CHADEMA, Kikwete uso kwa uso 27th Nov 2011

Status
Not open for further replies.
Tujiulize kama CDM wangeamua kunyamaza kimya nini kingetokea au nini kingeharibika? huko ikulu wanakwenda kwa faida ya nani? Kwa nini vyama vingine havija enda ikulu hata baada ya kuushauriwa viende ?
 
Cdm mwambieni huyo kama yamemshinda ajiuzulu mlango uko wazi
 
Leo Rais Jakaya Mrisho Kikwete anakutana na ujumbe na viongozi wa CHADEMA ikulu kwa mazungumzo ya kujadili muswada uliopitishwa na Bunge ambapo wabunge wa chadema walitoka nje eti hawaukubali.

wakati waliishawahi kutoka ndani ya bunge kwa hoja eti hawatambui mchakato uliomuweka madarakani Rais, ndipo Rais kikwete aliwaambia "Mtatoka mtaenda mtarudi hakuna Rais wa JMT ila ni mimi na Dkt Ally mohamed shain ndio Rais SMZ na Maalim seif sharif Hamad ni ndio Makamu wa kwanza wa Rais, Seif idd ni makamu wa pili wa Rais, kwa hiyo ili mambo yenu yawanyookee ni lazima mje kwangu"

Kwa maneno hayo ya Rais kikwete, Je viongozi wa chadema wamekwenda kwa ajili ya kutengeneza mambo yao? kama ni hivyo je ni nini hatma ya Chadema?

nafikiri kama alivyonena J Mtatiro kwamba wanaenda kutengeza mazingira ya kua CCM A.
 
Update ya kikao ni muhimu ila isiwe kama juzi kwenye NEC ya CCM, maana watu walikuwa wanakurupuka tu kututupia matango pori na taarifa za ajabu ajabu humu.

Lakini pia umesahau kutuwekea source hapa.

Hujasoma pale chini kasema Mwananchi
 
Nilivyoelewa tamko la Ikulu jioni ya j'mosi ni kuwa Rais hatotoa msimamo wa kukubali maoni ya CDM leo bali ataendelea kukutana na watu wengine (vyama vy aupinzani n.k) na ninategemea kuwa atatoa kauli yake pale atakapotia sahihi mswada kuwa mswada utakuwa sheria lakini utarudishwa tena Bungeni ili ufanyiwe mabadiliko na hivyo kimsingi kuzizima hoja za wapinzani kwani bila wabunge wa CCM kukubaliana na mabadiliko hayo au makubwa inavyotakiwa sheria itabakia kwa kiasi kikubwa jinsi ilivyo.
 
Kuna nyimbo 3 za Prof. Jay zinaendana na hali halisi. ilianza NDIYO MZEE, ikafuata KIKAO CHA DHARARU na mwishowe ..... NANG'ATUKA!
 
Kuna thred ilisema kikwete rais anaekula meza moja na kunywa kahawa na wabaya wake,analipa ubaya kwa wema.nampongeza kikwete kwa kukubali kucheka na wale wanaomchukia,wanaomtukana,wanaomkejeli kila siku.
 
Tunaomba kikao chao kiwafikirie watanzania zaidi na si manufaa yao ya kisiasa wala kutafuta nani kamshinda mwenzie kwenye kikao.
MUNGU IBARIKI AFRIKA MUNGU IBARIKI TANZANIA
 
Naombea mazungumzo yaende vema kwa mstakabali mwema wa taifa letu hususani issue ya mchakato wa kupata katiba mpya. Napongeza pande zote mbili yaan CDM na President kwa kuchagua njia ya majadiliano ambayo mimi naamini ndiyo njia bora ya kupata muafaka wa pamoja. Mungu ibariki Tanzania....
 
Kile kikao kilichoombwa na CHADEMA kukaa na JK kuzungumza kuhusu katiba mpya hatimaye leo kitafanyika.

Habari zinaendelea kudadavua kuwa kikao hicho kitahusisha ujumbe wa CHADEMA na JK na forum yake huku vyama vingine vya siasa kutokuwepo tofauti na ilivyopendekezwa na NEC ya CCM ambayo inaongozwa na JK.

Jamani pindi kikao kikianza kwa yeyote atakayepata kinachoendelea kikaoni atujuze. Naomba kuwasilisha.
:spy:

Source; Mwananchi newspaper
Mi ninachoweza kusema ni kwamba timu ya CDM iwe makini sana na ile sumu inayoitwa 'POLINIUM 310'. Pia wasikubali kikao kiendelee hadi usiku wa manane maana muda huo ukifika mtu akisinzia tu anadondoshewa kwenye glasi ya maji ya kunywa then unaanza kusikia mara flani ngozi yake inababuka mara kapelekwa Muhimbili, Mara imeshindikana wanampeleka India.

