Kati ya Vijana SHUJAA,MAHIRI na MAKINI katika mambo ya SIASA tulioweza kuwashuhudia katika uchaguzi wa Urais,Ubunge na Madiwani mwaka 2010 nchini Tanzania Amani Mwaipaja ni mmoja wapo. Kijana huyu aligombea Ubunge Jimbo la MOrogoro Mjini kwa Tiketi ya CHADEMA na kushika nafasi ya pili akimwacha Mgombea wa CUF Abeid Mlapakolo katika nafasi ya Tatu.
Nimejaribu kufuatilia historia yake ingawa haifahamiki kwa wengi lakini Amani Mwaipaja ana digrii ya sheria ya chuo kikuu Mzumbe, mratibu wa miradi mbalimbali ya Kijamii na ni mwanaharakati wa haki za Binadamu.
Kwa wananchi wa Morogoro wengi walikuwa hawamfahamu mpaka pale alipogombea Ubunge na kuonesha kiwango kikubwa sana alipokuwa jukwaani kipindi cha Kampeni, kusema ukweli, kwa siasa sa Morogoro Kijana huyu aliionesha ushindani mkubwa sana ingawa inawezekana hakupata sapoti kubwa kutokana na kuwa mgeni machoni pa wengi au kushindwa kufika maeneo mengi wakati wa kampeni kutokana na changamaoto ya fedha lakini ni potential sana huyu kijana
Nimekuwa pia nikufuatilia makala zake kwenye magazeti ya mwanahalisi na magazeti mbalimbali na kugundua kuwa ana uwezo mkubwa katika kufikiri isipokuwa hatumiki sawasawa kwa mfano, Amani Mwaipaja amekuwa akiendesha semina mbalimbali kwa jamii na vyuo na hata anaposhiriki katika mikutano ya Hadhara bado naonesha umahiri mkubwa sana wa kushawishi watu isipokuwa hatumiki sawasawa
Nakumbuka lile sakata la maaskari wanaoshirikiana na majambazi mkoani Morogoro huyu ndiye aliyekuwa mstari wa mbele katika kuandaa nyaraka mbalimbali akimsaidia askari jeshi aliyeamua kuweka uozo wa jeshi la Polisi Morogoro Hadharani ajulikanaye kwa jina la Dunga au afande Donald.
Sakata la afande Donald ndilo lililopekea akina SABA SITA NA WENZAKE kuhamishwa Morogoro (Source:Waraka uliosambazwa na Afande Donald kwa wananchi-Morogoro). Hiyo ni kazi ya Amani Mwaipaja ambaye hakuogopa vitisho vya akina Sabasita,alisimama kidete na tunaambiwa hata IGP Mwema alipounda Tume ya kuchunguza madai ya askari huyo alisindikizwa na Amani Mwaipaja akiwa kama mwanasheria mshauri.
Juzijuzi Amani Mwaipaja ametajwa tena na Afande Sele alipokuwa akihojiwa na Clouds Radio kuwa ndiye aliyekuwa mtu wa kwanza kumsaidia mwanzo mpaka mwisho pale Afande Sele na Twenty Percent walipokuwa Rumande,watanzania wote walisikia.
Amani Mwaipaja huyu wiki chache zilizopita ameonekana kwenye Runinga mbalimbali ikiwemo ITV na TBC akitoa maoni kuhusu mabadiliko ya Baraza la Mawaziri.
USHAURI wangu kwa CHADEMA Ni kwamba:
Iandae utaratibu wa namna ya kuwapangia majukumu hawa vijana wanaoonekana kuwa potential katika Chama badala ya kuwatumia wale tu ambao tayari ni wabunge au wana nafasi fulani makao makuu,
Kwa mkoa kama wa Morogoro ambao unahitaji nguvu ya ziada katika kuhamasisha na kujenga chama ISIACHE kuwatumia vijana kama hawa
Mzalendo: Chuo Kikuu Sokoine-Morogoro