Kibunango
Platinum Member
- Aug 29, 2006
- 8,420
- 2,271
2008-11-10 13:48:03
Na Mashaka Mgeta
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimezidi kukitesa Chama Cha Mapinduzi (CCM), baada ya kuwachukua wanachama wake kadhaa ambao ni wafanyabiashara maarufu wa wilayani Tarime, Mkoa wa Mara wanaoishi jijini Dar es Salaam.
Kuhama kwa wafanyabiashara hao, kumefanyika wakati kampeni ya operesheni sangara, ikipangwa kuendelea kwenye mikoa ya Kanda ya Ziwa Victoria.
Hatua hiyo ilifikiwa juzi jioni, katika hafla iliyoandaliwa nyumbani kwa mmoja wa matajiri hao, Chacha Kigula, Mikocheni na kuhudhuriwa na watu mbalimbali, akiwemo Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Mbunge mpya wa Tarime, Charles Mwera.
Awali, hafla hiyo ilitangazwa kuwa mahususi kwa ajili ya kumpongeza Mwera, ambaye pamoja na Diwani wa kata ya Tarime Mjini (Chadema), John Heche, walishinda katika uchaguzi mdogo uliofanyika jimboni Tarime Oktoba 12, mwaka huu.
Katika hafla hiyo, pamoja na Kigula, wafanyabiashara matajiri wengine waliojitokeza hadharani na kuchukua kadi za Chadema walizokabidhiwa na Mbowe, ni Mosama Mwita na James Binagi.
``Wapo waliochukua kadi lakini hawakupenda majina yao kujulikana, kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo usalama mahali pa kazi,`` alisema msemaji wa Chadema wilayani Tarime, Chacha Daniel Okong`o.
Okong`o, alisema watu wengine zaidi ya 20 wa kada tofauti, waliokuwa miongoni mwa washiriki katika hafla hiyo, walijiondoa katika vyama vyao na kujiunga Chadema.
Akizungumza na Nipashe, Mwita alisema walifikia uamuzi wa kuachana na CCM ili kukidhi mwelekeo wa siasa na mwitikio wa wananchi wa Wilaya ya Tarime.
Aidha, Mwita alisema tukio hilo ni sehemu ya ishara ya kuonyesha msimamo wa dhahiri kisiasa uliopo kwa wananchi wa Tarime.
``Sisi tulichangia kuwahamasisha vijana kutambua na kutetea haki zao, sasa tusingeeleweka kama tungeamua kuwa nje,`` alisema.
Naye Kigula, aliwaambia washiriki wa hafla hiyo kwamba CCM imeelekea kupoteza mwelekeo katika uongozi, hivyo njia pekee ni kupata chama mbadala kitakachochukua dhamana hiyo.
``Kama ningekuwa bado kijana kama wewe Mbowe, ninaamini kwamba ingekuwa rahisi sana kuichukua nchi hii, CCM wameshindwa kuongoza,`` alisema.
Kigula alisema viongozi na wabunge wa CCM, wameshindwa kutambua vipaumbele vya mahitaji na maendeleo ya wananchi, badala yake wanajihusisha na mambo yasiyoleta tija kwa umma.
Alitoa mfano kuwa, baadhi yao wanapopata uongozi, wanafikiria kujiimarisha madarakani kwa njia za kishirikina, hali inayowafanya waelekeze rasilimali na mbinu zao katika eneo hilo badala ya kuwafikiria wananchi waliowachagua.
Mbowe alisema kujiunga kwa wafanyabiashara hao, kutachochea ari ya mageuzi kwa wananchi ndani na nje ya Tarime.
Alisema hivi sasa Tarime ni eneo linalotolewa mfano wa kuigwa kwa jamii inayohitaji mageuzi ya kweli ndani na nje ya Tanzania.
Hata hivyo, alitahadharisha kuwa hatua ya watu kukihama chama kimoja na kujiunga katika chama kingine, isichukuliwe kama asili ya uhasama unaoweza kusababisha chuki miongoni mwa wananchi.
``Leo hii mmeiona CCM haiwafai, mmejiunga Chadema, hilo ni jambo jema kwa maana vyama vinatakiwa kujenga mazingira ya kukubalika kwa wananchi, kitu ambacho kinatukabili hata sisi huku Chadema,`` alisema Mbowe.
Wakati huo huo, taarifa zilizopatiakana jana kutoka Makao Makuu ya Chadema zilieleza kuwa operesheni sangara iliyoanza baada ya uchaguzi mdogo wa Tarime, inaendelea wiki hii mkoani Mwanza.
SOURCE: NIPASHE