Chonde chonde Dk Slaa. Nataka nikuone ukiapishwa 2015 kama rais wangu na sio kusikia unaumwa umwa baada ya kuhudhuri hicho kikao.
 
walishazoea kusema kuwa njia bora ni kutoka nje,, sasa wanaingia ikulu kufanyanini? Ni genge la kihuni linalotumia mgongo wa siasa kupotosha umma, maana ni wa2 wasikuwa na maadili, wasioheshimu viongozi wenzao,wanadharau police, mahakama, jeshi , tume ya uchaguzi na kila ki2, kuwa na wanasheria kibao kwenye chama chao ndo wanatufumbia macho kuwa kigezo cha kututetea?

Wasijidanganye kwa kuwa na washabiki wengi lakini kama hawawaelezi ukweli na dhamira yao ipo cku watatupwa kama umbwa na kuwasahau palepale.
 
Mi ninachoweza kusema ni kwamba timu ya CDM iwe makini sana na ile sumu inayoitwa 'POLINIUM 310'.

Pia wasikubali kikao kiendelee hadi usiku wa manane maana muda huo ukifika mtu akisinzia tu anadondoshewa kwenye glasi ya maji ya kunywa then unaanza kusikia mara flani ngozi yake inababuka mara kapelekwa Muhimbili, Mara imeshindikana wanampeleka India.

Chonde chonde Dk Slaa. Nataka nikuone ukiapishwa 2015 kama rais wangu na sio kusikia unaumwa umwa baada ya kuhudhuri hicho kikao.

..."Mimi hapa sina rahaa e naumia na mawazo...”Na:Sam wa Ukweli.
 
Hiyo ni mbinu ya kisiasa kuonana na JK, wanajua fika hawezi kubadili msimamo. Baada ya hapo then wanakuja kumshitaki kwa waajiri wake sisi wenyenchi ndio tuamue kusuka au kunyoa
 
Baada ya hapo sitaki kusikia tu ooh! fulani anaumwa anakimbizwa India (fare play inatakiwa)

Hicho usichotaka kukisikia ... Kuna uwezekano mkubwa ukakisikia! Jk ana unresolved conflicts za Magamba jumlisha hizo za katiba! If by any chance he miscalcalculate on this one .... Mkuu you hav no optiön and likely you wil have to face the unwanted! These types of conflicts when has deeply internalised they can to great extent compromise the immunity and hence ... .
 
Leo Rais Jakaya Mrisho Kikwete anakutana na ujumbe na viongozi wa CHADEMA ikulu kwa mazungumzo ya kujadili muswada uliopitishwa na Bunge ambapo wabunge wa chadema walitoka nje eti hawaukubali.

wakati waliishawahi kutoka ndani ya bunge kwa hoja eti hawatambui mchakato uliomuweka madarakani Rais, ndipo Rais kikwete aliwaambia "Mtatoka mtaenda mtarudi hakuna Rais wa JMT ila ni mimi na Dkt Ally mohamed shain ndio Rais SMZ na Maalim seif sharif Hamad ni ndio Makamu wa kwanza wa Rais, Seif idd ni makamu wa pili wa Rais, kwa hiyo ili mambo yenu yawanyookee ni lazima mje kwangu"

Kwa maneno hayo ya Rais kikwete, Je viongozi wa chadema wamekwenda kwa ajili ya kutengeneza mambo yao? kama ni hivyo je ni nini hatma ya Chadema?
Next tyme tumia kichwa kufikiri. CDM hawaendi kumwona ili mambo yao yanyooke, wanakwewnda pale kwa mustakabali wa Taifa.
 
Tatizo la CDM violence iko kama one of the options. Chama chochote makini kinachojali maslahi ya Umma hakiwezi kutumia violence na kutishia mara kwa mara kwenda porini, etc.

Nyerere alidai Uhuru wa nchi hii kwa wenye nguvu kuliko CCM na hakumwaga damu. Hatuwezi kukubali chama kinachotaka kujenga utamaduni wa kumwaga damu ambao hatuna.

walishazoea kusema kuwa njia bora ni kutoka nje,, sasa wanaingia ikulu kufanyanini? Ni genge la kihuni linalotumia mgongo wa siasa kupotosha umma, maana ni wa2 wasikuwa na maadili, wasioheshimu viongozi wenzao,wanadharau police, mahakama, jeshi , tume ya uchaguzi na kila ki2, kuwa na wanasheria kibao kwenye chama chao ndo wanatufumbia macho kuwa kigezo cha kututetea?

