CHADEMA KUFUNGUA KESI MAHAKAMANI KUPINGA UCHAGUZI WA UMEYA ARUSHA. (Mbunge apingwa)

jamani ccm inatapatapa, mwisho wake ndio umewadia wanajaribu kutumia njia mbadala kulazimisha kubaki madarakani baada ya ushawishi wa kisera kushindwa, hali hiyo ndio imetokea ktk majimbo mengi ya uchaguzi. sasa hiyo idadi ya madiwani ambao ndio huchagua meya ipo bayana kwa kuwa ni ndogo vinginevyo wangeongeza idadi hadi watoshe, na kwa kuwa haiwezekani ikabidi wapige kura kinyemela. tusikubali.
 
i won't be suprized if that case is take the whole 5 years serving term meant for CHADEMA. Mbayuwayu style in the makings...
 
UCHAGUZI wa Meya na Naibu wa Manispaa ya Arusha umechukua sura mpya baada ya kuibuka vurugu zilizosababisha Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema, kukamatwa na Jeshi la Polisi na kupigwa hadi kupoteza fahamu na kulazwa katika Hospili ya mkoa huo Mount Meru.Vurugu hizo zilizodumu kwa takribani saa sita, zilisababisha askari wa Kikosi cha Kuzuia Ghasia(FFU) kutumia mabomu ya machozi pamoja na maji ya kuwasha kuwatawanya maelfu ya wafuasi na wapenzi wa Chadema waliokuwa wamezingira ofisi za Manispaa hiyo na kufunga kwa muda Barabara ya Mkuu wa Mkoa na ya New Arusha Hotel.

Wanavuna matunda ya kuwa na misimamo ya ukigeugeu. Unafiki ndio ulio wajaa acha waonje joto ya jiwe na hiyo ni mwanzo tu.




Jitambue, Jithamini. Kumbuka kuwa kuna wakati wa kuzaliwa na wakati wa kufa, kuna wakati wa kucheka na wakati wa kulia, kuna wakati wa kupanda na wakati wa kushuka.
 
Penye haki hata ungepindisha sheria vipi, bado utaishia kuumbuka tu. Tanzania ya sasa si ya kutishiana na kunyanyasa wenye haki. Pole sa LEMA ila wewe ndio mkombozi na mpiganaji hodari hupitia magumu kwa muda wa kipindi cha mpito. Tunakuombea upone haraka na uendeleze mapambano, kwani mi naona ndo wamechokoza nyuki. Ccm ni adui wakubwa wa watz wote, tuungane kuwang'oa hata kabla ya 2015 and then tuwawajibishe hilo linawezekana chini ya jua.
 
Jamani! Hivi kweli kulikua na umuhimu wa Polisi kutumia nguvu kiasi hicho???!! Thats totaly Police brutality!! Hivi tutaonewa hivi mpaka lini???!! Mapaka lini jamani???!!
 
Hapa kilichobaki ni vijana wa Arusha kulishughulikia hili swala. Hawwezi kushindana na wananchi kama wananchi wanataka kuongozwa na chadema hawawezi kuwalazimisha kuongozwa na chama cha majambazi. Lema tumia vijana kufanya kazi mpaka kieleweke. Tusikubali kuendelea kugandamizwa namna hii . Haya ni mambo ya mwaka 47 si ya Tanzania ya leo. Mimi sioni hata sababu ya kwenda mahakamani maana mtakuwa mnawapa vichwa bure , hapa ni nguvu ya umma itumike mpaka kieleweke. Naomba mbowe atoe tamko jambo hili lishughulikiwe kwa nguvu ya umma na si mahakama. kwenda mahakamani ni kuwapa ujiko tu hawa mbuX2.
 
Hapa kilichobaki ni vijana wa Arusha kulishughulikia hili swala. Hawwezi kushindana na wananchi kama wananchi wanataka kuongozwa na chadema hawawezi kuwalazimisha kuongozwa na chama cha majambazi. Lema tumia vijana kufanya kazi mpaka kieleweke. Tusikubali kuendelea kugandamizwa namna hii . Haya ni mambo ya mwaka 47 si ya Tanzania ya leo. Mimi sioni hata sababu ya kwenda mahakamani maana mtakuwa mnawapa vichwa bure , hapa ni nguvu ya umma itumike mpaka kieleweke. Naomba mbowe atoe tamko jambo hili lishughulikiwe kwa nguvu ya umma na si mahakama. kwenda mahakamani ni kuwapa ujiko tu hawa mbuX2.

Taratibu mtatia akili na kujua mlikosea wapi!

 
Ukweli ni kwamba Kikwete na ccm yake hawaitakii nchi hii mema. Hayo wanayofanya sio tofauti na anavyofanya Gbagbo wa Ivory coast kwani wote wanawanyima haki yao wananchi wao. Kikwete should watch out Ocampo aliyekutana nae Kampala anaweza kuwa ndio anamtayalishia makao huko Hague waliko wakina Taylor ambao walikuwa marais kama yeye!! Kikwete na serikali yako hamuwezi kutuua kama kuku anyamore na mkawa huru!!
 
UCHAGUZI wa Meya na Naibu wa Manispaa ya Arusha umechukua sura mpya baada ya kuibuka vurugu zilizosababisha Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema, kukamatwa na Jeshi la Polisi na kupigwa hadi kupoteza fahamu na kulazwa katika Hospili ya mkoa huo Mount Meru.Vurugu hizo zilizodumu kwa takribani saa sita, zilisababisha askari wa Kikosi cha Kuzuia Ghasia(FFU) kutumia mabomu ya machozi pamoja na maji ya kuwasha kuwatawanya maelfu ya wafuasi na wapenzi wa Chadema waliokuwa wamezingira ofisi za Manispaa hiyo na kufunga kwa muda Barabara ya Mkuu wa Mkoa na ya New Arusha Hotel.


Vurugu hizo zilibuka baada Lema pamoja na madiwani wa Chadema kufika katika ofisi ya Manispaa hiyo, kupinga kufanyika kwa uchaguzi huo ambao uliitishwa na kinyemela bila kuwashirikisha madiwani wa chama hicho.

Uchaguzi huo umedaiwa kufanyika kwa kuwashirikisha madiwani na wabunge wa CCM na wa TLP wawili ambao walimchagua Diwani wa Kata ya Olorien (CCM), Gaudence Lyimo, kuwa Meya na naibu Meya wake Michael Kivuyo ambaye ni Diwani wa Kata ya Sokoni kwa tiketi ya TLP.

Kufuatia hali hiyo baadhi ya askari wa jeshi polisi waliokuwepo eneo hilo wakiwa wamevalia zana mbalimbali za kutuliza ghasia, walimzuia mbunge huyo kuingia ndani huku wakimwamuru atoke nje ya eneo hilo.

Alipokataa askari hao walianza kumpa kipigo na kusababisha kupoteza fahamu kwa dakika saba kisha wakampakia katika gari lao hadi Kituo Kikuu cha Polisi mjini Arusha na kumweka rumande.

Hali hiyo ilisababisha mamia ya wanachama na wafuasi wa chama hicho kujikusanya na kukizingira kituo hicho, huku wakiwatuhumu polisi kujiingiza katika masuala ya siasa ya kuisaidia CCM.


Majira ya saa 9 Alasiri, mbunge huyo aliachiwa kwa dhamana na kurejea katika ofisi za Manispaa akiwa na kundi kubwa la wafuasi wa Chadema ambao walikuwa wakirusha maneno makali huku wengine wakitishia kuchoma moto ofisi ya manispaa.

Katika ofizi hizo, FFU waliibuka tena na kurusha mabomu ya machozi pamoja na maji ya kuwasha, hali iliyosabisha Lema ambaye alikuwa akizungumza na madiwani wa Chadema kukimbia kisha kuanguka na kupoteza fahamu kwa dakika kama tano na kukimbizwa katika Hopitali ya Mount Meru kwa matibabu zaidi.

Mwananchi Jumapili ilishuhudia jana jioni Lema akiwa amelazwa katika moja ya wodi katika hospitali ya Mount Meru akiwa na mkewe.

Wakati Lema akiwa amelazwa katika wodi hiyo umati mkubwa wa wafuasi wa Chadema ulikuwa umetanda nje ya hospitali hiyo wakisubiri kujua hatima ya afya ya mbunge wao.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Tobias Adengenye alikiri kutokea kwa tukio hilo na kwamba kukamatwa kwake kunatokana na Lema kukaidi amri ya polisi.

Awali Lema aliliambia Mwananchi Jumapili kuwa kipigo alichopata, kilimsababisha matatizo ya mbavu pamoja na mkono wa kulia kuumia.

"Pamoja na mambo mengine, nina maumivu makali sana katika sehemu za mbavu pamoja na mkono wa kulia," alisema Lema.

Kiongozi wa kambi ya upinzani Arusha ambaye ni Diwani wa Chadema, Kata ya Elerai, John Bayo, aliwaambia waandishi wa habari kuwa wanatarajia kwenda mahakamani kesho (Desemba 20) kufunuga kesi kupinga uchaguzi huo kutokana na baadhi ya kanuni kutofuatwa.

Bayo alifafanua kwamba mojawapo ya kanuni iliyokiukwa ni kutozingatiwa kwa idadi ya theluthi mbili ambao ni madiwani 20 wenye mamlaka ya kumchagua meya na naibu wake.

Katika Manispaa hiyo, CCM ina jumla ya madiwani 14 huku Chadema ikiwa na jumla ya madiwani 16 huku TLP ikiwa na wawili.

"Jumatatu (kesho), tunaenda mahakamani kupinga uchaguzi huo, kwanza hatukupewa barua ya kuhudhuria uchaguzi leo baada ya jana kuhairishwa, lakini pili idadi yao haikutimia kumchagua meya na naibu wake kwani sheria inasema ni theluthi mbili itakamilisha uchaguzi, wao walikuwa 15," alisema Bayo.


Hata hivyo, uteuzi Diwani wa TLP wa Naibu Meya umezua utata kwa vile awali alikuwa akiwaunga mkono Chadema na kwamba hadi saa 5 asubuhi alikuwa katika mkutano wa madiwani wa upinzani.

"Alituaga kuwa anakwenda ndani ya ofisi za Manispaa kujua nini hatma ya uchaguzi, lakini hakurudi hadi tulipopata taarifa kuwa amechaguliwa kuwa Naibu meya,'' kilisema chanzo chetu.

Alipoulizwa kuhusiana na hali hiyo, Katibu wa Itikani na Uenezi wa CCM, John Chiligati alisema: "Uchaguzi si wa kinyemela unajulikana nchi nzima, lakini siwezi kuzungumza lolote kwa sasa kwa kuwa bado sijapata taarifa rasmi kuhusu hali hiyo".

Uchaguzi huo ulikuwa ufanyike juzi, lakini uliahirishwa na Msimamizi wa Uchaguzi, Estomi Chang'a ambaye pia ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Arusha kufuatia kutokea malumbano baada ya madiwani wa Chadema kupinga kitendo cha CCM kumteua, Mary Chatanda ambaye ni Mbunge wa Viti Maalumu mkoani Tanga na Katibu wa CCM mkoani Arusha kuwania nafasi hiyo ya umeya.

Sababu nyingine ni kambi ya upinzani kupinga kitendo cha msimamizi wa uchaguzi kumzuia Diwani wa viti maalumu wa TLP, Mwamvua Wahanza kutopiga kura kwa madai ya kutothibitishwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec).

Katika hatua nyingine, askari waliokuwa wakilinda ofoso manispaa hiyo waliwazuia baadhi ya waandishi wa habari kuingia ndani kwa madai kuwa hawana mwaliko rasmi huku isipokuwa mwandishi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Leornad Manga.

Pamoja na waandishi kuwasomea kanuni za kudumu za mikutano na shughuli za manispaa, walikataliwa kuingia.

Juhudi za kumpata Mkurugenzi wa Manispaa ya Arusha, Chang'a kuzungumzia suala hilo zilishindikana kutokana na simu yake ya mkononi kushindwa kupokelewa hadi tunakwenda mtamboni.

Alipoulizwa kuhusu hali hiyo, Mwasisi wa Chadema, Edwin Mtei aliiambi Mwananchi Jumapili jana kuwa analaani sana kitendo hicho cha kukamatwa mbunge wao na kwamba kinaonyesha wazi kuwa CCM bado imechaganyikiwa kutokana na kupoteza majimbo mengi katika uchaguzi mkuu.

Jambo la kushangaza uchaguzi wa mameya umekuwa na matatizo makubwa katika maeneo yote ambayo upinzani una madiwani wengi huku wakurugenzi wa halmashauri hizo, ambao ndiyo wasimamizi kwaikidaiwa kuhusika kupanga njama za kukipendelea Chama Cha Mapinduzi kwa kukiuka taratibu.

- Well, wakuu hivi kweli tunazo all the facts za hili tukio I mean nini kazi ya FFU kisheria?

William.
 
Huuyu Andengeye amefika hapo kwa kubebwa .....u RPC alipewa enzi za mahita ..kisa alikuwa msaidizi maalum wa mahita...mahita alipoona anakaribia kustaafu akampandisha vyeo haraka haraka kufikia hapo alipo......wenzake wenye elimu moja na uwezo sawa bado wanasota ..walioenda sana wamefikia u OCD.

Kitendo kilichofanyika Arusha sio uungwana kabisa ....kwa namna yeyote ile kiongozi wa umma...kuna utaratibu wake wa kumkamata ndio maana yule OCD aliyepewaga amri amkamate mbunge wa simanjiro ...na mkuu wa mkoa hakuitekeleza kwa kuwa kuna utaratibu wa kumkamata kiongozi ,....sio kwa kumpiga.....hiii ilikuwa inahatarisha maisha ya wote waliokuwapo hapo kwa OCd kukosa busara...wewe fikiria wananchi wangeamua kuchoma moto jengo la manispaa ,nani angebakia????

Yakitokea haya kikwete alikuwa umbali mfupi toka hapo city council kwenye ikulu ya Arusha..alienda arusha kufungua hoteli ya mount meru......kwanini watu wasiamini kuwa haya yoote yana baraka za rais........kwani kuna ubaya gani CHADEMA wakiongoza halmashauri arusha mbona wameshafanya hivyo maeneo mengine kwa amani...

nadhani sasa mtagundua tishio la kuvunjika amani linaletwa na nani .....amani inatishiwa tu pale CCM inapoelekea kushindwa....sasa siku wakishindwa urais si watauwa watu hawa???
Mbona mwaka huu walishindwa? Ni busara tu za Dr Slaa zimewezesha amani kuwepo!! Mbali na majina yote ya ukoo ya CCM kama vile Mafisadi, Majambazi, Wauwaji, Wasani, Waroho wa Madaraka kutaja tu machache lakini pia ni genge la wahuni linalojali maslahi ya wachache.
 
well...tusubiri hiyo mahakama itasemaje. Kama sheria inasema idadi ni 2/3 na haikufika hiyo...jibu ni simple...huyo Meya hawezi kusimama.
hii itakuwa ishu ikiwa mahakama itagoma kwenye hii ishu!

Kwa wajuzi wa sheria, je kuna uwezekano kuweka zuio kwa mayor huyo kuapishwa (kama bado) au kumzuia kutenda kazi za mayor (kama kesha apishwa). Iwapo mahakama haitatoa haki iliyo wazi basi CDM wamwapishe mayor wao mbona Ivory Coast kuna marais wawili?

Sitashangaa kusikia kuwa madiwani wa TLP wameshikishwa noti ndefu kuhama alliance! Na kama hilo ni kweli basi chama cha upinzani Tz ni kimoja na kinajulikana
 
...nauliza wanaojua....m'bunge wa viti maalum tanga lakini ni katibu wa ccm wilaya ya arusha ana haki ya kuingia na kupiga kura kwenye baraza la madiwani arusha? Sababu ya kwamba ofisi yake ya kazi ipo arusha inatosha? Je kama baada ya kupiga kura jana arusha mjini, leo akahamishwa na kuwa katibu wa ccm wilaya ambayo bado haijachagua meya,je atapiga tena? Je huku tanga anaweza kupiga kura? Mary chitanda kama damu itamwagika hapo arusha mjini itakuwa juu ya kichwa chako. Katibu mkuu wa ccm wilaya ana ulinzi gani?
 
Iko siku wote wataelemewa sio Polisi, Jeshi, Magereza,Mgambo, FFU(Polisi), Usalama wa Taifa . Siku hiyo itakuwa ni kilio na kusaga meno kwa CCM na wale wote wenye kuleta udini kama ajenda ya kisiasa ktk nchi ya Tanzania
 
Jambo la msingi ni wananchi kuelewa kuwa wasikubali kuyumbishwa na CCM ikiwezekana 2015 kuwaondoa kabisa hawa CCM maana ndio wanaotaka damu imwagike nchi hii.

Hivi hawa jamaa wanafikiri bado tuko karne ya 19 wakati wa kulazimishana hata kama hatutaki.


Peoples power
 
- Well, wakuu hivi kweli tunazo all the facts za hili tukio I mean nini kazi ya FFU kisheria?

William.

yani unataka kusema kazi ya FFU ni kupiga wananchi?
Leo hii kuna polisi yeyote anayeweza kuja kukupiga hapo NY kwa vile yeye ni polisi wa kutuliza ghasia?
hawa polisi wamezidi sasa na imefika muda muafaka wa kuwarudisha katika nafasi yao...
 
Back
Top Bottom