Crashwise
JF-Expert Member
- Oct 23, 2007
- 22,227
- 8,735
MAMIA ya wakazi wa Jiji la Arusha leo wanatarajia kujitokeza kwenda Mahakamani kusikiliza kesi inayowakabili vigogo wa Chadema, wakiongozwa na Mweyekiti wa chama hicho Taifa, Freeman Mbowe na Katibu mkuu, Dk Wilbrod Slaa.
Viongozi hao wa chadema , wakiwepo pia wabunge watatu, Philemon Ndesamburo (Moshi mjini), Joseph Selasini (Rombo) na Godbless Lema (Arusha mjini) na wafuasi wengine 24 wanakabiliwa na kesi ya kufanya mkusanyiko usio halali Januari 5 mwaka huu.
Kesi hiyo, inayosikilizwa na hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Mkoa Arusha, Charles Magesa imekuwa ikihudhuriwa na mamia ya watu hatua ambayo husababisha ulinzi kuimarishwa mahakamani.
Katika kesi hiyo, washitakiwa hao, wanatetewa na Mawakili, Method Kimomogoro na Abert Msando wakati upande wa mashitaka unaongozwa na mwanasheria wa serikali Zakaria Elisaria na wenzake.
Kwa mara ya kwanza leo, Mchumba wa Dk Slaa, Josephine Mushumbusi anatarajiwa kuungana na washitakiwa wengine mahakamani baada ya kukosekara mara mbili kutokana na ugonjwa.
Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba pia anatarajiwa leo kuunganishwa na watuhumiwa wengine katika kesi hiyo baada ya kukamatwa hivi karibuni na polisi na kushitakiwa kwa kosa hilo moja la kufanya mkusanyiko usio halali.
Washitakiwa wote wapo nje kwa dhamana, kesi hiyo ilitokana na maandamano waliofanya wafuasi wa Chadema, kupinga uchaguzi wa Meya wa Jiji la Arusha, Gaudence Lyimo (CCM) ambapo Chadema wamekuwa wakidai alichaguliwa kinyume cha taratibu.
Katika maandamano hayo, watu watatu waliuawa kwa kupigwa risasi na polisi na wengine zaidi ya 30 kujeruhiwa kwa risasi baridi na moto.
Source: Mwananchi