Wasijidanganye kwa kuwa na washabiki wengi lakini kama hawawaelezi ukweli na dhamira yao ipo cku watatupwa kama umbwa na kuwasahau palepale.
 
Katiba imekuwa ikiimbwa kwa miaka mingi na makundi, watu mbalimbali. Jamii imekuwa ikiamini katiba iliyopo haiifanyi jamii kuwa huru na kutumia rasilimali za nchi kujiendeleza. Ukiongea na wasomi, wana siasa, vikundi visivyo vya kiserikali, madhehebu ya dini wanachama wa vyama vya siasa wote wanakubali katiba yetu ni mbovu na tunahitaji katiba mpya.

CDM walipoona hawawezi kusikilizwa Bungeni walijitahidi kutafuta mbinu nyingine ya kuweza kusikilizwa na mawazo yao kufanyiwa kazi, moja ilikuwa kupeleka kilio cha katiba na ubovu wa mswada uliyoundwa wa kupata katiba mpya kwa wananchi.

CDM wameamua kukutana na raisi wa Jamhuri ya Muungano ambaye ni mwenyekiti wa chama cha mapinduzi ambaye wabunge wa chama chake wote wamepitisha mswada wa katiba unaopigiwa kelele na wengi kwenye jamii. Mwenyekiti huyu ameonyesha kushindwa kwa kiasi kikubwa kuweka chama chake kwenye mstari wakati huu kinapokabiliwa na migogoro mikubwa ya makundi na vita vya uraisi kupitia chama hicho ya 2015. Raisi JK ameonyesha kushindwa kabisa kuwajibisha wasaidizi wake wanaotuhumiwa kila kukicha kuibia nchi au kutoa maamuzi angamizi.

Leo CDM wanakutana na Raisi JK tutegemee nini?
Lugha ya kisanii isiyo na maamuzi.
Kupoteza muda wa wananchi na fedha za wananchi kwani hakuna makubaliano ya kitaifa yenye nia ya kunusuru janga la katiba mbovu.
Lugha za kejeli atakapoita wazee wake wa Dar kuwaeleza nini msimamo wake.
Hataona kwamaba katiba mpya nzuri sio kwa faida yake wala hao viongozi wa CDM bali ni kwa faida ya vizazi vya sasa na vijavyo.

CDM wanapaswa kutumia busara za kutosha, na ninawasihi wawe tayari kutoka ikulu bila ya kusikilizwa kwani hulka za Jk ni kumridhisha kila mtu akiwa naye kwa wakati huo bila ya utekelezaji wowote ambao utatokea. JK na serikali yake hawana kitengo cha utafiti kabla ya maamuzi.

Nawashauri CDM watambue kuwa nchi za Misri , Tunisia, Libya, Zaire, Kenya Syria nk zilikuwa na katiba zilizowanufaisha watala kwa asilimia mia, ila wananchi walipokataa hazikuwasaidia chochcote. CDM wawekeze kwenye elimu ya raia kujua haki zao na wajibu wa serikali kwa wananchi wake. Waongeze ushiriki wa vijana kutambua haki zao, wajenge misingi imara kwa vijana na kupenyeza vijana wengi polisi, usalama wa taifa, jeshini, nk hii iwe ni long term plan.

Haki za raia na wajibu wa raia kwa serikali yake, na haki ya serikali kwa raia. Raia wajue wanawajibu wa kulipa kodi na raia wajue kodi yao inahaki ya kuwahudumia. Halafu mapambano ya kudai haki hizi za msingi ni haki za raia , Tanzania haiwezi kuzuia watu wake kutaka haki zao za msingi, hatuna polisi wa kupambana na raia wakiamua kutafuta haki zao.

Ili haya yafanikiwe tunahitaji wapambanaji wa kweli wasioogopa vitisho na hujuma za vibaraka wachache. Kama tuliweza kumtoa mkoloni na silaha zake zote hatuwezi kushindwa hawa wakoloni ndugu zetu.

Mkutano wa JK na CDM hauwezi kuleta tume huru ya katiba Tanzania.
 
Leo ndiyo kikao kati ya JK na kamati iliyoundwa Chadema ili kumshauli Rais asi sign Mswada wa sheria ya katiba mpya Je inawezekana JK kukubaliana na mawazo ya chadema akadharau wabunge wa CCM na Cuf walioupitisha bungeni?

Naomba mawazo yenu wapendwa wana JF
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom