CHADEMA kutoa msimamo mzito leo; Ni baada ya rais kusaini muswada wa upatikanaji wa katiba mpya

Chadema sasa mnataka kutoa msimamo gani tena wakati juzi mmekutana na rais ikulu mkanywa chai pamoja mkampa mapendekezo yenu!

Mapendekezo yamefanyiwa kazi? au hoja zimejibiwa kwa mantiki?
 
Mimi nawapongeza CDM. Wamejaribu kufuata njia ya mazungumzo. Si ndio tunasisitiza kila siku? Watu wamalize njia zote za mazungumzo, ikishindikana kisago ndio njia pekee inayobaki. Kwa hiyo CDM hongereni sana. Mmedhihirisha hakuna Afrika katiba ya wananchi mpaka tuchinjane kwanza kama ilivyokuwa Rwanda na Kenya. Na hii itakuja tu, hata kama sote tulio hai leo tutakuwa tumekufa. Vizazi vyetu vijavyo watachapana tu ndio waheshimiane.
Nyie ndio mtakuwa wa kwanza kukimbilia Ulaya kama wakimbizi.

Na kwa akili yako hao watakao uana ni kina nani na nani?
 
After Chadema's apparent failure to dissuade JK from endorsing the controversial Constitution Bill, people's faith in the party's elite has eventually started to shrink. Everyone was made to believe that Chadema delegation was capable of preventing the Bill from being signed but the outcome was disappointing. That Chadema has failed to take an advantage of a rare Presidential meeting to convince him not approve the Bill means that its leaders do not have postulated abilities necessary for a political leader.
If it is controversial? so what are your suggestions, watu mnashangaa mlitaka Chadema wamshikie bunduki rais asisaini they have played their part so play yours as mwananchi, are these jokes stands for your part?
 
Ni kweli kabisa CHADEMA have played their role, wasingeweza kumshikia bunduki Rais Kikwete akubalie mapendekezo on the spot, jamani. Kuna mambo mengi sana hapo, great thinkres hamuwezi kuona mbali?
 
Nyie ndio mtakuwa wa kwanza kukimbilia Ulaya kama wakimbizi.

Na kwa akili yako hao watakao uana ni kina nani na nani?
Tatizo ni kufikiria kila siku ni leo. Ndio tatizo la viongozi wetu na baadhi yetu. Tumekuwa wachoyo sana kufikiria vizazi vyetu vijavyo kiasi kwamba 'we do not care anymore'! Sawa tunayo haki ya kufanya hivyo ila historia itatuhukumu.
 
wengi waliochangia kwa kuwaponda chedema na kumshangilia JK nimewashangaa sana tena sana, ni muhimu kutumia hekima kwa haya mambo yanayotuhusu na kutulenga kila mmoja wetu, hiyo sheria iliyopitishwa itatunyonya wote na kutukandamiza zaidi kiuchumi na tutabaki maskini kila siku! tena tutazidi kuwa walalahoi wakati watu wachache sana wakinufaika kimaisha. mimi sina chama chochote ila napenda kuwashauri wenzangu tuwe makini maana inatulenga kila mmoja,Chadema imefanya sehemu yake katika jitihada za kusaidia sheria irekebishwe ili kumnufaisha mwananchi ambae ni mimi na wewe, leo hii mtu anaongea vibaya na kushangilia kile kinachofanywa. natamani sana mngejua tunakoelekea ni kubaya zaidi, msingenena mliyonena wale mnaoshangilia, kaeni chini na kutafakari,yatakuwaje maisha yenu,watoto wenu na hata wajukuu zenu. ndio Tanzania tunayoitaka hiyo??? tujadili kihekima zaidi.
 
Wanataka kuja na tamko gani tena?kwamba kikwete kavunja makubaliano ya MUAFAKA!!
 
Ukweli ni kuwa sijaelewa muafaka wao katika mikutano ya mwanzo wa wiki hii!!!

Walikubaliana au walikubaliana kutokukubaliana!!! THis really confuses me!! Arrrrrh!!!
 
Hakuna ushauri ambao CDM huwa wanauchukua toka kwa wanachama wake...in other words CDM haina tofauti na Kikwete wa CCM!! kila kitu usanii.....ona sasa aibu hii!

Mkuu Waberayo me nadhani ungeweka hoja hapa ya ushauri wako kwa chadema kuliko kutoka povu kwa hasira! Je unatakaje? waungane na Cuf,tlp na ccm kupinga au waungane na jukwaa la katiba kuomboleza siku 9? Hebu tusubili hilo Tamko la cdm later then tujadili.
 
chadema walienda kumshauri kikwete kutosaini na hawakwenda kumlazimisha kutosaini so but maamuzi ya kusain au kutosain yalikua mikononi mwa kikwete. Tamko la nini tena kama kweli hawamwogopi Kikwete wangempa condion kwamba ukisain tutatoa tamko, hawana chochete walibaki kushangaa shangaa ikulu mwisho wakasahau kilichowapeleka.
kama kweli wanamsimamo wangempiga bit JK ili asisain.

kazi kweli.
 
After Chadema's apparent failure to dissuade JK from endorsing the controversial Constitution Bill, people's faith in the party's elite has eventually started to shrink. Everyone was made to believe that Chadema delegation was capable of preventing the Bill from being signed but the outcome was disappointing. That Chadema has failed to take an advantage of a rare Presidential meeting to convince him not approve the Bill means that its leaders do not have postulated abilities necessary for a political leader.
kaka unatutisha na misimamo yako ya kuyumbayumba...unakuwa kama 'Cameron' anayekula na kuliwa papohapo...! Haya bana...naona Nape amekushikilia kwenye ukuta kwelikweli!
 
Habari zenu wana JF;

Chama cha Demokrasia na Maendeleo leo tarehe 30/11/2011 kinatarajia kutoa msimamo mzito baada ya Rais kusaini muswada wa upatikanaji wa katiba mpya.

M/kiti wa CDM Mbowe "Tulimuomba Rais Kikwete asisaini muswada huu mpaka makubaliano yetu yatekelezwe"

Kaimu Katibu mkuu wa CDM, Mnyika "Chama kitatoa msimamo mzito leo, tulimshauri Raisi Kikwete asisaini muswada huu mpaka kwanza tuliyokubaliana yatimizwe"

Wakuu mwenye taharifa zaidi atujuze.

Nawasilisha.

mmefanikiwa kuweka kumbukumbu sahihi. hongereni kama ni kweli
 
wengi waliochangia kwa kuwaponda chedema na kumshangilia JK nimewashangaa sana tena sana, ni muhimu kutumia hekima kwa haya mambo yanayotuhusu na kutulenga kila mmoja wetu, hiyo sheria iliyopitishwa itatunyonya wote na kutukandamiza zaidi kiuchumi na tutabaki maskini kila siku! tena tutazidi kuwa walalahoi wakati watu wachache sana wakinufaika kimaisha. mimi sina chama chochote ila napenda kuwashauri wenzangu tuwe makini maana inatulenga kila mmoja,Chadema imefanya sehemu yake katika jitihada za kusaidia sheria irekebishwe ili kumnufaisha mwananchi ambae ni mimi na wewe, leo hii mtu anaongea vibaya na kushangilia kile kinachofanywa. natamani sana mngejua tunakoelekea ni kubaya zaidi, msingenena mliyonena wale mnaoshangilia, kaeni chini na kutafakari,yatakuwaje maisha yenu,watoto wenu na hata wajukuu zenu. ndio Tanzania tunayoitaka hiyo??? tujadili kihekima zaidi.
Kuna watu wanashangilia furaha ya leo rais kusaini bila kutafakari madhara yake miaka 10 ijayo, tena haya madhara yatakuja kuirudi CCM yenyewe. But what is needed ni kusonga mbele na watu hawa hata nchi iwe nzuri kiasi gani huwa hawakosekani tumejionea Libya mtu analipiwa hadi kodi ya nyumba lakini still wameona hayo hayatoshi. Chadema tenda wema usingoje shukrani ya wachache ama wengi hamuwezi kupongezwa na wote.
 
kaka unatutisha na misimamo yako ya kuyumbayumba...unakuwa kama 'Cameron' anayekula na kuliwa papohapo...! Haya bana...naona Nape amekushikilia kwenye ukuta kwelikweli!

Huwezi kutumia lugha za kiungwana mpaka utumie lugha za matusi ndio tukuone mjanja?
 
CHADEMA si walifanya majadiliano ni siri yao na hawataki kutueleza yaliyojiri?!!!
Sasa kuna haja gani ya kutuambia kuwa walikubaliana Rais asisagn mswada kuwa sheria? Waendelee na usiri wao na sisi sasa hatuamini kama wanachokisema sasa ni ukweli kwa sababu tulipowauliza wamejadiliana nini huko Ikulu walikataa kutuambia details. Sasa hatutaki details, tunafuatilia yanayojiri tu...
 
kaka unatutisha na misimamo yako ya kuyumbayumba...unakuwa kama 'Cameron' anayekula na kuliwa papohapo...! Haya bana...naona Nape amekushikilia kwenye ukuta kwelikweli!

as a supporter of chadema, hata hao viongozi nao hawana msimamo... i think nchi nzima haina msimamo
 
Napenda kuchukua nafasi hii kwa niaba ya watz wengi wapenda mabadiliko chanya, maendeleo na wazalendo wa kweli.

Kwanza niwapongeze sana viongozi na wabunge wa CHADEMA kwa kuibua na kulaani mambo mengi maovu ambayo yamekuwa yakifanywa na viongozi wa serikali ya CCM. Vile vile mmekuwa mstari wa mbele ktk kutetea haki za wananchi wanyonge na maskini wa nchi hii. Sidhani kama nina haja ya kuandika hapa harakati na jitahada zenu dhidi ya mapambano ya ufisadi na ukombozi wa taifa letu ambolo mpaka sasa liko mikoni mwa watu wachache wanaotuibia na walio juu ya sheria. Wafuatiliaji wote wa mustakabali wa hali ya siasa ya taifa wanajua na kiasi gani mnapambana.

Mmekuwa mwiba na sifingo kali sana kwa chama tawala kwa muda sasa. Lakini siku zote CCM imekuwa ikitumia mbinu mbalimbali za kuwaneutralize kama ilivofanikiwa kwa CUF hata hivo hamkonekana kutetereka hata kidogo. Watanzania wengi waliokosa matumaini na kukata tamaa, wanyonge, maskini, ambao wameporwa haki zao; wanaona nyie ndo tumanini jipya, nguvu mpya, wanaamini kupitia CDM iko siku haki zao zitarudi na misingi bora ya usawa ktk elimu, kazi, biashara na uongozi itarejeshwa ndani ya nchi yetu. Hiyo ilijidhihirisha baada ya matokeo ya uchaguzi uliopita, pamoja na hila zote za tume ya uchaguzi, polisi na usalama wa taifa lkn bado mliweza kuwaburuza CCM wakasahau kile walichozoea kuita "ushindi wa kishindo".

