CHADEMA kutoa msimamo mzito leo; Ni baada ya rais kusaini muswada wa upatikanaji wa katiba mpya

After Chadema's apparent failure to dissuade JK from endorsing the controversial Constitution Bill, people's faith in the party's elite has eventually started to shrink. Everyone was made to believe that Chadema delegation was capable of preventing the Bill from being signed but the outcome was disappointing. That Chadema has failed to take an advantage of a rare Presidential meeting to convince him not approve the Bill means that its leaders do not have postulated abilities necessary for a political leader.

Baada ya mwaka huu utakuwa mwita 26
Hongera sana
 
Kuna watu wanashangilia furaha ya leo rais kusaini bila kutafakari madhara yake miaka 10 ijayo, tena haya madhara yatakuja kuirudi CCM yenyewe. But what is needed ni kusonga mbele na watu hawa hata nchi iwe nzuri kiasi gani huwa hawakosekani tumejionea Libya mtu analipiwa hadi kodi ya nyumba lakini still wameona hayo hayatoshi. Chadema tenda wema usingoje shukrani ya wachache ama wengi hamuwezi kupongezwa na wote.

Huku ni kujifariji na kujiliwaza hakuna kitu, katiba ni mali ya watanzania sio mali ya Chadema..

Kama mmetoka bungeni wakati wa vikao halafu mnakimbilia ikulu kuonana na rais msiomtambua mnapa mapendekezo yenu sijui mnategemea nini
 
Mkuu Waberayo me nadhani ungeweka hoja hapa ya ushauri wako kwa chadema kuliko kutoka povu kwa hasira! Je unatakaje? waungane na Cuf,tlp na ccm kupinga au waungane na jukwaa la katiba kuomboleza siku 9? Hebu tusubili hilo Tamko la cdm later then tujadili.
Wanashangilia bila kujua wanachoshangilia ni upuuzi ukiwauliza sababu wanasema rais kasaini na Chadema walienda kunywa chai, it is riduculous indeed tukiambiwa watanzania ni wajinga tutabisha sana na mapovu juu.
 
Huo msimamo mlishindwa kuutoa mlipoenda ikulu mnataka muutoe leo. Hatutaki ngonjera zenu hapa za maandamano. Watu mmepewa heshima ya kuongea na Mkulu Ikulu mkaishia kukenua meno na kushangaa tausi wake tu. Mnataka mpewe nafasi gani zaidi ya hiyo?

hapa ndo naona pengo la Dr.kutokuwepo Ikulu siku ya makubaliano!
 
Jamani, tujipange na mapendekezo yetu kwa hatua inayofuata. Uundwaji wa TUME. Haya mengine tusubiri Bunge lijalo la January.
 
Wanashangilia bila kujua wanachoshangilia ni upuuzi ukiwauliza sababu wanasema rais kasaini na Chadema walienda kunywa chai, it is riduculous indeed tukiambiwa watanzania ni wajinga tutabisha sana na mapovu juu.

Huo ndio ukweli Chadema walikwenda kunywa chai ikulu..

Kwa nini sasa wanataka kutoa tamko la nini?
 
Huku ni kujifariji na kujiliwaza hakuna kitu, katiba ni mali ya watanzania sio mali ya Chadema..

Kama mmetoka bungeni wakati wa vikao halafu mnakimbilia ikulu kuonana na rais msiomtambua mnapa mapendekezo yenu sijui mnategemea nini
Hata Nape mmemponza kwa njia hii hii ya kushangilia komenti zake za kipuuzi, leo mmemkimbia hatuoni mkiongelea kwisha habari yake kaiacha Chadema, hata hili la katiba siku likimgeuka aliyesaini ambaye ni hero leo mtakimbia kwa sababu mko kwa ajili ya komenti ya siku husika mfurahishane hamkomenti huku mkifikiria kuna kesho kujibu.
 
Mimi nawapongeza CDM. Wamejaribu kufuata njia ya mazungumzo. Si ndio tunasisitiza kila siku? Watu wamalize njia zote za mazungumzo, ikishindikana kisago ndio njia pekee inayobaki. Kwa hiyo CDM hongereni sana. Mmedhihirisha hakuna Afrika katiba ya wananchi mpaka tuchinjane kwanza kama ilivyokuwa Rwanda na Kenya. Na hii itakuja tu, hata kama sote tulio hai leo tutakuwa tumekufa. Vizazi vyetu vijavyo watachapana tu ndio waheshimiane.

Mkuu nakuunga mkono. CDM wamekwepa propaganda za CCM kwamba ni chama cha fujo tu. Wame initiate kumwona Rais kumweleza namna ambavyo hawaridhiki na huo mswada na mchakato wake, sasa kama Rais atawapuuza ndipo sasa suala linakwena kwenye mahakama ya wananchi. Hilo ni bao ambalo CDM wamemfunga JK na CCM yake.

Toeni tanko nasi wazalendo wa kweli tuko tayari kusikia na kutekeleza. Hatimaye nchi ni lazima iufikie ukombozi wa kweli.

SAA YA UKOMBOZI NI SASA
 
viongozi wa cdm walikuwa sahihi kuonana na rais kumpa yaliyo mioyoni mwao, ni uamuzi wake sasa yeye km rais wa nchi sio wa ccm ameamua kusuka au kunyoa...cdm wametimiza wajibu wao wa kutoa maoni na kuwatetea watanzania wanyonge.
 
nawaona chadema kama wale watz wanaoishi kule marekani,
waliosema tunaandamana kumbe ni njaa tu,
mbowe aseme kilichompeleka huko ikulu ni kitu gani,
na kilichomkimbiza kule mjengoni ni kitu gani.
 
"The only man who makes no mistake is the man who never does anything. do not afraid of mistakes providing you do not make the same one twice"

CDM mmethubutu kufanya mengi sana mazuri na bado tuna imani sana na nyie, lkn kila binadam anayeishi na anyejishughulisha na jambo lolote huwa anakosea mahali fulani. This time mlikosea kumwamini JK na chama chake kwamba atawasikilizeni. Kwa kumbukumbu zangu hili ndo kosa lenu la kwanza la namna hii (i stand to be corrected).

Ombeni radhi kwa kutuficha ficha kuhusu huo mwafaka na tuambieni ukweli wa kila kitu mlichoongea ikulu na JK ili mrudishe imani kwa wananchi ambao kwa takribani siku 2 sasa wamekuwa gizani. Msipofanya hivo magamba watazidi kutumia mavyombo yetu ya habari ambayo mengi yameshannunuliwa kuposha umma wa tz. Stand up, dust yourselves off and let us go on all the way.

Peeeoooplez Pooooooooweeeeer!!!!!!
 
Back
Top Bottom