 2010.
Kwa hayo machache hapo juu hii inadhihirisha sera nzuri za CHADEMA na ukomo wa uwezo wa kufikiri na kubuni kwa viongozi wa CCM na kukopa sera za wapinzani.Pengine tutarajie mengine mengi.