Wakati wa kampeni zenu kuelekea uchaguzi mkuu 2010 moja ya ilani yenu ilikuwa ni kuanza mchakato wa kuandaa katiba mpya ndani ya siku 100 kama mngepata ridhaa ya wananchi ya kuongoza nchi. Kwa hila na njama kali sana kura za CDM hazikutosha, CCM kupitia rais wakawapora agenda yenu ya katiba. Kilichotokea toka siku JK anatangaza nia ya kuandika katiba mpya mpaka juzi mlivosusia mjadala wa muswada wa sheria ya kuandika katiba na kuomba kuonana na rais, kila mtu anajua. Macho na masikio ya wengi yalikuwa yakisubiri nini kitajiri baada ya CDM kukutana na JK. Tuliyoyaona na kusikia ni kinyume kabisa na matarajio ya wengi. Kwa ufupi tu, kumekuwa na maoni na mitazamo tofauti kwa kile kilichodaiwa ni muafaka uliyofikiwa baina ya CCM na CDM. Mbaya zaidi tunaambiwa rais tayari ameshasaini huo muswada kuwa sheria. Watu wanataka kujua kiundani;

1. Muafaka gani huo uliofikiwa baina ya CCM na CDM? Ni mapendekezo gani mliyopeleka, yapi yamekubaliwa na yapi yamekataliwa? Msimamo wa CDM ni nn iwapo mapendekezo yenu yaliyokubaliwa hayatatekelezwa?

2. Rais sasa ameshaini; nafasi ya wananchi iko wapi katika maboresho ya hiyo sheria kabla machakato wa kuandika katiba haujaanza? Na hivi ndivo mlivokuabaliana, kwamba asaini halafu michango ya wananchi itaendelea kupokelewa kuboresha sheria hiyo? Huu ni usanii!

Sitaki kuamini kwamba mliridhia haya na hamkujua hila za CCM. Nahisi kuna upotoshaji fulani toka kurugenzi ya mawasiliano ikulu kuhusu the so called "mwafaka". CCM sio wa kufanya nao muafaka wowote ,itisheni maandamano tuingie barabarani kieleweke. Narudia tena..hamna muafaka na dudu linaloitwa CCM a.k.a chama cha mafisadi, magamba, majambazi, majizi, mafedhuli.

Please CDM come out itisheni press conference mtueleze haya; vinginevyo hisia zilizotawala vichwani mwa watu sasa ni kwamba, CCM ameshatoa posa kwa mke pili ndoa itafungwa hivi karibuni. Binafsi sitaki kufikiria hivo bado nina imani na CDM, lakini bila majibu ya maswali haya mtatuacha njia panda tukijiuliza kama huu ndio mwisho wa CDM kama CUF.

Nawasilisha!!!
 
CCm na serikali yake wameamua kuupuza umma wa watanzania ktk swala muhimu la kuandika katiba huru na yenye kukidhi matakwa ya watanzania. Nia na matarajio yao ni kwamba waendelee kushika hatamu za Uongozi wa Taifa hili. Inajulikana kuwa ushindi wowote wa CCM ktk chaguzi zinazoshirikisha vyama vingine vya kisiasa umekuwa ukutokana na Ubovu wa katiba kandamizi tuliyonayo sasa. CCM wanajua kabisa wakiachia kuundwa katiba mpya katika misingi ya matarajio ya watanzania basi ni mwisho wao wa uongozi ktk taifa hili. Lakini sasa basi ningependa kuwashauri CHADEMA na wanaharakati kuwa walichokifanya ktk kunusuru lolote linaloweza kutoea imetosha na sasa wawe wapole muda utafika na ni Imani yangu kuwa matarajio ya CCM na serikali yake hayatatimia kamwe. Iwapo katiba mpya itaundwa kwa mfumo uliojitokeza kwa sasa itakuwa ni katiba ya rais na CCm yake na sio katiba ya wananchi ( watanzania).
Lakini habari njema ni kwamba CCM uchaguzi 2015 iwe ni chini ya katiba hii au mpya watakayochakachua ni kwamba kitakuwa chama cha upinzani tu.
Asilimia 80% ya watanganyika wamechoka chini ya CCM na wanataka mabadiliko kwa kila namna.

2015 CCM NI CHAMA CHA UPINZANI TENA CHINI YA KATIBA ITAKAYOWAUMIZA HATA WENYEWE WALIOICHAKACHUA.
 
Back
Top Bottom